Sunday, November 11, 2012

 

TOTO ACHEZEA SHARUBU ZA MNYAMA UWANJA WA TAIFA WAKATI ICE CREAM ZA AZAM ZIKIMWAGWA NA MGAMBO WA CITY MKWAKWANI.

Beki wa Toto African Elly Hamad akimdhibiti Haruna Chanongo wa Simba kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa leo uwanja wa taifa
Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi akiwa amedhibitiwa na kiungo  wa Toto African  Peter Mutabuzi kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa leo uwanja wa Taifa

Kiungo wa Simba Amri Kiemba akimtoka beki wa Toto African kwenye mchezo uliochezwa taifa
Wachezaji wa Toto wakimpongeza mfungaji wa bao lao baada ya mchezo waliocheza leo kwenye uwanja wa taifa na Simba baada ya mchezo kumalizika.
TIMU ya Simba leo imemaliza mzunguko wa kwanza kwa kufungwa na Toto African bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Bao pekee la Toto lilifungwa na Mussa Said Kimbu dakika ya 73.

Kimbu alifunga bao hilo baada ya kupiga direct free kick baada ya kutokea faulo na mpira huo kuwapita walinzi wa Simba na kipa wao Wilbert Mweta na kutinga wavuni.

Michezo mingine ya ligi iliyochezwa leo ni pamoja na Azam dhidi ya Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga ambapo wanalambalamba hao Azam wamefungwa 2-1.

Kwa matokeo haya, Yanga inazidi kukaa kileleni kwa pointi zake 26 na kesho itamaliza mechi yake ya mzunguko wa kwanza kwa kucheza Coastal Union mchezo uliopigwa Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.

Simba inaendelea kubaki nafasi ya tatu kwa pointi zake 23 na Azam yenye pointi 24 ni ya pili.

Simba SC: Wilbet Mweta, Nassor Masoud ‘Chollo’, Paul Ngalema, Komanbil Keita, Shomari Kapombe, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngassa, Felix Sunzu na Emanuel Okwi. 

Toto African; Erick Ngwengwe, Ally Ahmad, Eric Murilo, Evarist Maganga, Peter Mutabuzi, Hamisi Msafiri, Emanuel Swita, Kheri Mohamed, Mohamed Jingo, Suleiman Kibuta na Mussa Sai.

MABONDIA WA TANZANIA WADUNDWA NA WENZAO WA ZAMBIA

Bondia Kassim Hussein (aliyevaa nyekundu)  wa Tanzania a kikwepa konde la Bondia Charles Lumbwe wa Zambia (aliyevaa bluu) alloimrushia  kwenye mchezo wa kirafiki kg 64 ulichezwa kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo

Bondia Kassim Hussein (aliyevaa nyekundu)  wa Tanzania akijapanga jinsi ya kupiga ngumi zenye uzito mpinzani wake Bondia Charles Lumbwe wa Zambia (aliyevaa bluu)   kwenye mchezo wa kirafiki kg 64 ulichezwa kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo


Bondia Mohamed Chimbumbui wa Tanzania (aliyevaa nyekundu) akizuia ngumi nzito za Mbachi Kaonga wa Zambia kg 75


MABONDIA wa ngumi za Ridhaa wa Tanzania leo wamechezea kichapo baada ya kupingwa michezo minne kati ya mitano iliyochezwa leo na mabondia toka Zambia kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo

Mapambano haya ambayo yalikuwa ni ya kirafiki yenye raundi tatu ilishuhudia Said Hofu akifungua pazia (kg 49) kwa kupigwa kwa pointi na Caristo Bwalia toka Zambia

Mpambano wa pili kg 56 ulishuhudia Frank Nicolaus wa Tanzania akipigwa na Russel Mwamba wa Zambia kwa pointi pia.

Kg 60 ndipo mtanzania Ismail Galiatano alimshushia ngumi nzito nzito John Chimpwele wa Zambia na kusababisha kuchanika juu ya jicho na kutokwa damu nyingi ndipo mwamuzi alisimamisha mchezo na kumpa ushindi Ismail Galiatano.(RSC)

Mpambano wa nne kg 64 Mtanzania Kassim Hussein alipokea kipigo toka kwa  Charles Lumbwe kwa kupigwa kwa pointi.

Funga kazi kg 75 ikawa ndio usiseme maana Mohamed Chimbumbui alipigwa kwa TKO na Mbachi Kaonga wa Zambia baada ya kumsukumizia makonde mazito mazito na kushindwa kuyamili na kujikuta akianguka kila mara.

Katibu wa Chama ngumi za ridhaa, Makore Mashaga alisema wamepoteza mpambano huo lakini anashukuru wamepata mazoezi ya kujiandaa na mashindano ya ndano yanayotarajiwa kuanza Novemba 26 kwenye uwanja wa ndani wa taifa, jijini Dar es salaam.

Mabondia watanzania walisema kupigwa kwao kunatokana na maandalizi hafifu waliyopata na mashindano kuahirishwa mara kwa mara pia kuliwafanya morali kushuka.

Naye Katibu wa Ngumi za Ridhaa wa Zambia Lut. Kanali Man Muchimba amesema amefurahimu kucheza na watanzania kwani wamepata mazoezi ya kuwasaidia kucheza mashindano ya kanda ya tano yatakayofanyika nchini kwao mapema Desemba.

 

NI VIGUMU KUCHEZA KWA KIWANGO KILA BAADA YA SIKU TATU - RIBERY.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Bayern Munich, Franck Ribery amekiri kuwa klabu yake inapata wakati mgumu kucheza kwa kiwango kutokana na kucheza mechi kila baada ya siku tatu pamoja na kuongoza Ligi Kuu nchini Ujerumani maarufu kama Budesliga kwa alama saba zaidi.
 
 Ribery aliifungia bao la kuongoza Bayern katika dakika ya 44 dhidi ya Eintracht Frankfurt kabla ya kiungo wa kimataifa wa Austria David Alaba kufunga bao la pili na kupelekea timu hiyo kuondoka kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika Uwanja wa Allianz Arena jijini Munich. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Ribery amekiri kuwa kucheza kila baada ya siku tatu sio kazi rahisi tofauti na wapinzani wao Frankfurt ambao wenyewe walikuwa wamepumzika kutokana na kutokuwa na mechi zingine zaidi ya ligi.
 
 Ribery mwenye umri wa miaka 29 ambaye alijiunga na Bayern mwaka 2009 aliendelea kusema kuwa ratiba ya mechi za Bundesliga, Kombe la Ligi na Ligi ya Mabingwa Ulaya ndio inachangia wawe wanacheza mechi kila baada ya siku tatu kitu wakati mwingine inakuw vigumu kucheza kwa kiwango walichokizoea.
 
 Pamoja na kauli yake hiyo kocha wa kikosi cha Ufaransa, Didier Deschamps amemjumuisha mchezaji huyo katika kikosi chake kitakachocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Italia mchezo ambao utafanyika jijini Parma Jumatano ijayo.

KLITSCHKO ATETEA MATAJI YAKE.

BONDIA nyota wa uzito wa juu duniani, Wladimir Klitschko amefanikiwa kutetea mataji yake ya IBF, IBO, WBO na WBA baada ya kumpiga Mariusz Wach kutoka Poland kwa pointi katika pambano lilifanyika jijini Humburg nchini Ujerumani.  
 
Katika pambano hilo Klitschko alionekana kushindwa kuonyesha kuonyesha cheche zake katika raundi tano za kwanza lakini baadae alionyesha kurudi mchezoni na kuanza kumshambulia makonde mfululizo mpinzani wake ambaye alionyesha kuchoka baada ya raundi ya tano.
 
 Waamuzi wa mchezo huo walitoa alama 120-107, 120-107 na 119-109 huku alama nyingi kati ya hizo zikimwendea Klitschko ambaye alifanikiwa kutetea mataji yake katika mapambano 13 aliyocheza. 
 
 Hii ni mara ya kwanza kwa Klitschko kupambana bila kocha wake nguli wa mchezo huo Emanuel Steward ambaye alifariki mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 68 kwa ugonjwa wa kansa.

BOATENG KUIKOSA UHOLANZI.

BEKI wa kimataifa wa Ujerumani, Jerome Boateng anatarajiwa kuukosa mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya nchi yake na Uholanzi mchezo ambao utachezwa Jumatano baada ya kupata majeraha kwenye kinena. 
 
 Beki huyo alipata majeraha hayo wakati wa mchezo wa Bundesliga baina ya timu yake ya Bayern Munich na Eintracht Frunkfurt ambapo Bayern walishinda kwa mabao 2-0.
 
 Boateng mwenye umri wa miaka 24 alitolewa nje katika dakika ya 32 ya mchezo huo uliofanyika jijini Munich ambapo sasa anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili. Pamoja na maumivu hayo Boateng amefurahishwa na matokeo ambayo Bayern iliyapata katika mchezo huo ingawa kwa upande mwingine amesikitika kushindwa kuliwakilisha taifa lake katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Uholanzi. 
 
 Boateng anakuwa ni mchezaji wa pili kukosekana katika ukuta wa Ujerumani kwenye mchezo huo baada ya beki mwingine wa kati wa timu hiyo Holger Badstuber naye kuwa nje ya kikosi hicho kutokana na majeruhi.

WALCOTT HATIHATI KUIKOSA SWEDEN - WENGER

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amebainisha kuwa mshambuliaji nyota wa klabu hiyo yuko katika hatihati ya kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya timu ya taiafa ya Uingereza na Sweden wiki ijayo kufuatia kuumia msuli katika mchezo wa Ligi Kuu ambao Arsenal ilitoka sare ya mabao 3-3 na Fulham. 
 
 Mchezo huo uliochezwa jana ndio ulikuwa wa kwanza kwa Walcott kuanza toka ligi hiyo ilipofunguliwa ambapo mpira wa kona aliopiga mwanzoni mwa kipindi cha kwanza cha mchezo huo ulipelekea Olivier Giroud kuifungia Arsenal bao la kuongoza kwa kichwa.  
 
Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Wenger amesema kuwa Walcott alikuwa na tatizo la misuli na alikaribia kumpumzisha wakati wa mapumziko wakati alipkaribia kuanguka lakini waliamua kumuacha baada ya kuona kama anaendelea vyema.  
 
Wenger aliendelea kusema kuwa katika dakika za mwishoni hali yake ilizidi kuwa mbaya hivyo kuamua kumpumzisha na hadhani kama ataweza kujumuika na wenzake katika kikosi cha Uingereza.

BPL: LEO ndio LEO kwa Chelsea, Liverpool, City na Spurs!!

Oscar Dos Santos completes his transfer move to Chelsea from Internationale
>>CHELSEA, CITY KUWASOGELEA VINARA MAN UNITED??
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumapili, Novemba 11
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Manchester City v Tottenham Hotspur
[SAA 12 Jioni]
Newcastle United v West Ham United
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Liverpool
+++++++++++++++++++++++
BPL_LOGOLeo, kwenye mfululizo wa Mechi za Ligi Kuu England, BPL, zipo Mechi 3 lakini mbili ndio zipo kwenye midomo ya Wadau wengi wa Soka, zile za Manchester City v Tottenham Hotspur na Chelsea v Liverpool, hasa kwa vile zinahusisha Timu vigogo na pia kutaka kujua kama Chelsea na City wanaweza kuikaribia Manchester United ambao ndio vinara na jana walipiga hatua zaidi mbele baada ya kuibonda Aston Villa 3-2 na kuwafanya waongoze Ligi wakiwa Pointi 4 mbele ya Chelsea walio nafasi ya pili na Pointi 5 mbele ya City walio nafasi ya 3.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
1 Man United Mechi 11 Pointi 27
2 Chelsea Mechi 10 Pointi 23
3 Man City  Mechi 10 Pointi 22
+++++++++++++++++++++++
Manchester City v Tottenham
Manchester City wataingia kwenye Mechi hii wakitegemea kuwa nao tena Joleon Lescott, Maicon na David Silvaambao walikuwa majeruhi lakini Wachezaji Micah Richards, James Milner na Jack Rodwell kwa vile bado ni majeruhi.
Tottenham itakuwa bila majeruhi Mousa Dembele, Scott Parker, Benoit Assou-Ekotto na Younes Kaboul.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Manchester City: Hart, Pantilimon, Wright, Zabaleta, Maicon, Kompany, Lescott, Nastasic, K Toure, Clichy, Kolarov, Nasri, Y Toure, Barry, Garcia, Sinclair, Silva, Aguero, Dzeko, Balotelli, Tevez.
Tottenham: Friedel, Lloris, Cudicini, Gomes, Naughton, Walker, Caulker, Gallas, Dawson, Vertonghen, Livermore, Parrett, Huddlestone, Mason, Carroll, Sandro, Sigurdsson, Lennon, Townsend, Bale, Falque, Dempsey, Obika, Defoe, Adebayor.
Newcastle v West Ham
Newcastle watacheza bila ya Cheick Tiote na Fabricio Coloccini ambao wapo kifungoni.
Meneja wa West Ham Sam Allardyce yupo kwenye hali tete kwani hana uhakika wa Mabeki wake James Collins na James Tomkins kuwepo kwa vile wana maumivu.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Newcastle: Krul, Harper, Elliot, Santon, Ferguson, Tavernier, S. Taylor, Williamson, Bigirimana, Cabaye, Gutierrez, Ben Arfa, Anita, Obertan, Sammy Ameobi, Marveaux, Amalfitano, Abeid, Ba, Cisse, Shola Ameobi, Xisco.
West Ham: Jaaskelainen, Spiegel, O'Brien, Reid, Collins, Tomkins, McCartney, Demel, Noble, Diame, Nolan, Jarvis, Benayoun, Diarra, O'Neil, Maiga, Cole, Carroll, Spence.
Chelsea v Liverpool
Ashley Cole hatakuwepo kwenye Kikosi cha Chelsea kwa vile ni majeruhi lakini John Terry anaweza kuanza baada ya kumaliza Kifungo chake cha Mechi 4 kwa Ubaguzi.
Beki wa England Glen Johnson anatarajiwa kurudi dimbani baada ya kupona maumivu ya musuli za pajani na pia Kipa Jose Reina huenda akawemo baada ya pia kupona.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Chelsea: Cech, Ivanovic, Azpilicueta, Terry, Luiz, Cahill, Bertrand, Mikel, Romeu, Ramires, Mata, Oscar, Hazard, Moses, Marin, Torres, Sturridge, Turnbull
Liverpool: Jones, Gulacsi, Reina, Wisdom, Agger, Skrtel, Coates, Carragher, Enrique, Johnson, Downing, Allen, Sahin, Gerrard, Shelvey, Henderson, Assaidi, Yesil, Suso, Suarez, Sterling
 

BPL: Chicharito na HETITRIKI!!


>>MAN UNITED yatoka nyuma 2-0, washinda 3-2 VILLA PARK!!
CHICHARITO_SHANGILIAMSIMAMO:
1 Man United Mechi 11 Pointi 27
2 Chelsea Mechi 10 Pointi 23
3 Man City  Mechi 10 Pointi 22
+++++++++++++++++++++++
Javier Hernandez, Chicharito, leo amepiga hetitriki na kuibakisha Manchester United kileleni mwa Ligi Kuu England walipotoka nyuma kwa bao 2-0 na kuichapa Aston Villa 3-2 Uwanjani Villa Park.
+++++++++++++++++++++++
MATOKEO:
Jumamosi, Novemba 10
Arsenal 3 Fulham 3
Everton 2 Sunderland 1
Reading 0 Norwich City 0
Southampton 1 Swansea City 1
Stoke City 1 Queens Park Rangers 0
Wigan Athletic 1 West Bromwich Albion 2
Aston Villa 2 Manchester United 3
+++++++++++++++++++++++
Awali, Mechi tamu na ya vuta nikuvute ni ile ya Uwanjani Emirates ambapo Arsenal, waliumwaga uongozi wa bao 2-0 na kuiruhusu Fulham kurudisha na kuongoza bao 3-2 na wao kusawazisha lakini tena wakaukosa ushindi baada ya Mikel Arteta kukosa kufunga Penati ‘tata’ ya Dakika za mwisho.
VIKOSI:
Aston Villa: Guzan, Lowton, Vlaar, Clark, Stevens, Weimann, Westwood, Ireland, Bannan, Agbonlahor, Benteke
Akiba: Given, El Ahmadi, Albrighton, Holman, Delph, Bowery, Williams.
Man Utd: De Gea, Da Silva, Ferdinand, Smalling, Evra, Valencia, Carrick, Scholes, Young, Rooney, van Persie
Akiba: Lindegaard, Anderson, Hernandez, Welbeck, Cleverley, Fletcher, Buttner.
Refa: Kevin Friend
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumapili, Novemba 11
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Manchester City v Tottenham Hotspur
[SAA 12 Jioni]
Newcastle United v West Ham United
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Liverpool

No comments:

Post a Comment