Saturday, October 6, 2012

CAF CHAMPIONZ LIGI: KESHO Samatta kuipeleka Mazembe Fainali??

Jumamosi, 06 Oktoba 2012 14:13
   
Straika mahiri wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta, kesho ataongoza majeshi ya Klabu yake TP Mazembe kucheza na Mabingwa watetezi wa Afrika, Espérance Sportive de Tunis, ya Nchini Tunisia, katika Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI itakayochezwa huko Stade TP Mazembe, Mjini Lubumbashi, Congo.


Timu hizo zitarudiana huko Tunisia hapo Oktoba 20.
Nusu Fainali nyingine ya Mashindano haya itachezwa huko Nigeria hivi leo kati ya wenyeji Sunshine Stars na Vigogo wa Misri Al Ahly.


Timu hizi zitarudiana huko Cairo hapo Oktoba 21.
Washindi wa Nusu Fainali hizi watacheza Fainali Mwezi Novemba na Bingwa ndie ataiwakilisha Afrika kwenye Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani yatakayochezwa huko Japan Mwezi Desemba.


NUSU FAINALI:
[SAA za BONGO]
Jumamosi Oktoba 6        
17:00 Sunshine Stars – Nigeria v Al Ahly - Egypt
Jumapili Oktoba 7         
17:30 TP Mazembe - Congo, DR v Espérance Sportive de Tunis – Tunisia [Stade TP Mazembe Lubumbashi]
MARUDIANO
Jumamosi Oktoba 20         
22:30 Espérance Sportive de Tunis – Tunisia v TP Mazembe - Congo, The Democratic Republic Of The [Stade El Menzah]
Jumapili Oktoba 21         
20:30 Al Ahly – Egypt v Sunshine Stars – Nigeria [Cairo International Stadium]
 

Del Bosque: ‘Juan Mata hana nafasi Spain!’

Jumamosi, 06 Oktoba 2012 13:05
 
BRAZIL_2014_BESTKocha wa Mabingwa wa Dunia na Spain, Vicente Del Bosque, ametoboa kuwa Staa wa Chelsea Juan Mata ameachwa kwenye Kikosi cha Timu hiyo kwa vile hamna nafasi yake.


Del Bosque alitangaza Kikosi chake kwa ajili ya Mechi za Mchujo za Kundi I kwa Kanda ya Ulaya kuwania kuingia Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil ambazo watacheza na Belarus Oktoba 12 ugenini na kisha kucheza nyumbani na France hapo Oktoba 16.



Kwenye Kundi I, Spain wamecheza Mechi moja na kuifunga Georgia bao 1-0.
+++++++++++++++++++++

MSIMAMO:
KUNDI I:
1 France Mechi 2 Pointi 6
2 Spain Mechi 1 Pointi 3
3 Georgia Mechi 2 Pointi 3
4 Finland Mechi 1 Pointi 0
5 Belarus Mechi 2 Pointi 0


FAHAMU: Washindi 9 wa kila Kundi wataingia Fainali moja kwa moja na Washindi wa Pili 8 bora wenye rekodi nzuri dhidi ya Timu zilizomaliza nafasi za Kwanza, Tatu, Nne na Tano kwenye Kundi lao watapelekwa kwenye Droo kupanga Mechi 4 za Mchujo, zitakazochezwa nyumbani na ugenini, ili kupata Timu nne zitakazoingia Fainali.
+++++++++++++++++++++
Ingawa wengi huko Spain wameshangazwa na kutochukuliwa Juan Mata hasa ukizingatia fomu yake ya sasa na Klabu yake Chelsea lakini Del Bosque amesema: “Hatukuweza kupata nafasi yake. Tunao Wachezaji wa kutosha kwa michezo hii. Tumechagua wale tunaohisi wanafaa kwa Mechi hizi.”


KIKOSI KAMILI:
Makipa: Iker Casillas [Real Madrid], Victor Valdes [Barcelona], Jose Manuel Reina [Liverpool]


Mabeki: Raul Albiol [Real Madrid], Sergio Ramos [Real Madrid[ , Juanfran [Atletico Madrid     ], Alvaro Arbeloa [Real Madrid], Ignacio Monreal [Malaga], Jordi Alba [Barcelona]

Viungo: Sergio Busquets [Barcelona], Xabi Alonso [Real Madrid], Cesc Fabregas [Barcelona], Andres Iniesta [Barcelona], Xavi Hernandez [Barcelona], Benat Etxebarria [Real Betis], Javi Martinez [Bayern Munich], Santi Cazorla [Arsenal], David Silva [Manchester City]
 
 
Washambuliaji: Pedro [Barcelona], Jesus Navas [Sevilla], Roberto Soldado [Valencia], David Villa [Barcelona], Fernando Torres [Chelsea]
 

MANCINI alia na RATIBA!!

Jumamosi, 06 Oktoba 2012 08:03
 
>>LEO kuikwaa Sunderland ikiwa ni Siku 2 tu baada ya Dortmund!!
>>NI SUNDERLAND Msimu uliopita walitoka 3-3 na kufungwa nao 1-0!!
MANCINI_n_WENGERKILE kilio cha Siku nyingi cha Sir Alex Ferguson na Arsen Wenger kuitaka FA pamoja na Wasimamizi wa Ligi Kuu England ‘kuzilinda’ Timu za England zinazoshiriki michuano ya Klabu Barani Ulaya sasa kimeangukia kwa Meneja Roberto Mancini wa Mabingwa Manchester City.


Man City walicheza Mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Jumatano Usiku Uwanja wa Etihad na kutoka sare 1-1 na Mabingwa wa Germany Borussia Dortmund na leo Saa 8 Dak 45 Mchana, Bongo taimu, wanatinga tena Uwanja huo huo kucheza Mechi ya Ligi Kuu na Sunderland.


Mancini amebwata: “Tunahitaji muda wa kupumzika, kupona maumivu na hekaheka za Mechi ya juzi lakini tunacheza Jumamosi mapema! Sielewi hili! Inashangaza unacheza Jumatano Usiku na tena Jumamosi mchana! Tuna Siku 2 na Masaa 12 tu kupumzika!”


Aliongeza: “Hatukucheza vizuri Jumatano lakini tulipoteza nguvu nyingi, tunahitaji kupumzika, tupone. Kwingine kote Timu zinazocheza CHAMPIONZ LIGI hucheza Mechi zao za Ligi ya nyumbani Siku 3 au 4 kabla na baadae hupumzika si chini ya Siku 3 baada ya Mechi ya Ulaya!”


Leo, katika Mechi ya kwanza kabisa ya Ligi Kuu England Wikiendi hii, Man City wanaivaa Sunderland, ambayo Msimu huu haijafungwa, na ambayo Msimu uliopita kwenye Ligi Kuu walitoka nayo 3-3 Uwanjani Etihad na kufungwa nayo bao 1-0 nyumbani kwa Sunderland Stadium of Light.
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Oktoba 6
[Saa 8 Dak 45 Mchana]
Manchester City v Sunderland
[Saa 11 Jioni]
Chelsea v Norwich City
Swansea City v Reading
West Bromwich Albion v Queens Park Rangers
Wigan Athletic v Everton
[Saa 1 na Nusu Usiku]
West Ham United v Arsenal
Jumapili Oktoba 7
[Saa 9 na Nusu Mchana]
Southampton v Fulham
[Saa 11 Jioni]
Tottenham Hotspur v Aston Villa
Liverpool v Stoke City
[Saa 12 Jioni]
Newcastle United v Manchester United
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 6 isipokuwa inapotajwa]
1 Chelsea Pointi 16
2 Everton 13
3 Man United 12
4 Man City 12
5 Tottenham 11
6 WBA 11
7 West Ham 11
8 Arsenal 9
9 Fulham 9
10 Newcastle 9
11 Swansea 7
12 Stoke 7
13 Sunderland Mechi 5 Pointi 7
14 Liverpool 5
15 Aston Villa 5
16 Wigan 4
17 Southampton 3
18 Norwich 3
19 Reading Mechi 5 Pointi 2
20 QPR 2
+++++++++++++++++++++++++++++++++
 

KIFUNGO kwa Kocha wa Juve Conte chapunguzwa kuwa Miezi 4!!

Jumamosi, 06 Oktoba 2012 07:01
 
>>NI ADHABU kwa SKANDALI LA the 'CALCIOSCOMMESSE!!'
ANTONIO_CONTE_of_JUVEKocha wa Mabingwa wa Italy, Juventus, Antonio Conte, amepunguziwa adhabu ya Kifungo cha Miezi 10 hadi Miezi 4 kwa kuhusishwa na Skandali la 'Calcioscommesse'. Kamati ya Olimpiki ya Italy, ambayo ndio yenye jukumu la mwisho kwa Rufaa za michezo Nchini humo, imempunguzia adhabu Conte, mwenye Miaka 43, na sasa anaweza kurudi kwenye Benchi la Juventus kuanzia Desemba 9.
Conte alifungiwa Mwezi Agosti Mwaka huu kuhusu tuhuma za Wachezaji kupanga matokeo Mechi kwenye Mechi mbili na yeye kuhusishwa kwa kujua hujuma hizo lakini akashindwa kuziripoti wakati akiwa Meneja wa Klabu ya Serie B, Siena, katika Msimu wa 2010/11.
Baadae, Conte alisafishwa kwenye Mechi moja na adhabu yake kubaki kwa kuhusishwa na Mechi moja.
Conte alijiunga na Juventus kwenye Msimu wa 2011/12 na kuiongoza Klabu hiyo kongwe kutwaa Ubingwa Msimu huo huo bila kufungwa hata Mechi moja.
Adhabu ya Kifungo cha Miezi 10 ilimaanisha haruhusiwi kukaa kwenye Benchi la Juve wakati wa Mechi na pia haruhusiwi kuingia Vyumba vya Kubadili Jezi wakati wa Mechi lakini aliruhusiwa kuifundisha Timu yake wakati wa mazoezi.
Kifungo cha awali cha Miezi 10 kingemfanya aukose Msimu mzima wa 2012/13 lakini sasa kwa kupunguziwa atazikosa Mechi 15 za Serie A na Mechi zote za Kundi lao za UEFA CHAMPIONZ Ligi, ikiwemo ile ya marudiano na Chelsea.
Pia, Msaidizi wa Conte huko Siena, Angelo Alessio, ambae pia ndie Msaidizi wake hapo Juve, amepunguziwa toka adhabu ya Miezi 8 na kubakishiwa 6.
Skandali hili la 'Calcioscommesse' limehusisha kuchunguzwa kwa Klabu zaidi ya 20 huko Italy.

No comments:

Post a Comment