KLABU ya Everton
imetangaza kuwa itakata rufani kufuatia kadi nyekundu aliyopewa nyota
wake Darron Gibson katika mchezo ambao walishinda mabao 2-1 dhidi West
Ham United. Kiungo
huyo wa zamani wa Manchester United alitolewa na mwamuzi Anthony Taylor
aliyechezesha mchezo huo kwa kumchezea vibaya Mark Noble wa West Ham
katika dakika za majeruhi. Mshambuliaji
wa West Ham Carlton Cole naye alitolewa nje mapema kutokana na tukio
kama hilo alilofanya kwa beki wa Everton Leighton Baines. Rufani
hiyo hiyo kama ikifanikiwa itamaanisha kuwa Gibson ambaye ni raia wa
Jamhuri ya Ireland ataweza kucheza katika mchezo dhidi ya Wigan Athletic
utakaochezwa katika siku ya maboksi Desemba 26.
No comments:
Post a Comment