Wafungaji wa mabao ya Stars leo, Kiemba kulia na Bocco kushoto wakipongezana |
Hadi
mapumziko, Stars walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na kiungo Amri
Kiemba, dakika mya 33 akiunganisha pasi ya Mwinyi Kazimoto aliyewapunguza
wachezaji wawili wa Rwanda kabla ya kutoa pasi maridadi.
Katika mechi
hiyo iliyochezeshwa na refa Mohamed El Fadil kutoka Sudan, mshambuliaji John
Raphael Bocco ‘Adebayor’ alikuwa mwiba mchungu kwa safu ya ulinzi ya Rwanda na
aliwafanya waende kwenye vyumba vya kupumzikia wakiwa hoi.
Katika hicho
kipindi cha kwanza, Rwanda walikosa bao la wazi dakika ya 12 baada ya krosi ya
Jean Claude Iranzi kuokolewa na beki Kevin Yondan kwa kichwa na dakika ya 19
Jean Baptiste Mugiraneza alipiga juu akiwa nje kidogo ya eneo la hatari.
Stars pamoja
na kufunga bao hilo kipindi hicho cha kwanza, katika dakika ya 30 krosi nzuri
ya Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mrisho Ngassa na Bocco walishindwa kuiunganisha
na ikawapita wote.
Ngassa tena,
katika dakika ya 38 alipiga shuti kali kutoka wingi ya kushoto, lakini likaenda
nje sentimita chache.
Kipindi cha
pili,
Kipindi cha
pili Stars walirudi vizuri tena na kuendelea kucheza kwa kuonana, ingawa na Rwanda
nao waliendelea kucheza kwa bidii kutafuta bao la kusawazisha.
Hata hivyo,
walikuwa ni Stars tena waliofanikiwa kupata bao la pili 53 baada ya John Bocco kuuwahi
mpira uliotemwa na kipa Jean Claude Ndoli kufuatia shuti kali la Mwinyi
Kazimoto kutoka nje ya eneo la hatari.
Baada ya bao
hilo, Rwanda walionekana kupagawa, lakini hawakusahau kushambulia lango la
Stars na dakika ya 86 Dadi Birori hakujali ameotea akasukuma mpira nyavuni,
lakini refa akakataa bao hilo.
Kwa ushindi
huo, Stars sasa inasubiri mshindi kati ya Uganda na Ethiopia kesho kukutana naye
kwenye Nusu Fainali.
Stars; Juma
Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, Amri Kiemba,
Salum Abubakar/Athumani Iddi dk51, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngassa
na John Bocco/Shaaban Nditi dk 85.
Rwanda; Jean
Claude Ndoli, Emery Basiyenge, Ismail Nshutimayamangara/Fabrice Twagizimana
dk19, Jimmy Mbaraga/Imran Nshiyimana dk67, Charles Tibingana/Barnabe Mbuyumbyi
dk61, Michel Rusheshangoga, Jean Baptiste Mugiraneza, Haruna Niyonzima, Jean
Claude Iranzi, Dadi Birori na Tumaine Ntamuhanga. CECAFA TUSKER CUP: KILIMANJARO STARS USO KWA USO NA ZANZIBAR HEROES NUSU FAINALI.
TIMU ya taifa ya
Tanzania Bara-Kilimanjaro Stars imefanikiwa kutinga katika hatua ya robo
fainali ya michuano ya Cecafa Tusker Cup kwa kuifunga Rwanda kwa mabao
2-0 katika Uwanja wa KCC uliopo eneo la Lugogo, Kampala Uganda. Katika
mchezo huo ambao vijana wa Kilimanjaro walionyesha ufundi mkubwa na
kuwafunika kabisa Rwanda walifanikiwa kupata bao la kwanza katika dakika
ya 33 bao ambalo lilifungwa na kiungo Amri Kiemba baada ya kupokea pasi
murua kutoka kwa Mwinyi Kazimoto. Bao
hilo lilionyesha kuamsha ari ushindi wa ambapo Kilimanjaro waliongeza
kasi ya mashambulizi na kukosa mabao kadhaa kabla ya timu hizo
hazijakwenda mapumziko Rwanda au Amavubi wakiwa vichwa chini kwa kuwa
nyuma kwa bao moja. Vijana
wa Kilimanjaro ambao wananolewa na kocha Kim Poulsen walianza kupindi
cha kwa kasi kubwa na kuenyesha hawakutosheka na bao walilopata katika
kipindi cha na juhudi zao hizo zilizaa matunda dakika ya 55 baada ya
John Bocco kufunga bao la pili akimalizia mpira uliotemwa na kipa baada
ya kushindwa kumudu kunyaka shuti kali la Kazimoto. Kikosi
cha Amavubi ambacho kilikuwa kikiongozwa na nahodha wake Haruna
Niyonzima katika mchezo wa leo hakikuonyesha kuwa na madhara sana kwa
vijana wa Kilimanjaro baada ya kubanwa kila idara. Katika
robo fainali nyingine Zanzibar Heroes nayo ilifanikiwa kutinga hatua ya
nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga Burundi kwa changamoto
ya mikwaju ya penati 6-5 baada ya timu hizo kutoka sare ya bila ya
kufungana katika muda wa kawaida. Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Zanzibar Heroes watakutana na ndugu zao Kilimanjaro Stars katika nusu fainali ya michuano hiyo.
UHALIFU HUPUNGUA PINDI CHICHARITO ANAPOKUWA AKICHEZA - POLISI.
NYOTA wa kimataifa wa
Mexico na klabu ya Manchester United, Juvier Hernandez amekuwa maarufu
nchini kwake mpaka kufikia hatua ya matukio ya uhalifu kupungua pindi
anapocheza. Mbali
na uhalifu kupungua lakini wanawake wajawazito wanaokaribia kujifungua
nao hushikwa na uchungu kwa furaha pindi nyota huyo anapoifungia bao
timu yake ya United hivyo idadi ya watoto kuzaliwa kuongezeka. Ofisa
wa juu wa polisi wa mji mkuu wa nchi hiyo Mexico City, Jorge Carlos
Martinez amesema kuwa uhalifu kama wa kuteka magari, uvamizi na ukabaji
hupungua na inavyoonekana wahalifu hutumia muda huo kumuona shujaa wao
wakati anacheza. Ofisa
huyo wa polisi amesema kuwa ana matumaini meneja wa United Sir Alex
Ferguson ataendelea kumtumia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24
wakati wa kipindi hiki ambacho mji huo unakumbwa na matukio mengi ya
uhalifu. Watu zaidi ya 15,000 huuliwa kila mwaka na magenge ya wauza madawa ya kulevya.
TASWA KUFANYA MKUTANO MKUU BAGAMOYO.
Amir Mhando, Katibu Mkuu TASWA. |
MARIGA AREJEA UWANJANI.
KIUNGO wa kimataifa wa
Kenya, Mcdonald Mariga ameshindwa kuzuia kuonyesha furaha yake wakati
aliporejea tena uwanjani wakati Inter Milan ikishinda bao 1-0 dhidi ya
Palermo Jumapili Jioni. Mariga
amekuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi nane baada ya kuwa majeruhi
na kudai kuwa kilikuwa kipindi kigumu mno lakini anashukuru amepona na
amerejea tena kuitumikia klabu yake ya Inter. Kocha
wa Inter, Andrea Stramaccioni alimpanga Mariga katika kikosi chake
ikiwa ni mara ya kwanza msimu huu kwa mkenya huyo kucheza mchezo wa Ligi
Kuu nchini Italia maarufu kama Serie A. Pamoja
na kushindwa kufunga katika mchezo huo Mariga alionyesha kufurahishwa
kurejea tena uwanjani na kuahidi kufanya vizuri zaidi huko mbeleni kama
atapewa nafasi ya kucheza mara nyingi zaidi. Mariga
alitengeneza historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika
Mashariki kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati huo Jose
Mourinho ambaye ni kocha Real Madrid ya Hipsnia kwasasa alipokuwa
akiifundisha Inter Milan.
ADEBAYOR AJIENGUA KUSHIRIKI MATAIFA YA AFRIKA.
MSHAMBULIAJI wa klabu ya
Tottenham Hotspurs Emmanuel Adebayor amempa ahueni kocha wake Andre
Villas-Boas baada ya kujiondoa kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika
ambayo inatarajiwa kufanyika Januari mwakani. Adebayor
mwenye umri wa miaka 28 alitishia kujitoa katika timu ya taifa ya Togo
kama wachezaji ahwatalipwa fedha ambazo walikuwa wakidai katika
Shirikisho la Soka la nchi hiyo. Akihojiwa
nyota huyo amesema kuwa kama hakutakuwa na mabadiliko yoyote atastaafu
rasmi soka la kimataifa na wachezaji wengi wataacha kuichezea nchi yao. Kufuatia
shirikisho la nchi hiyo kushindwa kutatu suala hilo mshambuliaji huyo
ambaye amewahi kucheza katika klabu za Arsenal na Manchester City
aliamua kujiondoa kushiriki michuano ya mataifa ya Afrika
yatakayofanyika nchini Afrika Kusini ili kuonyesha msisitizo wa nia
yake.
ABRAMOVICH KUMUITA GRANT ILI KUMUONGEZEA NGUVU BANITEZ.
JOHN BOCCO WA PILI KWA UBORA DUNIANI WIKI ILIYOPITA, AMPIKU HADI INIESTA WA BARCELONA
John Bocco |
World Player of the Week |
|
Ajax Mainz | 1-4 1-2 | Borussia Dortmund Borussia Dortmund |
Mario Gotze was in scintillating form this week as Borussia Dortmund laid down a marker both in the Bundesliga and the Champions League, and took his personal tally to two goals and seven assists in his last five appearances.
The 20-year-old was simply too hot to handle for Ajax on Wednesday, setting up three goals for the rampant German champions, while notching a strike of his own.
On Saturday, the Germany starlet was pivotal again as his side maintained their hopes of clinching a third consecutive Bundelisga title, picking out Robert Lewandowski with a delightful pass for the game's decisive goal.
@GeoffKm on says: "#WPOTW should easily go to Mario Gotze, his performance against Ajax was Messi-like, plus it confirmed first place in group D!"
Goal.com Germany expert Christian Ehrhardt was equally impressed with Gotze's past week: "Right before the match against Ajax, Gotze played 'Hacky-Sack' with his chewing-gum and this shows the coolness of this young and talented player. He spit out his gum, kicked it into the air four times and caught it with his mouth again (see above video).
"When he was sidelined with his injury a lot of critics predicted some sort of decline in his career. But he responded and as you can see on the pitch and in this video, he got his laughter back, and he's playing with a lot of fun!"
Congratulations to Mario Gotze, Goal.com's 184th World Player of the Week winner! |
The Shortlist
JOHN BOCCO ATABIRIWA MAISHA SUPERSPORT
John Bocco 'Adebayor' |
JOHN Raphael Bocco amezidi kuwa gumzo kubwa katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge yanayoendelea mjini hapa.
Wapiga picha
wa Televisheni ya SuperSport wanamsifia sana Bocco na wanasema kuna uwezekano
sasa klabu ya SuperSport United ya Afrika Kusini ikamgeukia tena.
“Amefunga
katika kila mechi aliyocheza, huyu ni mfungaji wa uhakika, ni mshambuliaji
mwenye nguvu, kasi na uwezo wa kumiliki mpira, anapiga sana vichwa, ana kiwango
cha kucheza PSL (Ligi Kuu ya Afrika Kusini),”alisema mmoja wa wapiga picha hao
jana.
Jamaa wa
SuperSport wanemuhesabia Bocco hata bao ambalo alifunga kwenye mechi dhidi ya
Burundi lakini refa akakataa, ndiyo maana wanasema amefunga katika kila mechi.
Hadi sasa,
rasmi Bocco ana mabao manne, ukiondoa hilo ambalo refa ameminya. Alifunga mabao
mawili katika mechi dhidi ya Sudan na akarudia kufunga idadi hiyo dhidi ya
Somalia.
Bocco
anazidiwa bao moja tu na Mrisho Khalfan Ngassa, aliyefunga matano, lakini yote
katika mechi moja dhidi ya Somalia.
Bocco maarufu
kwa jina la utani ‘Adebayor’ anayechezea Azam FC ya Dar es Salaam, alifanya
vizuri katika majaribio yake kwenye klabu ya SuperSport United ya Afrika Kusini
Agosti mwaka huu, lakini klabu hiyo ikashindwa kufika dau la kumng’oa Chamazi.
SuperSport
ilivutiwa na soka ya Bocco, katika michuano ya Klabu Bingwa ya soka Afrika
Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Julai mwaka huu mjini Dar es Salaam hivyo
kumuita kwa majaribio, ambayo alifuzu.
Katika Kombe
la Kagame, Bocco alifunga mabao matano na kushika nafasi ya tatu katika
wafungaji bora, nyuma ya Hamisi Kiiza aliyefungana na Tadi Etikiama kwa mabao
sita, na Said Bahanuzi wa Yanga, aliyeibuka mfungaji bora kwa mabao yake saba.
Lakini Bocco
pia alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita,
kwa mabao yake 18 akiwapiku hadi washambuliaji wa kigeni waliocheza ligi hiyo
msimu huo, Emmanuel Okwi, Kenneth Asamoah, Davies Mwape na Dalington Enyiana.
Tangu
aipandishe Ligi Kuu Azam FC msimu wa 2008/2009 kwa mabao yake, akiibuka
mfungaji bora wa Ligi Daraja la Kwanza, Bocco amekuwa akiingia kwenye mbio za
kuwania kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu, msimu wa kwanza akizidiwa na Boniphace
Ambani aliyekuwa Yanga, msimu wa pili Mussa Mgosi aliyekuwa Simba na msimu wa
tatu na Mrisho Ngassa, kabla ya msimu uliopita kutimiza ndoto zake za kuwa
mfungaji bora wa ligi hiyo.
Iwapo
atanunuliwa na SuperSport, Bocco ataweka historia ya kuwa mchezaji wa pili wa
Tanzania kuchezea klabu hiyo, baada ya Suleiman Matola 2005 hadi 2007, akitokea
Simba SC.
AZAM WATUA KAMPALA KUSAKA SAINI, OKWI...
Okwi katika Challenge ya mwaka huu |
AZAM FC
wametuma mwakilishi wao hapa kufuatilia wachezaji katika mashindano ya Kombe la
Mataifa ya Afrika Masahariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge yanayoendelea
mjini hapa tangu Novemba 24, hadi Desemba 8, mwaka huu.
Mwakilishi
huyo alitua hapa jana na kuanzia leo ataanza kufanya kilichomleta mjini hapa.
Rasmi Azam
inakuwa klabu ya pili kutuma mwakilishi wake hapa baada ya El Merreikh ya
Sudan.
Mapema
mwanzoni mwa mashindano haya, ilielezwa wawakilishi wa Simba, Yanga na Coastal
Union watakuja pia hapa kutazama vipaji vya kuongeza katika klabu zao, lakini
hadi jana hakukuwa na taarifa za mwakilishi yoyote wa klabu hizo kufika hapa.
Mkurugenzi
wa Ufundi wa Coastal Union, Nassor Bin Slum ilielezwa atatua leo sawa na Seif
Ahmad ‘Seif Magari’, Abdallah Ahmad Bin Kleb wa Yanga na Geoffrey Nyange
‘Kaburu’ wa Simba.
Kiongozi wa
zamani wa Simba SC, Alhaj Juma Nkamia, ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Kondoa
Kaskazini yeye tayari yupo hapa kwa wiki nzima, lakini ameletwa na mapenzi yake
kwa timu yake ya taifa.
Kuna
wasiwasi, mmoja wa wachezaji ambao Azam imekuja kuwatazama huku ni mshambuliaji
wa Simba SC, Mganda Emmanuel Okwi ambaye inadaiwa mkataba wake umemalizika,
ingawa klabu yake imesema unaisha Mei mwakani.
APR WATAKA KUIPIKU YANGA BOOONGE LA STRIKER
Taddy Etikiama |
KLABU ya
A.P.R. ya Rwanda inataka kumsajili mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Taddy Etikiama wa A.S. Vita.
Etikiama
anayeichezea Rwanda katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA
Tusker Challenge, akitumia jina la Dadi Birori, tayari amekwishaonyesha nia ya
kujiunga na Yanga.
Habari
kutoka ndani ya kambi ya Rwanda, zimesema kwamba A.P.R. inayomilikiwa na jeshi
la nchi hiyo imevutiwa na uwezo wa mchezaji huyo na kwa kuwa amekwishamaliza
mkataba wamke Vita, inataka kumsajili.
“Huyu Dadi
APR wanataka kumsajili, akirudi tu Kigali watazungumza naye, na kwa vile
amekwishamaliza mkataba wake AS Vita, watamsajili, ni mzuri sana,”kilisema chanzo kutoka kambi ya
Rwanda, hoteli ya Sports View mjini hapa.
Mwishoni mwa
wiki, Etikiama aliwaambia Yanga SC ya Dar es Salaam, wasikosee kusajili
mshambuliaji mwingine yeyote zaidi yake, kwani yeye ndiye mkali anayewafaa
zaidi.
Akizungumza mjini uganda , Taddy ambaye hadi ameifungia Rwanda mabao mawili katika
Kombe la CECAFA Tusker Challenge alisema kwamba huu ni wakati mzuri Yanga
kumsajili, kwani amemaliza mkataba na klabu yake A.S. Vita ya DRC.
Alisema
anaijua Yanga vizuri na mfumo wake wa uchezaji pia na anaamini akijiunga nayo
atawafungia sana mabao. “Najua wana wapinzani wao wakubwa, Simba, mimi
nikisajiliwa Yanga nitakuwa nawafunga sana hao Simba,”alisema Etikiama na
kuongeza.
“Mimi ni
mkali kweli, nimekuwa mfungaji bora wa Kongo (DRC), nimefunga mabao 15 ligi
yenye timu nzuri kama TP Mazembe, St Eloi Lupopo na DC Motema Pembe,
nimewashinda akina Mbwana Samatta, Yanga wakinipata watapata mchezaji mzuri wa
ushindi,”alisema.
Taddy
alikuwa na A.S. Vita kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati,
Kombe la Kagame, ambayo Yanga iliibuka bingwa.
Katika
mashindano hayo yaliyofanyika mjini Dar es Salaam Taddy alikaribia kuwa
mfungaji bora baada ya kushika nafasi ya pili kwa mabao yake sita, nyuma ya
Said Bahanuzi wa Yanga aliyefunga saba na kutwaa kaitu cha dhahabu cha michuano
hiyo.
Taddy
alifunga idadi sawa ya mabao na mshambuliaji mwingine wa Yanga, Hamisi Kiiza
‘Diego‘, ambaye katika Challenge hii naye anachezea nchi yake, Uganda.
EL MERREIKH YAVAMIA ANGA ZA SIMBA, CHELEWA CHELEWA UTAKUTA MWALI SI WAKO
Umony akiwa na ramadhan Sarpei, |
MSHAMBULIAJI
wa Uganda, Brian Umony amekwishasema yuko tayari kujiunga na klabu ya Simba ya
Dar es Salaam, lakini kabla Wekundu hao wa Msimbazi hawajachukua hatua yoyote,
El Merreikh ya Sudan imetuma mwakilishi wake hapa azungumze na mchezaji huyo.
Habari zimesema kwamba, Merreikh
inayosuka upya kikosi chake baada ya kukosa ubingwa wa Sudan, imetuma
mwakilishi wake hapa afanye mazungumzo na Umony, aliyekoswakoswa kidogo tu na
Simba mwaka 2009, alipokuwa KCC ya hapa.
Mwandishi
mmoja wa habari wa Sudan, alisema jana katika hoteli ya Silver Springs
mjini hapa kwamba, tayari mwakilishi huyo wa Merreikh yuko hapa kwa kazi hiyo.
Aidha,
Mwandishi huyo amesema mwakilishi huyo wa Merreikh atatazama vipaji zaidi
kuanzia hatua ya Robo Fainali kwa ajili ya kupendekeza wachezaji wapya wa
kusajiliwa na klabu hiyo.
Mwandishi
huyo alisema tayari Merreikh pia imekubaliana biashara na Yanga juu ya kiungo
Haruna Niyonzima, Nahodha wa Rwanda katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki
na Kati, CECAFA Tusker Challenge.
Mwishoni mwa
wiki, akizungumza mjini uganda baada ya
kuiongoza Uganda kuifunga Sudan Kusini maao 4-0 katika mechi ya mwisho ya Kundi
A, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na kati, CECAFA Tusker Challenge, Umony
alisema Simba kama wanamtaka wamfuate haraka wamalizane.
Brian
amerejea nyumbani Uganda na kujiunga na Express baada ya kumaliza mkataba wake,
Becamex Binh Duong F.C. ya Vietnam.
Mwaka 2009,
baada ya Simba kuzidiwa kete na SuperSport United ya Afrika Kusini, ikamsajili
Emmanuel Okwi aliyekuwa SC Villa wakati huo.
Umony
aliichezea Supersport United hadi 2010 alipohamia University of Pretoria ya
Afrika Kusini pia hadi mwaka 2011 alipohamia Portland Timbers ya Marekani kwa
mkopo na mwaka huu akatua Becamex Binh Duong F.C. Brian anang’ara katika Kombe
la Challenge, hadi sasa ana mabao matatu.
KILA LA HERI STARS NA HEROES ROBO FAINALI TUSKER CHALLENGE LEO, MAANA NI SHUGHULI PEVU
Kikosi cha Tanzania Bara |
DUA njema za
Watanzania kwa ujumla, leo zitaelekezwa mjini hapa, wakati timu mbili kutoka
Jamhuri ya Muungano wetu, Bara na Zanzibar zitakapokuwa zikipigana katika Robo
Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker
Challenge kwenye Uwanja wa Lugogo.
Bara,
maarufu Kilimanjaro Stars watakuwa wa kwanza kutupa kete yao leo kuanzia saa
8:00 mchana kwa kumenyana na Rwanda, kwa jina la utani Amavubi, yaani Nyigu,
wakati Zanzibar Heroes watasubiri hadi saa 10:00 kukipiga na Burundi, Int’hamba
Murugamba, yaani Mbayuwayu.
Robo Fainali
nyingine zinatarajiwa kuchezwa kesho kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kenya
ikianza na Malawi saa 10:00 jioni kabla wenyeji Uganda kumenyana na Ethiopia
saa 1:00 usiku.
Zanzibar wakiomba dua kabla ya mechi na Rwanda waliyoshinda 2-1 |
Mchezo kati
ya Burundi na Zanzibar unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua, na zaidi
Mashujaa wa Visiwani wanatakiwa kumchunga sana Nahodha wa Mbayuwayu, Suleiman
Ndikumana kwa sababu ndiye amekuwa akiiongoza vema timu yake.
Ndikumana
amekuwa akihaha Uwanja wa mzima, akicheza kwa kuwahamasisha wadogo zake na hadi
sasa ndiye Nahodha bora zaidi katika mashindano haya.
Hazina ya
Zanzibar ni safu nzuri ya kiungo inayoongozwa na Suleiman Kassim Selembe na
Khamis Mcha ‘Vialli ’bila kusahau ukuta imara chini ya mabeki Nadir Haroub
‘Cannavaro’ na Aggrey Morris na hata kipa hodari, Mwadini Ally.
Safu ya
ushambuliaji leo hakuna shaka itaongozwa na Jaku Juma, mkali wa mabao katika
Ligi Kuu ya Zanzibar na Seif Abdallah, nyota wa Ruvu Shooting ya Bara aliye
mbioni kuhamia Azam FC.
Mambo zaidi
ni Rwanda na Bara; jezi namba nane (8) leo zinatarajiwa kuwa kila kitu. Jezi
hiyo kwa upande wa Rwanda anavaa Haruna Hakizimana Niyonzima na Bara Mrisho
Khalfan Ngassa.
Wawili hawa
ndio wamekuwa kama roho ya timu zao katika mashindano haya na leo wanatarajiwa
kuendelea kubeba jukumu hilo.
Ngassa
anacheza wingi ya kushoto kwa sasa kwenye kikosi cha Bara, wakati Niyonzima
anapangwa wingi ya kulia katika kikosi cha Rwanda. Niyonzima huwa anabadilika
na kuingia ndani na wakati mwingine upande wa pili na kwa ujumla huhaha Uwanja
mzima, vivyo hivyo kwa Ngassa.
Dadi Birori au
Taddy Etikiama kwa jina lingine atasimama mbele bila kuongoza mashambulizi kwa
Rwanda na langoni atakuwapo kipa mgumu kufungika, Jean Claude Ndoli.
Kocha wa
Bara, Mdenmark Kim Poulsen anacheza na mshambuliaji mmoja, John Bocco, lakini
anatumia mawinga wenye kushambulia mno- Ngassa na Simon Msuva, wakati Micho pia
hutumia washambuliaji wawili na hana viungo wenye kasi sana, ila mafundi.
Mabeki wa
pembeni wa Rwanda wanapitika kwa urahisi na leo Ngassa na Msuva washindwe
wenyewe tu. Beki ya kati ya Rwanda ni ugonjwa wa moyo, maana yake John Bocco
leo ni umakini wake tu.
Kwa ujumla,
Bara ina nafasi kubwa ya kuitoa Rwanda, tena kwa kuipa kipigo kitakatifu tu
kama watatumia vyema nafasi zao.
Mwinyi
Kazimoto amepona na bila shaka atakuwa mmoja wa viungo watatu leo, wengine
Frank Domayo na Amri Kiemba maana yake, kwenye benchi watakuwapo Athumani Iddi
‘Chuji’ na Shaaban Nditi.
Piga, ua
Juma Kaseja atasimama langoni, kulia Erasto Nyoni na kushoto uzoefu utambeba
Amir Maftah ingawa Issa Rashid anakuja vizuri, wakati katikati Kevin Yondan
atacheza pacha na Shomary Kapombe.
Hii ni mara
ya pili ndani ya miaka mitatu Bara kukutana na Rwanda katika hatua hii na mara
ya mwisho ilikuwa Desemba 8, mwaka 2010 wakati bao pekee la mkwaju wa penalti
la aliyekuwa Nahodha wa Stars, Nsajigwa Joel Shadrack Mwandemele dakika ya 61
lilipoipa Bara ushindi wa 1-0 na kutinga Nusu Fainali hadi kutwaa ubingwa Dar
es Salaam.
Lakini mwaka
jana pia timu hizo zilikutana Dar es Salaam katika michuano hii, Kundi A na
Rwanda iliilaza Bara 1-0 Novemba 26, katika michuano ambayo wenyeji waliboronga
vibaya na kutolewa mapema.
Tangu mwaka
2001, timu hizi zimekutana mara tisa katika Challenge na Rwanda imeshinda mechi
sita, wakati Bara imeshinda mechi tatu tu. Idadi kubwa ya mabao Tanzania
kuifunga Rwanda ni 3-0, wakati Amavubi wamewahi kuichapa Bara 5-1.
Pamoja na
yote, Robo Fainali za leo ni nzuri- zaidi Watanzania kwa ujumla Bara na
Visiwani, wanatakiwa kuziombea dua njema timu zao zivuke hatua hii, kwani
katika soka lolote hutokea. Mungu
ibariki Bara na Zanzibar, ibariki Tanzania. Amin.
REKODI YA
TANZANIA NA RWANDA CHALLENGE:
Desemba 17, 2001; Nusu Fainali Rwanda
Tanzania 1-2
Rwanda B
Desemba 11, 2002; Nusu Fainali Mwanza
Tanzania 3-0
Rwanda
Desemba 19, 2004; Kundi A Ethiopia
Tanzania 1-5
Rwanda
Desemba 6, 2005; Kundi A Rwanda
Tanzania 1-3
Rwanda
Desemba 5, 2006; Robo Fainali Ethiopia
Tanzania 1-2
Rwanda
Januari 7, 2009; Kundi A Uganda
Tanzania 2-0
Rwanda
Desemba 10, 2009: Nusu Fainali Kenya
Tanzania 1-2
Rwanda
Desemba 8, 2010; Robo Fainali Dar es Salaam
Tanzania 1– 0 Rwanda
Novemba 26, 2011; Kundi A, Dar es Salaam
Tanzania 0 – 1 Rwanda
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE
2012
Mrisho
Ngassa Tanzania 5
John Bocco Tanzania 4
Suleiman
Ndikumana Burundi 3 (1 penalti)
Brian Umony Uganda 3
Chris
Nduwarugira Burundi 3
Khamis Mcha Zanzibar 2
David
Ochieng Kenya 2
Clifton
Miheso Kenya 2
Dadi Birori Rwanda 2BUSQUETS AWASIHI WENZAKE KUTOBWETEKA.
KIUNGO nyota wa klabu ya
Barcelona, Sergio Busquets amesisitiza kuwa hawatakiwi kujibweteka kama
wanataka kushinda taji la Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga
msimu huu. Barcelona
wametofautia alama sita na Atletico Madrid ambao wanashika nafasi ya
pili kufuatia ushindi wa mabao 5-1 waliopata kutoka kwa Athletic Bilbao
wakati bado wameacha pengo la alama 11 dhidi ya mahasimu wao Real Madrid
ambao wanashika nafasi ya tatu. Busquests
aliiambia wavuti ya klabu hiyo kuwa pamoja na kuongoza La Liga kwa
tofauti ya alama nyingi lakini safari bado ni ndefu kufikia mwishoni mwa
msimu hivyo bado hakuna muda wa kupumzika kwa sasa. Kiungo
huyo alimsifu mchezaji mwenzake nyota Lionel Messi na kudai kuwa ndio
mchezaji bora wa dunia kwasasa kwasababu anaweza kufunga mabao na kuwa
sehemu ya mashambulizi yote ambayo klabu imekuwa ikifanya. Messi
alifunga mabai mawili katika mchezo dhidi ya Bilbao uliochezwa Jumamosi
na kufikisha mabao 21 katika mechi 14 alizocheza msimu huu.
FERGUSON AMTAKA MOURINHO KUVAA VIATU VYAKE OLD TRAFORD.
FIFA KOMBE la MABARA: Wenyeji Brazil kufungua na Japan, Kundi moja na Italy!
>>SPAIN pamoja na Uruguay!!
+++++++++++++++++++++++++++++
MAKUNDI:
KUNDI A:
-Brazil
-Japan
-Mexico
1Italy
KUNDI B:
-Spain
-Uruguay
-Tahiti
-Bingwa wa Afrika (Kujulikana Februar10, 2013)
+++++++++++++++++++++++++++++
Wenyeji Brazil watacheza Mechi ya
ufunguzi ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara kwa kucheza na Japan
Mjini Brasilia hapo Juni 15, 2013 baada ya Droo ya Mashindano hayo
kufanyika huko Sao Paulo ambayo ilipanga Makundi mawili.
Mara baada ya Mechi hiyo, Brazil watacheza na Mexico na kumaliza na Italy katika Mechi za Kundi A.
Kundi B lina Mabingwa wa Dunia Spain, Uruguay, Tahiti na Bingwa wa Afrika (Kujulikana Februar10, 2013).
FIFA ilishatangaza Miji ambayo itatumika
kwa ajili ya Mashindano hayo ambayo ni Brasilia, Belo Horizonte,
Fortaleza, Rio de Janeiro, Recife na Salvador.
RATIBA:
Juni 15
Brazil v Japan
Juni16
Mexico v Italy
Spain v Uruguay
Juni 17
Tahiti v Bingwa Afrika
Juni 19
Brazil v Mexico
Italy v Japan
Juni 20
Spain v Tahiti
Bingwa Afrika v Uruguay
Juni 22
Japan v Mexico
Italy v Brazil
Juni 23
Bingwa Afrika v Spain
Uruguay v Tahiti
NUSU FAINALI
Juni 26
Mshindi A v Mshindi wa Pili B
Juni 27
Mshindi B v Mshindi wa Pili A
FAINALI
Juni 30
FA CUP RAUNDI ya 3: Droo yafanyika, Man United kuivaa Hammers Upton Park!!
>>MECHI 4 tu kukutanisha Timu za Ligi Kuu!!
Manchester
United watatua Upton Park kucheza na West Ham United katika Raundi ya 3
ya FA CUP kwa mujibu wa Droo iliyofanyika leo hiyo ikiwa moja ya Mechi 4
tu zitakazokutanisha Timu za Ligi Kuu England.
Mechi nyingine za Timu za Ligi Kuu
England ni zile za Southampton watakaokuwa nyumbani kucheza na Mabingwa
watetezi Chelsea, QPR kuikaribisha West Brom na Arsenal kusafiri kucheza
na Swansea.
Timu nyingine vigogo wa LigI Kuu, kama
vile Mabingwa wa Ligi Manchester City, wao watacheza na Watford,
Tottenham kucheza na Coventry.
Mechi zitachezwa Jumamosi Januari 5, 2013 na Jumapili Januari 6, 2013.
RATIBA:
RAUNDI ya TATU:
Crystal Palace v Stoke
Brighton v Newcastle
Tottenham v Coventry City
Wigan v Bournemouth
Fulham v Blackpool
Aston Villa v Ipswich
Charlton v Huddersfield
Barrow or Macclesfield v Cardiff
Barnsley v Burnley
Manchester City v Watford
Swansea v Arsenal
Leicester v Burton
Millwall v Preston
Cheltenham or Hereford v Everton
Derby v Tranmere
Crawley v Reading
Aldershot v Rotherham or Notts County
Middlesbrough v Harrogate or Hastings
Accrington Stanley or Oxford v Sheffield United
Southampton v Chelsea
QPR v West Brom
Peterborough v Norwich
Lincoln or Mansfield v Liverpool
Bolton v Sunderland
Nottingham Forest v Oldham
West Ham v Manchester United
Hull v Alfreton or Leyton Orient
Blackburn v Bristol City
Leeds v Birmingham
Bury or Southend v Bradford or Brentford
Luton v Wolves
Sheffield Wednesday v MK Dons
Ferguson adokeza Difensi yake dhidi ya Cluj!
Sir Alex Ferguson amesema anategemea
Nahodha wake Nemanja Vidic atacheza Mechi yao ya Jumatano ya kukamilisha
Ratiba tu ya UEFA CHAMPIONZ LIGI dhidi ya CFR Cluj baada ya kupona goti
lake.
Pia alidokeza Mechi hiyo ni muafaka kwa Difensi yake kuwa na Phil Jones, Chris Smalling na Alexander Büttner.
Manchester United tayari wameshafuzu
toka Kundi H wakiwa vinara wa Kundi hilo lakini nafasi ya pili bado
inagombewa na Galatasaray na Cluj hivyo ni muhimu kwao kuchezesha Kikosi
imara ili kutoa haki kwa ushindani wa Timu mbili zinazogombea nafasi ya
pili.
Katika Mechi iliyopita ya Kundi H wakati
tayari wakiwa wamefuzu, Man United walibadili Kikosi na kufungwa 1-0
huko Uturuki na Galatasaray.
Anderson NJE WIKI KADHAA!!
Sir Alex Ferguson amethibitisha
Anderson atakuwa nje ya Uwanja kwa Wiki kadhaa baada ya kuumia kwenye
Mechi ya Ligi Kuu England walipoifunga Reading Bao 4-3 juzi Jumamosi.
Anderson, ambae amecheza Mechi 8 za
mwisho za Man United, Jumamosi wakicheza na Reading alifunga Bao la
kwanza zuri lakini ikabidi atolewe kabla haftaimu baada ya kuumia musuli
za pajani.
Adebayor asusa kuichezea Togo, kuikosa AFCON 2013!
Emmanuel Adebayor, ambae ni Nahodha wa
Timu ya Taifa ya Togo, ametangaza kusimama kuichezea Nchi hiyo kutokana
na mgogoro wa Wachezaji kutolipwa stahili yao baada ya kucheza Mechi ya
Kirafiki na Morocco na uamuzi huo huenda ukamfanya asicheze Fainali za
Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, zitakazochezwa huko Afrika
Kusini kuanzia Januari 19 na kumalizika Februari 10, Mwaka 2013.
Uamuzi huo, bila shaka, utaufurahisha Klabu yake Tottenham ambayo itakuwa na uhakika wa kuweza kumtumia katika kipindi hicho.
Akitangaza uamuzi wake, Adebayor alisema
Shirikisho la Soka la Togo lilipokea EURO 35,000 toka kwa wenzao wa
Morocco lakini wao hawakuwalipa Wachezaji ila baadhi tu walipewa nusu
wakati pesa zilipokelewa na Rais wa Shirikisho hilo.
Adebayor alistaafu kuichezea Togo Mwaka
2010 mara baada ya Basi la Timu ya Togo kushambuliwa kwa risasi Nchini
Angola na kutokea vifo lakini Mwaka huu alirudia tena kuichezea na
kufanikisha kutinga kwao Fainali za AFCON 2013.
No comments:
Post a Comment