Wednesday, December 26, 2012

TAARABT NJE MOROCCO AFCON 2013, QPR KUNUFAIKA!!


Kiungo wa QPR Adel Taarabt ameachwa kwenye Kikosi cha Morocco kitakachocheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, zitakazochezwa huko Afrika Kusini kuanzia tarehe 19 Januari 2013.
Juzi, Taarabt, mwenye Miaka 23, alitangaza kuwa akichaguliwa ataichezea Morocco AFCON 2013 msimamo ambao ulipokelewa kwa masikitiko na Klabu yake QPR ambayo iko mkiani kwenye Ligi Kuu England na yeye ndio tegemezi lao kubwa.
Wachezaji wanaocheza Ligi Kuu England ambao wamechukuliwa na Morocco ni Mchezaji wa Liverpool Oussama Assaidi na Karim El Ahmadi wa Aston Villa.
+++++++++++++++++++
MECHI ZA QPR AMBAZO ANGEZIKOSA TAARABT AKIWA AFCON 2013:
-19 Jan - West Ham v QPR
-29 Jan - QPR v Man City
-2 Feb - QPR v Norwich
-9 Feb - Swansea v QPR
+++++++++++++++++++
Kocha wa Morocco Rachid Taoussi ameteua Wachezaji 24 na atalazimika kumtema Mchezaji mmoja kabla Fainali hizo kuanza.
Taarabt, ambae ameichezea Morocco Mechi 15 na kufunga Bao 4, amekuwa na uhusiano mbovu na Nchi yake na kuna wakati aligomea kuichezea.
Kwenye AFCON 2013, Morocco wapo Kundi A pamoja na Wenyeji Afrika Kusini, Angola na Cape Verde.
KIKOSI KAMILI (Kwenye Mabano ni Klabu za Morocco labda itajwe):
MAKIPA: Nadir Lamyaghri (Wydad Casablanca), Anas Zniti (MAS), Khalid Askiri (Raja Casablanca)
MABEKI: Abderahim Chakir and Younes Bekakhdar (both FAR Rabat), Mehdi Benatia (Udinese, Italy), Issam El Adoua (Guimaraes, Portugal), Ahmed Kantari (Stade Brest, France), Abdelhamid El Kaoutari (Montpellier, France), Zakarya Bergdich (Lens, France)
VIUNGO: Karim El Ahmadi (Aston Villa, England), Adil Hermach (Al Hilal, Saudi Arabia), Kamal Chafni (Stade Brest, France), Mehdi Namli (Moghreb Tetouan), Younes Belhanda (Montpellier, France), Abdelaziz Barrada (Getafe, Spain), Chahir Belghazouani (Ajaccio, France)
MAFOWADI: Oussama Assaidi (Liverpool, England), Adeliliah Hafidi (Raja Casablanca), Youssef Kadioui (FAR Rabat) Abderrazak Hamdallah (Olympique Safi), Youssef El Arabi (Granada, Spain), Mounir El Hamdaoui (Fiorentina, Italy), Nordin Amrabat (Galatasaray, Turkey).

FRIEDEL ASAINI MYPA SPURS!
Kipa mkongwe wa Tottenham Hotspur Brad Friedel amekubali kusaini Mkataba mpya utakaomweka hadi Mwaka 2014.
Friedel, alijiunga na Spurs kutoka Aston Villa Mwaka 2011 na ameichezea Klabu hiyo mara 49 na atafikisha Miaka 43 Mkataba wake ukimalizika Mwaka 2014.
Kwa sasa Friedel, ambae aliichezea USA mara 82, ameporwa Nambari Wani hapo Spurs na Kipa wa Kimataifa wa France, Hugo Lloris.
Brad Friedel yupo kwenye Ligi Kuu England tangu Mwaka 1997 na awali alikuwa Klabu za Liverpool na Blackburn.
Kipa huyo ndie anaeshikilia Rekodi ya kwenye Ligi Kuu England ya kucheza zaidi ya Mechi 300 mfululizo.


RIO KUSUBIRI KUSAINI MPYA MWAKANI!!
Beki wa Manchester United Rio Ferdinand amekiri kuwa kitu pakee kitakachompa Mkataba mpya Mwakani wakati Mkataba wake wa sasa utakapomalizika Mwezi Juni ni ikiwa yeye atakuwa fiti bila kuandamwa na majeruhi.
Katika Miaka ya hivi karibuni, Rio amekuwa akiandamwa na majeruhi ya mara kwa mara lakini katika Miezi 18 iliyopita tatizo hilo limepungua na amekuwa akicheza Mechi nyingi.
Hivi majuzi, Meneja wa Man United, Sir Alex Ferguson, alidokeza Rio, mwenye Miaka 34, anaweza kuendelea kucheza kwa Miaka kadhaa na hilo lilileta matumaini ya kuongezewa Makataba.
Mwenyewe Rio ametamka: “Kumsikia Ferguson akisema naweza kucheza kwa Miaka mingine miwili au mitatu kunatia moyo! Lakini nitaangalia hali yangu na kuamua kama niendelee hapo baadae!”

LAMPARD ‘APIGWA BUTI’ CHELSEA, TERRY NAE……!!!
Hivi juzi Mkongwe wa Chelsea alipiga Bao safi katika ushindi wa Bao 8-0 dhidi ya Aston Villa katika Mechi ya Ligi Kuu England lakini habari za kuaminika toka ndani ya Stamford Bridge zimedokeza kuwa Kiungo huyo ameshaambiwa hana lake ndani ya Klabu hiyo na atafute kwingine.
Lampard, Miaka 34, ameshaambiwa yuko huru Januari 1 kusaka Klabu nyingine.
Katika utumishi wake, Lampard ameiwezesha Chelsea kuwa Mabingwa wa Ulaya, Mabingwa wa England mara 3, FA CUP 4 na LIGI CUP 2.
Hali kama ya Lampard pia inaelekea itamkumba Mkongwe mwingine wa Chelsea, Nahodha wao John Terry.

UEFA KUJIKATIA WENYEWE RUFAA KUHUSU ‘WABAGUZI ’SERBIA!!
UEFA inatarajiwa kuzikatia Rufaa Adhabu zote ambazo Serbia imepewa kuhusiana na Mechi yao ya EURO 2013 na England ya Vijana Chini ya Miaka 21 ambayo iligubikwa na tuhuma za Ubaguzi toka Mashabiki wa Serbia kwa Wachezaji wa England na pia vurugu za Maafisa wa Nchi hiyo.
Timu hiyo ya Serbia ya U-21 iliaadhibiwa kwa kutakiwa kucheza Mechi 1 bila Watazamaji na pia kupigwa Faini Pauni 65,000 kwa Ubaguzi wa Washabiki wao waliofanya kwenye Mechi na England U-21 iliyochezwa Uwanja wa Mladost, Mjini Krusevac, Serbia Oktoba 16.
Adhabu hizo zilitolewa na Jopo Huru la Udhibiti na Nidhamu la UEFA lakini leo UEFA, kupitia Tovuti yake, imeamua kuzikatia Rufaa adhabu zote hizo baada ya kupokea malalamiko mengi kuhusu uhafifu wake dhidi ya Tuhuma nzito.
Sambamba na Adhabu hizo kwa Serbia, Wachezaji wa England U-21, Steven Caulker alifungiwa Mechi mbili na Tom Ince, Mechi 1.

No comments:

Post a Comment