Thursday, December 13, 2012

MAANDALIZI YA PAMBANO LA CHEKA NA MMLAWI CHIMWEMWE YAKAMILIKA


MAANDALIZI la pambano la Francis Cheka na bondia Chiotka Chimwemwe toka Malawi litakalochezwa Desemba 26 mwaka huu kwenye uwanja wa Sheikh Abeid Amani Karume jijini Arusha yamekamilika.

Akizungumza  jijini Dar es Salaam promota wa pambano hilo Andrew George amesema taratibu za mchezo huo umekamilika.

"Taratibu zote za pambano zimekamilika kwa asilimia 90 ikiwa pamoja na kumtumia tiketi bondia Chiotka Chimwemwe", alisema George.

George alisema ameamua kulipeka pambano hilo Arusha kwa kuwa anaamini watu wa Arusha wanapenda ngumi na siku hiyo ni siku ya sikukuu hivyo watakuj kwa wingi pamoja na familia zao kwani pambano litaanza saa nane mchana.

Pia alisema mabondia watapima uzito siku ya sikukuu ya krismasi jijini Arusha.

Pambano hili litakuwa ni la raundi 12 na Mmalawi huyu anajigamba atampiga Cheka ndani ya ardhi ya nchi yake hivyo kuwasihi watanzania kuja kwa wingi kwani hata ulinzi utakuwepo wa kutosha, alisema George
WAKENYA KUCHEZESHA MECHI YA STARS, ZAMBIA

 Mwamuzi Sylvester Kirwa kutoka Kenya ndiye atakayechezesha mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Taifa Stars na mabingwa wa Afrika, Zambia (Chipolopolo) itakayofanyika Desemba 22 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kirwa anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) atasaidiwa na Elias Wamalwa na Marwa Range. Waamuzi hao wasaidizi ambao vilevile watatoka Kenya pia wanatambuliwa na FIFA.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari iko kambini hoteli ya Tansoma, na inafanya mazoezi katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na ule wa Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake.


MTIBWA SUGAR YAICHAPA TOTO 3-1 KOMBE LA UHAI


Mtibwa Sugar ya Morogoro leo asubuhi (Desemba 14 mwaka huu) imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Toto Africans ya Mwanza katika mechi ya michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U20) za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom.
Juma Luzio alifunga mabao yote matatu (hat trick) katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam. Alifunga mabao hayo dakika za 44,81 na 88.
Hata hivyo, Toto Africans ndiyo walioanza kufunga katika mechi hiyo ya kundi A. Bao hilo katika michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Said Salim Bakhresa kupitia maji Uhai lilifungwa dakjika ya 22 na Pastol Makula.
Nayo Simba imenguruma baada ya kuitandika Mgambo Shooting ya Tanga katika mechi nyingine ya michuano hiyo iliyochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi. Wafungaji kwa washindi walikuwa Ramadhan Mdoe dakika ya 19, Mohamed Salum dakika ya 77 na Ramadhan Singano dakika ya 89.
Michuano hiyo inaendelea leo mchana na jioni. Mechi ya Ruvu Shooting na Kagera Sugar iliyokuwa ichezwe mchana Uwanja wa Azam, Chamazi sasa itafanyika saa 10 kamili jioni katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Mechi nyingine za leo ni Coastal Union vs JKT Ruvu (mchana- Karume), African Lyon vs Azam (jioni- Chamazi). Vilevile mechi kati ya JKT Oljoro na Yanga inachezwa leo Uwanja wa Chamazi.
Kesho (Desemba 15 mwaka huu) ni mapumziko, na michuano hiyo itaendelea Jumapili kwenye viwanja vyote viwili- Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na Uwanja wa Azam- Chamazi.

MSIMAMO WA UHAI CUP KUNDI C, JKT OLJORO VINARA
















TANZANIA FOOTBALL FEDERATION
STANDING UHAI CUP 2012














NO TEAMS P W D L GF GA GD PTS YLW RED TOTAL
1 KAGERA SUGAR 1 0 0 1 0 3 -3 0



2 JKT OLJORO 2 2 0 0 6 2 4 6



3 YANGA S. C 2 0 1 1 2 3 -1 1



4 RUVU SHOOTING 1 0 1 0 0 0 0 1





3 1 1 1 8 8 0 8 0 0 0

MSIMAMO WA UHAI CUP KUNDI B, SIMBA YASHIKILIA USUKANI
















TANZANIA FOOTBALL FEDERATION
STANDING UHAI CUP 2012














NO TEAMS P W D L GF GA GD PTS YLW RED TOTAL
1 AFRICAN LYON 2 1 0 1 5 2 3 3



2 POLISI MOROGORO 2 1 0 1 1 4 -3 3



3 AZAM FC 2 1 0 1 2 1 1 3



4 JKT MGAMBO 2 0 0 2 0 5 -5 0



5 SIMBA S.C 2 2 0 0 5 1 4 6

















MSIMAMO WA UHAI CUP KUNDI A COASTAL UNION YAONGOZA




























TANZANIA FOOTBALL FEDERATION
STANDING UHAI CUP 2012













NO TEAMS P W D L GF GA GD PTS YLW RED TOTAL
1 COASTAL UNION 2 2 0 0 5 2 3 6


2 TZ PRISONS 2 0 0 2 1 3 -2 0


3 JKT RUVU 2 1 0 1 2 3 -1 3


4 MTIBWA SUGAR 2 2 0 0 6 2 4 6


5 TOTO AFRICAN 2 0 0 2 2 6 -4 0
















PONGEZI KWA UONGOZI MPYA DRFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaupongeza uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika juzi (Desemba 12 mwaka huu) hoteli ya Mbezi Garden.
Ushindi aliopata Almasi Kasongo aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti pamoja na wajumbe wengine wa Kamati ya Utendaji unaonesha jinsi ambavyo wajumbe wa Mkutano Mkuu wa DRFA walivyo na imani kwao.
TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya DRFA ambayo hivi sasa ina kinara mpya, na kwamba ina changamoto kubwa ya kuhakikisha inaendesha shughuli za DRFA kwa kuzingatia katiba na kanuni.
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA chini ya Juma Simba na Kamati ya Uchaguzi ya TFF inayoongozwa na Deogratias Lyatto kwa kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa utulivu na kwa kuzingatia katiba na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Safu mpya ya uongozi wa DRFA inaundwa na Kasongo (Mwenyekiti), Meba Ramadhan (Makamu Mwenyekiti), Msanifu Kondo (Katibu), Muhsin Said (Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa TFF), Benny Kisaka (Mwakilishi wa Klabu), Ally Hobe (Mhazini) na wajumbe Mohamed Shabani, Sunday Mwanahewa na Bakari Mapande.


CAF KUFANYA UKAGUZI WA ‘LESENI ZA KLABU’ JANUARI


Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litatuma ofisa wake nchini mwezi ujao kwa ajili ya kufanya ukaguzi kwenye klabu za Ligi Kuu ya Tanzania kabla ya kutoa leseni kwa zile ambazo zitakuwa zimekidhi vigezo vilivyowekwa. Ili klabu ishiriki mashindano ya CAF ni lazima iwe na leseni hiyo.
Kwa mujibu wa CAF, ofisa huyo atakuwa nchini kuanzia Januari 7 mwakani ambapo atafanya ukaguzi huo hadi Januari 14 mwakani. Mbali ya ukaguzi katika klabu, pia ofisa huyo atakagua viwanja vitakavyotumika katika mashindano yake na hoteli ambazo timu kutoka nje zitakuwa zinafikia kabla ya mechi.
Baadhi ya masharti kabla ya klabu kupewa leseni ya CAF ni pamoja na kuwa na ofisi (physical address), uwanja wake wa mazoezi, programu ya maendeleo kwa vijana, sekretarieti ya kuajiriwa, hesabu za fedha zilizokaguliwa (audited accounts) na benchi la ufundi linaloundwa na watu wenye sifa zinazostahili.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
 

CAF YATUMA MTU KUJA KUZIKAGUA SIMBA NA AZAM KAMA ZINA VIGEZO VYA KUCHEZA AFRIKA

Simba SC
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) litatuma ofisa wake nchini mwezi ujao kwa ajili ya kufanya ukaguzi kwenye klabu za Ligi Kuu ya Tanzania kabla ya kutoa leseni kwa zile ambazo zitakuwa zimekidhi vigezo vilivyowekwa. Ili klabu ishiriki mashindano ya CAF ni lazima iwe na leseni hiyo.
Kwa mujibu wa CAF, ofisa huyo atakuwa nchini kuanzia Januari 7 mwakani ambapo atafanya ukaguzi huo hadi Januari 14 mwakani. Mbali ya ukaguzi katika klabu, pia ofisa huyo atakagua viwanja vitakavyotumika katika mashindano yake na hoteli ambazo timu kutoka nje zitakuwa zinafikia kabla ya mechi.
Baadhi ya masharti kabla ya klabu kupewa leseni ya CAF ni pamoja na kuwa na ofisi (physical address), uwanja wake wa mazoezi, programu ya maendeleo kwa vijana, sekretarieti ya kuajiriwa, hesabu za fedha zilizokaguliwa (audited accounts) na benchi la ufundi linaloundwa na watu wenye sifa zinazostahili.

TFF WAWAPA HEKO MABOSI WAPYA DRFA


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) linaupongeza uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika juzi (Desemba 12 mwaka huu) hoteli ya Mbezi Garden.
Ushindi aliopata Almasi Kasongo aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti pamoja na wajumbe wengine wa Kamati ya Utendaji unaonesha jinsi ambavyo wajumbe wa Mkutano Mkuu wa DRFA walivyo na imani kwao.
TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya DRFA ambayo hivi sasa ina kinara mpya, na kwamba ina changamoto kubwa ya kuhakikisha inaendesha shughuli za DRFA kwa kuzingatia katiba na kanuni.
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA chini ya Juma Simba na Kamati ya Uchaguzi ya TFF inayoongozwa na Deogratias Lyatto kwa kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa utulivu na kwa kuzingatia katiba na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Safu mpya ya uongozi wa DRFA inaundwa na Kasongo (Mwenyekiti), Meba Ramadhan (Makamu Mwenyekiti), Msanifu Kondo (Katibu), Muhsin Said (Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa TFF), Benny Kisaka (Mwakilishi wa Klabu), Ally Hobe (Mhazini) na wajumbe Mohamed Shabani, Sunday Mwanahewa na Bakari Mapande.

AZAM NDANI YA J.N.I.A. TAYARI KWA SAFARI YA KINSHASA

 Uhuru
 kutoka kulia Mwaikimba, Babbi na kocha wa makipa wa Kenya, Razzack Ssiwa wakikumbushia enzi zao walipokuwa Yanga, baada ya kukutana Airport leo
 Kipre Tchetche
 Jabir Aziz
 Kocha Stewart Hall 
Himid Mao anachaji simu 
Katibu wa Azam, Nassor Idrisa akiwa na Abubakar Makwisa mida hii ndani ya Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam tayari kwa safari ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kushiriki Kombe la Hisani, mashindano ambayo yanaanza leo
Wachezaji wapya wa Azam FC, Uhuru Suleiman na Seif Abdallah kwa nyuma, wakiwa ndani ya Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam mida hii tayari kwa safari ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kushiriki Kombe la Hisani, mashindano ambayo yanaanza leo mjini Kinshasa.


Wachezaji wanaingia ndani


Daktari wa Azam, Mjerumani Gomiz akiingia uwanja waq ndege


Kutoka kulia Zahor Pazi, Uhuru na Himid


Kutoka kulia Abubakar Mapwisa, Nassor na Abdi Kassim 'Babbi'


Msemaji wa Azam, Jaffar Iddi kulia katikati kipa wa zamani wa Simba na Yanga, Abdulamalik Nemes na Ofisa wa Azam FC, Jemedari Said nje ya uwanja wa Ndege

City ‘kujiliwaza’ St James Park? Man United wapo Old Trafford!!

BPL_LOGOLIGI KUU ENGLAND inaendelea Jumamosi kwa Mabingwa watetezi Manchester City kusafiri kwenda St James Park kuivaa Newcastle ikiwa ni Mechi yao ya kwanza tangu wapewe kipigo chao cha kwanza Msimu huu kwenye Ligi walipofungwa na Manchester United Bao 3-2 Uwanjani Etihad na Wababe Man United, baadae Siku hiyo hiyo, wao watakuwa nyumbani kucheza na Sunderland.
ZIFUATAZO NI DONDOO FUPI KUHUSU MECHI ZA WIKIENDI:
+++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi 15 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Newcastle v Man City
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Aston Villa
Man United v Sunderland
Norwich v Wigan
QPR v Fulham
Stoke v Everton
+++++++++++++++++++
Newcastle v Man City
Man City wanaingia kwenye Mechi hii wakiwa wametoka kupokea kipigo chao cha kwanza Msimu huu mikononi mwa Man United ambao ndio wapo kileleni na Man City kubakia nafasi ya pili Pointi 6 nyuma yao.
Lakini Man City wanakutana na Newcastle, Timu ambayo imefungwa Mechi 5 kati ya 6 za Ligi walizocheza mwishoni lakini tatizo hili hasa ni kukabiliwa na majeruhi kibao.
Kwa upande wa Man City, Wadau wengi huwa wanajiuliza ni kwa sababu gani Meneja wao huwa anampiga benchi Carlos Tevez na kumuanzisha Mario Balotelli ambae, mara nyingi, hucheza chini ya kiwango kama alivyoonyesha Jumapili iliyopita walivyochapwa 3-2 na Man United.

Liverpool v Aston Villa
Liverpool wameanza kuzinduka hasa baada ya kuichapa West Ham Mechi iliyopita walipocheza bila ya Mfungaji wao Luis Suarez aliekuwa kifungoni lakini kwenye Mechi hii na Aston Villa Suarez atarudi dimbani.
Aston Villa, baada ya kupata ushindi mnono wa Bao 4-1 hapo juzi walipoifunga Norwich City na kutinga Nusu Fainali ya CAPITAL ONE CUP, wataingia kwenye Mechi hii wakiwa na morali kubwa.

Man Unted v Sunderland
Sunderland walipata ushindi muhimu Jumanne iliyopita walipoitwanga Bao 3-0 Reading lakini Jumamosi  wanapambana na Vinara wa Ligi, Manchester United, ambao Jumapili iliyopita walipata ushindi mtamu wa ugenini walipowatwanga Mahasimu wao Man City Bao 3-2 na kuwapa kipigo chao cha kwanza Msimu huu na pia kuvunja rekodi ya City kutofungwa kwao Etihad kwa Miaka miwili.
Pia, Man United wana habari njema za kurudi Uwanjani kwa Nahodha wao Nemanja Vidic ambae alikuwa nje tangu Septemba 19 akiuguza goti lake.

Norwich v Wigan
Norwich watataka kufuta machungu ya kutwangwa Bao 4-1 wakiwa Uwanja huu huu wa nyumbani, Carrow Road, walipopigwa 4-1 na Aston Villa na kutolewa nje ya CAPITAL ONE CUP.
Lakini, Norwich wanakutana na Wigan isiyotabirika na lolote linaweza kutokea.

QPR v Fulham
Je hii itakuwa ni Mechi ambayo QPR watapata ushindi wao wa kwanza kwenye Ligi Msimu huu?
Tangu Meneja mpya Harry Redknapp aanze kuiongoza QPR wamecheza Mechi 3 na hawajafungwa na zipo kila dalili sasa wanacheza Kitimu kupita ilivyokuwa chini ya Meneja aliepita Mark Hughes.
Lakini, Fulham, ambao Jumatatu waliifunga Newcastle na kusimamisha wimbi lao la kufungwa mfululizo, si Timu rahisi.
Stoke v Everton
Stoke City ni wagumu na nguvu kazi wakicheza kwao lakini Everton, kama walivyoonyesha Wiki iliyopita walipopindua kuwa nyuma Bao 1-0 walipokuwa ugenini White Hart Lane na kuichapa Tottenham Bao 2-1 katika Dakika za majeruhi, ni Timu hatari.
Hii ni Mechi ngumu kuitabiri.
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumapili 16 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Tottenham v  Swansea
[SAA 1 Usiku]
West Brom v West Ham
+++++++++++++++++++++++
Tottenham v Swansea
Hii ni gemu ambayo lazima Tottenham washinde ikiwa kweli wanataka kumaliza Ligi wakiwa 4 bora hasa kwa vile Swansea City sio Timu yenye msimamo thabiti na huwa haitabiriki kama vile walivyofanya kwa kwenda ugenini na kuifunga Arsenal lakini waliporudi nyumbani Mechi iliyofuata wakachapwa na Norwich City.
West Brom v West Ham
West Brom wamefungwa Mechi 3 mfululizo hadi sasa lakini kipigo chao cha mwisho mikononi mwa Arsenal kilichangiwa na Arsenal kupewa Penati isiyostahili.
Wapinzani wa WBA ni West Ham ambao huwa ubwete kwa Mechi za ugenini ingawa katika Mechi zao za hivi karibuni wapinzani wao walikuwa baadhi ya Vigogo kama vile Spurs, Manchester United, Chelsea na Liverpool.
Hii ni Mechi tamu na yeyote anaweza kushinda.
Prediction: 2-1
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumatatu 17 Desemba 2012
[SAA 5 Usiku]
Reading v Arsenal
+++++++++++++++++++++++
Reading v Arsenal
Hii si Bigi Mechi lakini kwa Wadau wa Arsenal kwao ni Mechi muhimu mno hasa baada ya juzi kutupwa nje ya CAPITAL ONE CUP na Timu ya Daraja la 4 Bradford City na kuibua hali tete Klabuni kwao ikiwakumbusha sasa ni Miaka 8 tangu watwae Taji lolote.
Mara ya mwisho kukutana kwa Timu hizi, Arsenal walishinda Bao 7-5 kwenye CAPITAL ONE CUP.
+++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
[Kila Timu Mechi 16]
1 Man United Pointi 39
2 Man City 33
3 Chelsea 29
4 Everton 26
===============
5 Tottenham 26
6 WBA 26
7 Arsenal 24
8 Swansea 23
9 Stoke 23
10 Liverpool 22
11 West Ham 22
12 Norwich 22
13 Fulham 20
14 Newcastle 17
15 Sunderland 16
16 Southampton 15
17 Aston Villa 15
===============
18 Wigan 15
19 Readind 9
20 QPR 7

AFCON 2013: Ghana yateua Kikosi, Andre Ayew NDANI, Jordan Ayew NJE!


AFCON_2013_LOGOKocha James Kwesi Appiah ameteua Kikosi cha Wachezaji 26 cha Timu ya Taifa ya Ghana kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, zitakazoanza Januari 19 na kumalizika Februari 10, Mwaka 2013, huko Afrika Kusini lakini amewatenganisha Ndugu wawili, wote Wachezaji wa Marseille, Watoto wa Nguli Abedi Pele, kwa kumchukua Andre Ayew na kumuacha Jordan Ayew na vile vile kuchukua Wachezaji wanne tu wanaocheza Soka lao ndani Nchini Ghana.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
MAKUNDI:
KUNDI A: South Africa, Cape Verde, Morocco, Angola
KUNDI B: Ghana, DR Congo, Niger, Mali
KUNDI C: Zambia, Ethiopia, Nigeria, Burkina Faso
KUNDI D: Ivory Coast, Togo, Tunisia, Algeria
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Akionyesha kusikitika kwa kutochukuliwa, Jordan Ayew alisema: “Nimehuzunika lakini Marseille itafaidika mie kubaki Mwezi Januari. Nawatakia kila la heri Ghana na naomba Kaka yangu arudi Marseille Februari na Medali!”
Miongoni mwa Mastaa wa Ghana ni wale wanaocheza Ulaya ambao ni pamoja na John Paintsil, Christian Atsu, Kwadwo Asamoah na Anthony Annan, na pia yupo Asamoah Gyan ambae hivi sasa yupo na Klabu ya Al Ain, UAE, Falme za Nchi za Kiarabu.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Adam Kwarasey (Stromsgodset, Norway), Fatau Dauda (AshantiGold, Ghana), Daniel Adjei (Liberty Professionals, Ghana)
MABEKI: John Paintsil (Hapoel Tel-Aviv, Israel), Harrison Afful (Esperance, Tunisia), Mubarak Wakaso (Espanyol, Spain), Richard Kissi Boateng (Berekum Chelsea, Ghana), John Boye (Rennes, France), Jonathan Mensah (Evian, France), Isaac Vorsah (Red Bull Salzburg, Austria), Jerry Akaminko (Eskisehirspor, Turkey), Rashid Sumaila (Asante Kotoko, Ghana), Awal Mohammed (Maritzburg United, South Africa).
VIUNGO: Andre Ayew (Marseille, France), Christian Atsu (FC Porto, Portugal), Anthony Annan (Osasuna, Spain), Derek Boateng (Dnipro, Ukraine), Solomon Asante (Berekum Chelsea, Ghana), Emmanuel Agyemang Badu (Udinese, Italy), Kwadwo Asamoah (Juventus, Italy), Albert Adomah (Bristol City, England), Rabiu Mohammed (Evian, France)
MAFOWADI: Asamoah Gyan (Al Ain, UAE), Emmanuel Clottey (Esperance, Tunisia), Richmond Boakye Yiadom (Sassoulo, Italy), Yahaya Mohammed (Amidaus Professionals, Ghana)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
VIWANJA:
-Soccer City, Johannesburg [Mashabiki 94,700]
-Moses Mabhida Stadium, Durban [Mashabiki 54,000]
-Nelson Mandela Bay Stadium, Port Elizabeth [Mashabiki 48,000]
-Mbombela Stadium, Nelspruit [Mashabiki 41,000]
-Royal Bafokeng Stadium, Rustenburg [Mashabiki 42,000]
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi Januari 19
South Africa v Cape Verde Islands [Soccer City Saa 1 Usiku]
Angola v Morocco [Soccer City Saa 4 Usiku]
Jumapili Januari 20
Ghana v Congo DR [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Mali v Niger Nelson Mandela Bay Stadium 20:00
Jumatatu Januari 21
Zambia v Ethiopia [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Nigeria v Burkina Faso [Mbombela Stadium Saa 3 Usiku]
Jumanne Januari 22
Ivory Coast v Togo [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Tunisia v Algeria [Royal Bafokeng Stadium Saa 3 Usiku]
Jumatano Januari 23
South Africa v Angola [Moses Mabhida Stadium Saa 12 Jioni]
Morocco v Cape Verde Islands [Moses Mabhida Stadium Saa 3 Usiku]
Alhamisi Januari 24
Ghana v Mali [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Niger v Congo DR [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
Ijumaa Januari 25
Zambia v Nigeria [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Burkina Faso v Ethiopia [Mbombela Stadium Saa 3 Usiku]
Jumamosi Januari 26
Ivory Coast v Tunisia [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Algeria v Togo [Royal Bafokeng Stadium Saa 3 Usiku]
Jumapili Januari 27
Morocco v South Africa [Moses Mabhida Stadium Saa 2 Usiku]
Cape Verde Islands v Angola [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 2 Usiku]
Jumatatu Januari 28
Congo DR v Mali [Moses Mabhida Stadium Saa 2 Usiku]
Niger v Ghana [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 2 Usiku]
Jumanne Januari 29
Ethiopia v Nigeria [Royal Bafokeng Stadium Saa 2 Usiku]
Burkina Faso v Zambia [Mbombela Stadium Saa 2 Usiku]
Jumatano Januari 30
Algeria v Ivory Coast [Royal Bafokeng Stadium Saa 2 Usiku]
Togo v Tunisia [Mbombela Stadium Saa 2 Usiku]
ROBO FAINALI
Jumamosi Februari 2
Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
Jumapili Februari 3
Mshindi Kundi D v Mshindi wa Pili Kundi C [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi Kundi C v Mshindi wa Pili Kundi D [Mbombela Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
NUSU FAINALI
Jumatano Februari 6
Mshindi RF 3 v Mshindi RF 2 [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi RF 1 v Mshindi RF 4 [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
MSHINDI wa TATU
Jumamosi Februari 9
[Nelson Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
FAINALI
Jumapili Februari 10
[Soccer City Saa 3 Usiku]

LIGI za ULAYA: MESSI, FALCAO USO kwa USO JUMAPILI!!

>>LA LIGA, SERIE A & BUNDESLIGA ZAELEKEA VAKESHENI HADI 2013!!
RADAMEL_FALCAO2Tofauti na Ligi Kuu England, Ligi za Spain, Italy na Germany, yaani LA LIGA, SERIE A & BUNDESLIGA, ndio zinaelekea ukingoni kwa kucheza Mechi za mwisho hivi karibuni, na kisha kuelekea Mapumziko ya Krismas na Mwaka mpya hadi Januari Mwakani lakini Jumapili macho ya Ulaya yatakuwa Nou Camp kushuhudia Mitambo Imara ya Magoli wakati Supastaa Lionel Messi atakapokutana uso kwa uso na moto wa Radamel Falcao Garcia katika Mechi ya La Liga kati ya Vinara FC Barcelona na Timu ya Pili Atletico Madrid.
+++++++++++++++
WAFUNGAJI BORA LA LIGA:
-Lionel Messi=Bao 23
-Radamel Falcao=16
-Ronaldo=13
-Aduriz=9
+++++++++++++++
Hadi sasa Barcelona wapo Pointi 6 mbele ya Atletico Madrid ambao nao wapo Pointi 5 mbele ya Timu ya Tatu Real Madrid ambao ndio Mabingwa watetezi ambao nao Jumapili hiyo hiyo wapo nyumbani Santiago Bernabeu kucheza na Espanyol.
Licha ya kuzikutanisha Timu ambazo zipo juu kwenye La Liga, Barca na Atletico, mvuto mkubwa ni kuwaona Wafungaji mahiri Messi na Falcao wakishindana.
Falcao ataingia kwenye Mechi hii akiwa moto baada ya kufunga Bao 5 kati ya 6 ambazo Atletico Madrid waliwachapa Deportivo La Coruna Bao 6-0 katika Mechi yao ya mwisho hivi juzi.
Lakini Lionel Messi ni habari nyingine kwani kwanza ndie anaongoza kwenye La Liga kwa kufunga Bao nyingi, akiwa na Bao 23 kwa Mechi 15 za Ligi na pia ana Goli 88 kwa Mwaka huu 2012 ikidaiwa ndie anashikilia Rekodi ya Goli nyingi kwa Mwaka mmoja kitu ambacho kimepingwa na Zambia wanaodai Mchezaji wao Godfrey Chitalu ndie anaeshikilia Rekodi kwa kufunga Bao 107 Mwaka 1972 huku nao Brazil wakiibuka na kudai Supastaa wao, Zico, alifunga Bao 89 Mwaka 1979.
Ingawa mvuto nia hao Mastraika wawili lakini Vita itakayoleta ushindi ni ile ya Sehemu ya Kiungo wakati Mastaa wa Barca, Xavi, Andres Iniesta na Cesc Fabregas watakapopigana na Arda Turan, Raul Garcia na Cristan Rodriguez wa Atletico.
Huko Italy, Mabingwa watetezi na vinara, Juventus, watakuwa nyumbani kucheza na Atalanta lakini mvuto mkubwa ni Mechi kati ya Napoli, walio nafasi ya 4, na Inter Milan, walio nafasi ya 2.
Nako Germany, vinara Bayern Munich wao watafungua Wikiendi ya BUNDESLIGA hapo Ijumaa kwa Mechi ya nyumbani dhidi ya Borussia Mönchengladbach wakati Mabingwa watetezi Borussia Dortmund watacheza ugenini Jumapili na TSG Hoffenheim.
RATIBA:
LA LIGA
Jumamosi Desemba 15
18:00 Getafe CF v Osasuna
20:00 Real Mallorca v Athletic de Bilbao
22:00 Granada CF v Real Sociedad
Jumapili Desemba 16
0:00 Sevilla FC v Malaga CF
14:00 Real Zaragoza v Levante
19:00 Valencia v Rayo Vallecano
21:00 Real Madrid CF v RCD Espanyol
23:00 FC Barcelona v Atletico de Madrid
Jumatatu Desemba 17
22:00 Deportivo La Coruna v Real Valladolid
23:30 Celta de Vigo v Real Betis
Alhamisi Desemba 20
22:00 Rayo Vallecano v Levante
Ijumaa Desemba 21
0:00 RCD Espanyol v Deportivo La Coruna
0:00 Real Sociedad v Sevilla FC
2200 Valencia v Getafe
Jumamosi Desemba 22
0:00 Atletico Madrid v Celta Vigo
1800 Real Betis v Real Mallorca
2000 Real Valladolid v FC Barcelona
2200 Malaga v Real Madrid
2200 Osasuna v Granada
Jumapili Desemba 23
Athletic Bilbao v Real Zaragoza
**LIGI MAPUMZIKONI HADI JANUARI 6
Jumapili Januari 6
3:00 FC Barcelona v RCD Espanyol
3:00 Celta de Vigo v Real Valladolid
3:00 Deportivo La Coruna v Malaga CF
3:00 Real Mallorca v Atletico de Madrid
3:00 Real Madrid CF v Real Sociedad
3:00 Rayo Vallecano v Getafe CF
3:00 Sevilla FC v Osasuna
3:00 Real Zaragoza v Real Betis
3:00 Levante v Athletic de Bilbao
3:00 Granada CF v Valencia
SERIE A
Jumamosi Desemba 15
20:00 Udinese v Palermo
22:45 SS Lazio v Inter Milan
Jumapili Desemba 16
14:30 Fiorentina v Siena
17:00 AC Milan v Pescara
17:00 Chievo Verona v AS Roma
17:00 Juventus v Atalanta
17:00 Parma v Cagliari
17:00 Genoa v Torino FC
17:00 Catania v Sampdoria
22:45 Napoli v Bologna
Ijumaa Desemba 21
20:00 Pescara v Catania
22:45 Cagliari v Juventus
Jumamosi Desemba 22
14:30 Inter Milan v Genoa
17:00 Atalanta v Udinese
17:00 Bologna v Parma
17:00 Torino FC v Chievo Verona
17:00 Sampdoria v SS Lazio
17:00 Siena v Napoli
17:00 Palermo v Fiorentina
22:45 AS Roma v AC Milan
**LIGI MAPUMZIKONI HADI JANUARI 6
AC Milan v Siena
Chievo Verona v Atalanta
Juventus v Sampdoria
Lazio v Cagliari
Parma v Palermo
Udinese v Inter Milan
Napoli v AS Roma
Genoa v Bologna
Catania v Torino
Fiorentina v Pescara
BUNDESLIGA
Ijumaa Desemba 14
22:30 Bayern Munich v Borussia Mönchengladbach
Jumamosi Desemba 15
17:30 Bayer 04 Leverkusen v Hamburger SV
17:30 VfL Wolfsburg v Eintracht Frankfurt
17:30 FSV Mainz 05 v VfB Stuttgart
17:30 SpVgg Gr. Fürth v FC Augsburg
17:30 Fortuna Dusseldorf v Hannover 96
20:30 Schalke 04 v SC Freiburg
Jumapili Desemba 16
17:30 TSG Hoffenheim v BV Borussia Dortmund
19:30 SV Werder Bremen v FC Nuremberg
**LIGI MAPUMZIKONI HADI JANUARI 18
Ijumaa Januari 18
22:30 Schalke 04 v Hannover 96
Jumamosi Januari 19
17:30 Bayer 04 Leverkusen v Eintracht Frankfurt
1730 Bayern Munich v SpVgg Gr. Fürth
17:30 VfL Wolfsburg v VfB Stuttgart
17:30 FSV Mainz 05 v SC Freiburg
17:30 TSG Hoffenheim v Borussia Mönchengladbach
20:30 SV Werder Bremen v BV Borussia Dortmund

No comments:

Post a Comment