Wednesday, November 14, 2012

KAMATI YA SERENGETI YAKUSANYA MZIGO WA KUTOSHA KUISHINDISHA TIMU

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Saidia Serengeti Boys Ishinde, Kassim Mohamed Dewji akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Serengeti, ndani ya hoteli ya JB Bellmonte, katikati ya Jiji la Dar es Salaam asubuhi ya leo kuhusu maandalizi ya mechi ya Jumapili dhidi ya Kongo Brazzaville, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za U-17 Afrika. Dewji amesema Kamati yake imefanikiwa kukusanya Sh. Milioni 35 kati ya Milioni 60 zinazotakiwa kwa maandalizi ya mchezo huo wa kwanza. Wengine kulia ni Henry Tandau, Katibu wa Kamati na kushoto, Angetile Osiah, Mjumbe wa Kamati.  

Mjumbe wa Kamati, Abdallah Ahmad Bin Kleb 

Kutokas kulia Bin Kleb, Tandau, Dewji, Osiah na Mjumbe mwingine wa Kamati, Salim Abdallah

Salim Abdallah kushoto na Osiah kulia

Makamu Mwenyekiti wa Kamati, KD akizungumza kwa simu na Mwenyekiti wake, Ridhiwani Kikwete ambaye hakuhudhuria mkutano kwa sababu yupo msibani kwao Bagamoyo.  

LADY JAYDEE SASA NDANI YA EATV KATIKA DIARY

Mwanamuziki maarufu nchini, Lady Jaydee (kulia), akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Nyumbani Lounge, Oysterbay, Dar es Salaam kuhusu kipindi chake kipya cha Lady Jaydee Diary, kitakachokuwa kikirushwa hewani na kituo cha East African TV, maarufu kama Channel 5 kila Jumapili saa 3:00 usiku. Kushoto ni Mkuu wa vipindi EATV, Lydia Igarabuza.  



MWANAMUZIKI mkongwe nchini, Lady Jadee ameanzisha kipindi cha TV kiitwacho Diary Ya Lady Jaydee, kitakachokuwa kikirushwa hewani na kituo cha East African TV, maarufu kama Channel 5 kila Jumapili saa 3:00 usiku.
Kama msanii, Lady Jaydee amefanikiwa na kutambulika katika kiwanda cha muziki ndani na nje ya nchi, huku akitunukiwa tunzo nyingi zaidi akiwa albamu zake tano. Pamoja na kuwa anaendelea na fani yake ya muziki, Lady Jaydee ameamua kuwafikia na kuwaburudisha wapenzi wa kazi zake kwa njia nyingine.
Lady Jaydee sasa anaanza sura mpya ya burudani kwa kuleta kipindi cha TV kiitwacho DIARY YA LADY JAYDEE, ambacho kutaonekana katika kituo cha TV cha EATV
Diary Ya Lady Jaydee itaonesha maisha na hadithi za kweli za Lady Jaydee kwa lengo la kuburudisha kwa kuonyesha mambo yate mazuri anayopitia au kuyaona Lady Jaydee kuelimisha kwa kushiriki mambo ya kijamii, kutia moyo wengine wafuate ndoto zao kwa uadilifu, kuongeza kipato kama msanii kwa kutangaza biashara mbalimbali na hatimae kudumisha ajira binafsi kwa njia ya sanaa.
Lady Jaydee anatoa shukrani kwa mashabiki kwa kuendelea kumpokea, jambo ambalo linampa nguvu zaidi ya kufanya kaza.
Pia anashukuru sana vyombo vya habari na zaidi anawashukuru EATV na washirika wake kwa kumpa nafasi ya kurusha kipndi chake kipya Diary Ya Lady Jaydee. EATV imekuwa mchango wa aina yake katika kuwakuza wasanii Tanzania.
Lady Jaydee anatoa wito kwa vyombo vya habari kuendelea kushirikiana na naye kwa kila namna, ili kukuza na kuendeleza kipaji chake na sanaa ya muziki wa Tanzania kwa ujumla wake.
Zaidi anatoa wito kwa makampuni kishiriki na kuungana nae ili waweze kumpa nguvu msanii, kutangaza biashara zao na kushawishi ajira katika fani ya muziki.
Na mwisho Lady Jaydee anawaribisha wote kusikiliza CDs zake au kuburidika na kundi lake la Machozi Band au kupata chakula ktk mgahawa wake wa kisasa Nyumbani Lounge au ukiwa umepumzika nyumbani utazame kipindi chake Diary Ya Lady Jaydee ktk EATV.

RHINO RANGERS WAENDELEZA MAUAJI LIGI DARAJA LA KWANZA FDL WAITANDIKA MORAN FC 2-1
 
Timu ya maafande wa jeshi la wananchi  ya mkoani tabora  RHINO RANGERS jana waliendelea  kuwapa raha wakazi wa tabora baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya moran fc ya kiteto manyara kule.
mabao ya rhino rangers hiyo jana yalifungwa  na SHIJA MONGO na ABDALAH SIMBA mshambuliaji ambaye ananguvu ,kasi,mashuti na mtaalaamu wa kumiliki mpira .
Ligi hiyo inaendelea  tena leo tarehe 15 kwa michezo mitatu katika miji  ya   kigoma,shinyanga namwanza.mechi ambazo zitachezwa hii leo ni kati ya  kanembwa vs polisi mara,,,pamba vs polisi tabora na mchezo wa mwisho utakuwa kati ya mwadui vs polisi dodoma
Mechi hizi zimeahirishwa kutokana na kupisha mchezo uliokuwa katika kalenda ya FIFA kati ya taifa stars timu ya taifa ya Tanzania na timu ya harambee stars timu ya taifa ya Kenya.
  MSIMAMO KUNDI C
1.RHINO RANGERS MECHI 7 POINTI 17
2.KANEMBWA JKT MECHI6 POINTI 13
3.MWADUI FC MECHI 6 POINTI 10
4.POLISI DODOMA MECHI  POINTI 8
5.PAMBA MECHI 6 POINTI 8
6.POLISI MARA MECHI 6 POINTI 5
7.POLISI TABORA MECHI 6 POINTI 3
8.MORAN FC MECHI 6 POINTI 2
FAHAMU;Kila kundi litatoa timu moja ambayo itapanda ligi kuu ya vodacom tanzania bara VPL msimu ujao na tayari timu ya maafande ya polisi moro imeonyeshwa mlango wa kutokea kwani imemaliza mzunguko wa kwanza wa  VPL ikiwa imecheza mechi 13 na ina pointi 4 inashika mkia.timu zitakazo panda ni kutoka kundi A,B,na C
 MATOKEO TOKA LIGI IANZE oktoba 24
===Kanembwa vspolisi dodoma 3-0
===pamba vs polisi mara 3-2
===rhino rangers vs polisi tabora 2-1
===mwadui vs moran 3-0
oktoba 27
====polisi tabora vs polisi dodoma 0-1
====mwadui vs polisi mara 3-0
====kanembwa JKT vs moran 2-0
====pamba vs rhino rangers 1-1
oktoba 31
====polisi mara vs rhino rangers 0-0
====moran vs polisi tabora 1-1
====polisi dodoma vs pamba2-0
====kanembwa vs mwadui 3-2
novemba 4
===polisi mara vs polisi tabora 1-1
===moran vs polisi dodoma1-1
===rhino rangers vs kanembwa JKT 3-1
===mwadui vs pamba...2-0......
novemba 7
====polisi tabora vs kanembwa  JKT 1-4
====polisi dodoma vs polisi mara 0-0
====pamba vs moran ya manyara 2-0
novemba 8
====rhino rangers vs mwadui FC 2-0
novemba 11
====kanembwa vs pamba 0-0
====polisi tabora vs mwadui 0-0
====polisi dodoma vs rhino rangers 0-2
====polisi mara vs moran 3-1

 

YONDAN: HAIKUWA KAZI NYEPESI KUMDHIBITI OLIECH

Kevin Yondan

BEKI wa Yanga, Kevin Yondan amesema kwamba licha ua kuwafunga Kenya, Harambee Stars, lakini wapinzani wao hao ni wazuri na zaidi akamsifia mshambuliaji wa klabu ya Daraja la Pili Ufaransa, AJ Auxerre, Dennies Oliech kwamba ni mtu hatari.
Akizungumza  kwa simu kutoka Mwanza jana, Yondan alisema kwamba walifanya kazi kubwa mno kumdhibiti Oliech, kwani mtu huyo ni hatari.
“Yule jamaa anajua, mimi binafsi ilinibidi nitulize sana akili katika kukabiliana naye, ndiyo maana hakufunga, bila hivyo Yule mtu angefunga,”alisema Yondan.
Hata hivyo, beki huyo wa kati alisema timu yao ilicheza vizuri kwa ujumla jana na anaamini hizi ni dalili nzuri za kuwapa Watanzania.
“Tunamshukuru Mungu kwa ushindi huu, lakini tunaendelea kuomba mashabiki wetu waendelee kutupa sapoti ili tufanye vizuri zaidi,”alisema.
Taifa Stars, jana iliibwaga Kenya, Harambee Stars bao 1-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza katika mchezo wa kirafiki ulio katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Hadi mapumziko, Stars ilikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na beki Aggrey Morris katika dakika ya nne, baada ya kupanda kusaidia mashambulizi.
Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa anayetambuliwa na FIFA, Oden Mbaga, Kenya walitawala dakika 10 za mwanzo, lakini baada ya hapo Stars wakafunguka nao na kuanza kula nao sahani moja na Harambee Stars.
Kipindi cha pili, Kenya walianza na mabadiliko kocha Henri Michel akiwapumzisha James Situma, Jerry Santo na Wesley Kemboi na kuwaingiza Christopher Wekesa, Anthony Akumu na Timbe Ayoub.
Pamoja na mabadiliko hayo, mambo yaliendelea kuwa magumu kwa Harambee Stars, kwani wenyeji waliendelea kucheza kwa makini, wakishambulia na kujilinda zaidi.
Kocha wa Stars naye, Mdemnark, Kim Poulsen aliwatoa Amir Maftah, Salum Abubakar, Mwinyi Kazimoto, Mbwana Samatta, Mrisho Ngassa na Thomas Ulimwengu na kuwaingiza Nassor Masoud ‘Chollo’, Amri Kiemba, Simon Msuva, John Bocco ‘Adebayor’, Shaaban Nditi  na Issa Rashid.  
Baada ya mchezo huo, kocha wa Harambee, Mfaransa Michel alionyesha kukerwa na matokeo hayo na kusema timu yake haikucheza vizuri, wakati Polusen, amefurahia ushindi huo akisema timu yake haijacheza kwa miezi miwili na baada ya siku mbili za mazoezi wameifunga Kenya. 
Taifa Stars; Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Amir Maftah/Nassor Masoud ‘Chollo’ dk70, Aggrey Morris, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar/Amri Kiemba dk69, Mwinyi Kazimoto/Simon Msuva dk69, Mbwana Samatta/John Bocco dk 84, Mrisho Ngassa/Shaaban Nditi dk72 na Thomas Ulimwengu/Issa Rashid dk 89.  
Harambee Stars; Frederick Onyango, Brian Mandela, Eugene Asike, James Situma/Christopher Wekesa dk 46, Edwin Wafula, Jerry Santo/Anthony Akumu dk 46, Peter Opiyo/Charles Okwemba dk 67, Patrick Obuya, Patrick Osaika/Mulienge Ndeto dk 73, Dennis Oliech na Wesley Kemboi/Timbe Ayoub dk 46.
REKODI YA STARS MWAKA HUU NA RATIBA YA MECHI ZIJAZO:
Februari 23, 2012
Tanzania 0 – 0 DRC (Kirafiki)
Februari 29, 2012
Tanzania 1 – 1 Msumbiji   (Kufuzu Mataifa ya Afrika)
Mei 26, 2012
Tanzania 0 – 0 Malawi
Juni 2, 2012
Ivory Coast 2 – 0 Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 10, 2012
Tanzania 2 – 1 Gambia      (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 17, 2012
Msumbiji 1 – 1 Tanzania   (Tanzania ilitolewa kwa penalti kufuzu Mataifa ya Afrika)
Agosti 15, 2012
Botswana 3 – 3 Tanzania (Kirafiki)
Novemba 14, 2012
Tanzania 1-0 Kenya (Kirafiki)
Machi 22, 2013
Tanzania Vs Morocco (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 7, 2013
Morocco Vs Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 14, 2013    
Tanzania Vs Ivory Coast    (Kufuzu Kombe la Dunia)
Septemba 6, 2013
Gambia    Vs Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)

HATIMA YA MILOVAN SIMBA LEO, KIKAO KIZITO MNO CHAFANYIKA

Kocha wa Simba SC, Milovan Cirkovick kushoto akiwa ameishiwa nguvu baada ya kufungwa na Toto Africans mwishoni mwa wiki katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kulia ni wachezaji wake, Shomary Kapombe na Jonas Mkude.

KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Simba ya Dar es Salaam inatarajiwa kuwa na kikao kizito leo, kujadili mambo mbalimbali kuhusu mustakabali wa klabu hiyo na mwenendo wa timu yao ya soka kwa ujumla.
Habari kutoka ndani ya Simba, zimesema kwamba kikao hicho kitashirikisha Wajumbe wote wa Kamati hiyo, chini ya Mwenyekiti wake, Alhaj Ismail Aden Rage.
Miongoni mwa ajenda zinazotarajiwa kuwa mjadala nzito ni matokeo ya timu hiyo kushika nafasi ya tatu katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, licha ya kuanza vyema na kufikia kuongoza kwa wastani wa pointi saba zaidi.
Aidha, katika kikao hicho, habari zinasema Makamu Mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ atawasilisha rasmi barua ya kujiuzulu kwake uongozi, kufuatia kuibuka watu wanaompinga na kushinikiza ajiuzulu.
Lakini pia bado mjadala mpana utakuwa kuhusu mustakabali wa timu kuelekea mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Litajadiliwa suala la kipa Juma Kaseja kuomba kung’atuka baada ya kufanyiwa fujo na mashabiki.
Litajadiliwa suala la kusimamishwa kwa beki Juma Said Nyosso na kiungo Haruna Moshi ‘Boban’. Litajadiliwa suala la kuboreshwa kwa timu kuelekea mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa mwakani.
Lakini pia habari zinasema litajadiliwa pendekezo la kutaka kocha wa timu hiyo, Mserbia Profesa Milovan Cirkovick aondolewe na masuala mengine ya msingi, kama salio la malipo ya kiwanja, ambacho klabu hiyo inataka kujenga uwanja wake wa michezo. 
Kwa ujumla, hamkani si shwari ndani ya Simba hivi sasa, baada ya mabingwa hao wa Ligi Kuu kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu wakiwa katika nafasi ya tatu, tena wakizidiwa pointi sita na wapinzani wao wa jadi, Yanga wanaoongoza ligi hiyo.

CHEKA KUPANDA ULINGONI ARUSHA KUMVAA MWAHILA

Bondia maarufu kuliko wote Tanzania Francis Cheka atamvaa Udiadia Mwahia kutoka nchini DRC Kongo kugombea mkanda wa ubingwa wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi.
Mabondia hao watakutana katika mpambano wa kwanza tangu Arusha liwe jiji katika uwanja wa Shekh Amri Abeid tarehe 26 Desemba 2012 siku ya Boxing Day!

Akimtambulisha Francis Cheka kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa Maelezo jijini Dar Es Salaam jana , mratibu wa mpambano huo na ambaye alishawahi kuwa bingwa wa Tanzania kwenye ngumi za ridhaa George Andrew alisema kuwa bondia Udiadia Mwahila anakaa Lusaka Zambia ambako ndipo anapofanya shughuli zake za ngumi chini ya promota maarufu Anthony Mwamba!
 Udiadia ana rekodi ya mapambano 12 na ametoka sare pambano moja na hajapoteza hata moja wakati Francis Cheka ana rekodi ya mapambano 33 amepoteza 6 na kutoka sare pambano moja.
George alisema kuwa mpambano huo utatumika kulitangaza jiji la Arusha kama Las Vegas ya ngumi katika bara la Afrika na kulifananisha jiji la Arusha na jiji la Geneva lililoko nchini Switzerland.

Mpambano huo unakuja wakati ambapo mpambano mwingine wa Francis Cheka na bondia kutoka Ujerumani wa kugombea mkanda wa IBF wa mabara ulifutwa baada ya Simon kuumia katika mazoezi.
Naye Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Ghuba ya Uajemi Onesmo Ngowi alisema kuwa wao kama IBF wamesharuhusu maandalizi ya mpambano huo. Rais huyo aliwataka wadhamini pamoja na wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa mingine kujitokeza kwa wingi ili kulifanya pambano hilo kuwa la mafanikio.
 Naye bondia Francis Cheka alisema kuwa amejiandaa kwa kiasi kikubwa na atazidi kufanya mazoezi ili kupata ushindi kwake pamoja na nchi ya Tanzania. Aliendelea kusema kuwa kila Mtanzania anajua uwezo wake kwa hiyo amewataka wote wafike kwa wingi ili kupata uhondo na burudani tosha

 

MWAKALEBELA KUANZA HARAKATI ZA KUMNG'OA BAYI TOC LEO HII

Habari za uhakika kutoka kwa aliyekuwa katibu mkuu wa TFF katika awamu ya kwanza ya uongozi wa Leadgar Tenga, Bwana Frederick Mwakalebela ni kwamba kesho asubuhi ataenda kuchukua fomu za kugombea uongozi wa ukatibu mkuu wa kamati ya Olimpiki Tanzania.

Mwakalebela ambaye ni mmoja ya wadau wenye kuonyesha nia ya dhati katika kukuza michezo kwa kutoa misaada mbalimbali pamoja na kuandaa michuano kama 'Mwakalebela CUP' ambayo imekuwa ikitoa vipaji vingi amesema ameamua kuchukua fomu ya kugombea ukatibu mkuu kwa sababu anaamini ana uwezo na nia ya dhati ya kuongoza kamati hiyo ili kuiwezesha nchi yetu ipige hatua zaidi katika michezo.

Kuchukua fomu kwa Mwakalebela kunamaanisha katibu mkuu huyo wa zamani wa TFF, ameanza mbio za kumng'oa madarakani kidemokrasia Fibert Bayi ambaye amekuwa kiongozi wa kamati hiyo kwa muda mrefu sasa.

Leo ndio siku ya mwisho ya kuchukua fomu.

MATAIFA HURU YA AFRIKA: MAREFA KUFICHWA KUEPUSHA UPANGAJI WA MATOKEO

Marefa  wa fainali zijazo za kombe la mataifa huru ya Afrika watawekwa mbali na watu wengine wakati wa michuano hiyo nchini South Africa ili kuzuia upangaji wa matokeo.

Hali ya ulinzi ilitumika pia katika fainali ya za kombe la dunia mwakak 2010 zilizofanyika nchini SA.

CEO wa kamati ya ndani ya uandaaji Mvuso Mbebe alisema: "Marefa watakuwa mafichoni katika hotel mojawapo ambayo hakuna mtu atakuwa na uwezo wa kuwafikia.

"Hawatokuwa na uwezo wa kuwasiliana na mtu yoyote kutoka nje, kwa sababu hatuwezi kujua nini kinaweza kufanyika katika mawasiliano yao na watu wasioruhusiwa.

Aliongeza: "Watakuwa wanaondoka hotelini, chini ya ulinzi mkali utakaokuwa ukisindikizwa na vikosi maalum vya ulinzi, hali itaendelea mpaka mwisho wa michuano."

Shrikisho la soka la Afrika limepitisha hatua hiyo ya ulinzi wa marefa ambao utaanza kuanzia January 19 mpaka February 10

 

MECHI za KIMATAIFA: Sweden, Ibrahimovitch, waichapa England 4-2! 

>>FRANCE yaifunga ITALY, MESSI ashindwa kutamba JANGWANI, GERMANY, HOLLAND sawa!!

>>BRAZIL 2014: Japan yashinda ugenini, yachungulia safari ya Brazil!!
FIFA_LOGO_BESTWakicheza kwenye Uwanja mpya wa Friends Arena Nchini Sweden, Wenyeji Sweden waliitwanga England Bao 4-2 huku bao zote za Sweden zikifungwa na Straika hatari Zlatan Ibrahimovic.
Bao za England zilifungwa na Danny Welbeck na Caulker.
France, wakicheza ugenini, waliifunga Italy Bao 2-1 kwa bao za Valbuena na Gomis na Bao la Italy kufungwa na Stephan El Shaarawy.
Vigogo Germany na Netherlands walitoka sare ya 0-0.
Huko Jangwani Nchini Saudi Arabia, Nyota Lionel Messi jana alishindwa kuivunja rekodi nyingine ya kuifungia Nchi yake Argentina Bao nyingi ndani ya Mwaka mmoja walipotoka 0-0 na Saudi Arabia.
Nayo Brazil ilitoka 1-1 na Colombia huku Neymar akiifungia Brazil na Cuadrado akiipatia Bao Colombia.
Mabingwa wa Dunia Spain waliicharaza Panama Bao 5-1.
Katika Mechi za Mchujo za kuwania kwenda Brazil 2014 kwenye Fainali za Kombe la Dunia, Japan ilipata ushindi wa ugenini wa Bao 2-1 dhidi ya Oman na matokeo hayo yamewafanya wawe karibu kabisa kufuzu wakiwa na Pointi 13 katika Kundi B huku Timu ya Pili, Australia, ikiwa na Pointi 5 tu.
MECHI ZA KIMATAIFA ZA KIRAFIKI:
MATOKEO:
Jumatano Novemba 14
Kuwait 1 Bahrain 1
Rwanda  2 Namibia 2
Niger  1 Senegal 1
Angola v Congo
Lesotho v Mozambique
Tanzania 1 Kenya 0
Congo, DR 0 Burkina Faso 1
South Korea 1 Australia 2
Cape Verde 0 Ghana 1
China 1 New Zealand 1
Malaysia 1 Hong Kong 1
Georgia  0 Egypt 0
Russia  2 United States 2
United Arab Emirates 2 Estonia 1
Bulgaria 0 Ukraine 1
Czech Republic 3 Slovakia 0
Andorra  0 Iceland 2
Macedonia 3  Slovenia 2
Algeria  0 Bosnia And Herzegovina 1
Cyprus 0 Finland 3
Israel 1 Belarus 2
Armenia 4 Lithuania 2
Saudi Arabia 0 Argentina 0
Tunisia 1 Switzerland 2
South Africa 0 Zambia 1
Liechtenstein 0 Malta 1
Morocco 0 Togo 1
Romania 2 Belgium 1
Chile 1 Serbia 3
Turkey 1 Denmark 1
Luxembourg 1 Scotland 2
Austria 0 Ivory Coast 3
Hungary 0 Norway 2
Gabon 2 Portugal 2
Sweden 4 England 2
Netherlands 0 Germany 0
Poland  1 Uruguay 3
Ireland 0 Greece 1
Albania 0 Cameroon 0
Italy  1 France 2
Alhamisi Novemba 15
Panama 1 Spain 5
Honduras 0 Peru 0
Paraguay 3 Guatemala 1
Brazil 1 Colombia 1
Venezuela 1 Nigeria 3
Bolivia  1 Costa Rica 1
KOMBE LA DUNIA Brazil 2014: Bara la Asia=MCHUJO
Jumatano Novemba 14
Oman 1 Japan 2
Iraq 1 Jordan 0
Qatar 1 Lebanon 0
Iran 0 Uzbekistan 1
Msimamo:
Kundi A:
1 Uzbekistan Mechi 5 Pointi 8
2 South Korea Mechi 4 Pointi 7
3 Iran Mechi 5 Pointi 7
4 Qatar Mechi 5 Pointi 7
5 Lebanon Mechi 5 Pointi 4
Kundi B:
1 Japan Mechi 5 Pointi 13
2 Australia Mechi 4 Pointi 5
5 Iraq Mechi 5 Pointi 5
3 Oman Mechi 5 Pointi 5
4 Jordan Mechi 5 Pointi 4
 

MAN UNITED: Deni lao lapungua!!

Deni ambalo linaikabili Manchester United limeshuka kwa Asilimia 18 baada ya Klabu hiyo kuuza Hisa kwenye Soko la Hisa la New York na kuongeza Mapato kupitia Udhamini mpya na kulifanya Deni hilo liporomoke toka Pauni Milioni 436.9 hapo Juni 30 na kufikia Pauni Milioni 359.7 mnamo Septemba 30.
MAN_UNITED_WALLKwa mujibu wa Takwimu za Mahesabu zilizotolewa leo zinaonyesha Man United ilipata Faida ya Pauni Milioni 20.5 kwa Kipindi cha Miezi mitatu iliyoishia Septemba 30.
Mapato ya Kibiashara kwa Klabu yako kwenye malengo na yanategemewa kufikia si chini ya Pauni Milioni 350 Milioni kwa Mwaka huu wa Fedha baada ya kukua kwa Asilimia 24.
Katika Miezi hiyo mitatu, Wadhamini 10 waliingia Mkataba na Klabu ikiwa ni pamoja na Kampuni kubwa ya Magari huko Marekani General Motors ambayo Nembo ya Gari lake la aina ya Chevrolet itaanza kuoneka kwenye Jezi za Man United kuanzia Msimu wa Mwaka 2014/15.
Licha ya kutotwaa Taji lolote Msimu uliopita, Man United Msimu huu ndio inaongoza Ligi Kuu England na tayari imesonga mbele kwenye Raundi nyingine ya UEFA CHAMPIONZ LIGI huku ikiwa na Mechi mbili mkononi na pengine hii ni kwa sababu ya kuimarisha Kikosi kwa kuwanunua Wachezaji wapya.
Man United imewanunua Shinji Kagawa, Nick Powell na Robin van Persie.
Man United inamilikiwa na Familia ya Kimarekani ya kina Glazer ambao walinunua Mwaka 2005 kwa kutumia Mikopo toka Benki mbalimbali na kuiingiza Klabu hii ambayo ilianzishwa Mwaka 1878 kwenye Deni kubwa ingawa ina Mapato makubwa Kibiashara.
HUKO NYUMA==
TULIANDIKA: Jumanne, 16 Novemba 2010 20:25
Wadau wa Manchester United, hasa Kikundi cha Mashabiki kiitwacho MUST [Manchester United Supporters Turst] kimekuwa kikiwapinga Familia ya Glazer kwa kuitumbukiza Man United kwenye deni na wasiwasi huo ulisababisha kuibuka kwa upinzani uliotaka kuwabwaga Familia hiyo ya Kimarekani na Mashabiki wakivaa Jezi za Kijani na Dhahabu wakati wa mechi za Man United.GREEN_n_GOLD_OF_MAN_UNITED
Rangi za kijani na dhahabu ni rangi za Klabu ya Newton Heath iliyoanzishwa mwaka 1878 na hapo tarehe 26 Aprili 1902 kubadilishwa jina kuitwa Manchester United na rangi kuwa nyekundu, nyeusi na nyeupe zinazotumiwa mapaka sasa.
Newton Heath ilianzishwa na Wafanyakazi wa Depo iliyokuwepo eneo lla Newton Heath la Reli ya Lancashire na Yorkshire..
Mwaka 2005 Familia ya Matajiri kutoka Florida Marekani iitwayo Glazer iliinunua Manchester United na kuiingiza kwenye deni kubwa ambalo, ingawa Menejimenti ya Klabu inadai hilo deni ni kitu cha kawaida na uwezo wa kulilipa upo, Washabiki hawapendeziwi nalo na wameanzisha upinzani mkubwa kwa Familia ya Glazer.
Ndio maana Mashabiki, kwenye mechi za Manchester United, wanavaa skafu, fulana na kofia rangi za kijani na dhahabu ikiwa ni alama ya chimbuko la Manchester United, Klabu ya Newton Heath iliyoanzishwa na Wafanyakazi makabwela wa Depo ya Reli.
Nje ya Uwanja wa Old Trafford fulana za rangi hiyo ya kijani na dhahabu huuzwa huku nyuma zina maandishi [Shairi la Kiingereza] na tafsiri ya haraka ni:
“Roho ya United haiuzwi, Ndio maana kwa fahari tunavaa Kijani na Dhahabu,
Hatutavaa ile Jezi Nyekundu inayosifika, Mpaka Glazer waondoke au wafe,
Hivyo inua viwango vya zamani juu, Kwa Kijani na Dhahabu tutaishi na kufa,
Na hakika siku itafika tena, Tutakapovaa Nyekundu yetu kwa mara nyingine tena!”

GOLI BORA DUNIANI 2012: FIFA yatangaza Wagombea 10!


>>MESSI, NEYMAR wamo, RONALDO hana Bao!!
>>KUPIGIWA KURA, Mshindi kujulikana Januari 7, 2013!!
NEYMAR_v_MESSIZile mbio za kumpata Mshindi wa Tuzo ya FIFA ya PUSKAS kwa ajili ya GOLI BORA la MWAKA zimeanza leo kwa kutangazwa Wagombea 10 na Mabao yao bila ya Jina la Mshindi wake wa kwanza kabisa wa Tuzo hiyo, Cristiano Ronaldo, kuwemo.
Mashabiki Dunia nzima ndio watapiga Kura kuamua lipi Goli Bora kati ya Mabao 10 yaliyoteuliwa na Wataalam wa FIFA.
Mchujo wa kupata Magoli matatu Bora utakamilika hapo Novemba 29 na itaanza Kura nyingine kuchagua Goli Bora kati ya hayo matatu ambapo Mshindi atatangazwa Januari 7, 2013, Siku ambayo pia Dunia itamjua nani atatwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani, FIFA Ballon d’Or.
Tuzo ya FIFA ya PUSKAS kwa ajili ya GOLI BORA la MWAKA ilianzishwa Mwaka 2009 na Mshindi wake wa kwanza ni Cristiano Ronaldo alipofunga Bao katika Mechi ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ya Manchester United dhidi ya FC Porto.
+++++++++++++++++++++++++++++
WASHINDI WALIOPITA:
-2011==Neymar: Goli Santos v Flamengo
-2010==Giovanni van Bronckhorst: Goli Netherlands v Uruguay
-2009==Cristiano Ronaldo: Goli Man United v FC Porto
+++++++++++++++++++++++++++++
Tuzo hii ya Puskas ni kwa heshima na kumbukumbu ya Ferenc Puskás, Nahodha na Nyota wa Hungary katika Miaka ya 1950.
WAGOMBEA GOLI BORA:
Agyemang BADU (Ghana - Guinea 1 February 2012)
Hatem BEN ARFA (Newcastle United - Blackburn Rovers 7 January 2012)
Radamel FALCAO (América de Cali - Atletico Madrid 19 May 2012)
Eric HASSLI (Vancouver Whitecaps - Toronto FC 16 May 2012)
Olivia JIMENEZ (Mexico - Switzerland 22 August 12)
Gastón MEALLA (Nacional Potosí - The Strongest 29 January 2012)
Lionel MESSI (Brazil - Argentina 9 June 2012)
NEYMAR (Santos - Internacional 7 March 2012)
Moussa SOW (Fenerbahce - Galatasaray 17 March 2012)
Miroslav STOCH (Fenerbahçe - Gençlerbirliği 3 March 2012

BPL: Kilingeni Jumamosi, kuanza DABI ya London Arsenal v Spurs!!

WALCOTT_WILSHERE_OX
>>DABI hii ni MSHIKEMSHIKE kwa WENGER na VILLAS-BOAS!!!
Baada ya Mechi za Kimataifa za Kirafiki za katikati ya Wiki, Wikiendi hii Ligi Kuu England, BPL, inarudi kwa kishindo na Mechi ya kwanza kabisa Siku ya Jumamosi ni Dabi ya Jiji la London kati ya Arsenal na Tottenham itakayochezwa Uwanja wa Emirates na Mechi ya mwisho Siku hiyo hiyo ni kati ya Norwich City na vinara wa Ligi Manchester United itakayochezwa Uwanja wa Carrow Road.
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi, Novemba 17, 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Arsenal v Tottenham Hotspur
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Wigan Athletic
Manchester City v Aston Villa
Newcastle United v Swansea City
Queens Park Rangers v Southampton
Reading v Everton
West Bromwich Albion v Chelsea
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Norwich City v Manchester United
+++++++++++++++++++++++
Arsenal na Tottenham zitaingia kwenye Dabi hiyo huku zikiwa nafasi ya 7 kwa Tottenham na ya 8 kwa Arsenal na kila mmoja atawania ushindi ili kujiiimarisha zaidi hasa baada ya kuwa na mwendo mbovu kwenye Ligi Msimu huu.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
1 Man United Mechi 11 Pointi 27
2 Man City  Mechi 11 Pointi 25
3 Chelsea Mechi 11 Pointi 24
4 Everton Mechi 11 Pointi 20
5 WBA Mechi 11 Pointi 20
6 West Ham Mechi 11 Pointi 18
7 Tottenham Mechi 11 17
8 Arsenal Mechi 11 Pointi 16
+++++++++++++++++++++++
Ikiwa Timu moja itafungwa basi presha kwa Mameneja, Arsene Wenger wa Arsenal na Andre Villas-Boas, itazidi na Wadau wengi watainua Mabango kukandamiza kuwa Klabu ipo mashakani.
Ndio maana Mechi hii ni muhimu mno kwa kila Klabu hasa ukizingatia mwendo wao mbovu wa hivi karibuni ambapo Arsenal wameshinda mara moja tu katika Mechi 8, tena dhidi ya Klabu ya mkian QPR, na wamefungwa jumla ya bao 12 katika Mechi zao 4 zilizopita na wenzao Tottenham wakifungwa katika Mechi 3 kati ya 4 walizocheza mwisho.
+++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumapili, Novemba 18, 2012
[SAA 1 Usiku]
Fulham v Sunderland
Jumatatu, Novemba 19, 2012
[SAA 5 Usiku]
WestHam v Stoke City

No comments:

Post a Comment