ligi daraja la kwanza imeendelea hii leo katika uwanja wa ALLY HASSAN MWINYI kwa mchezo mmoja wa raundi ya tano kati ya RHINO RANGERS NS MWADUI FC na rhino rangers wametoka kifua mbele kwa mabao 2-0 mabao yaliyofungwa na ALLY NUMBA dk 18 na VICTOR HAGAYA dk ya 86 dhidi ya wachimba almasi mwadui ya shinyanga . na wachezaji wawili wa mwadui mapunda ulanga na aman abdalah walitolewa kwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya na mwamuzi SAID SAID kutoka singida na siku ya jumamosi kwa michezo minne katika miji ya kigoma ,tabora,dodoma,na mara,,kanembwa JKT vs atakuwa na pamba katika dimba la lake tanganyika kigoma...polisi dodoma vs rhino rangers katika dimba la jamhuri dodoma,,,polisi tabora vs mwadui katika dimba la ally hassan mwinyi,,na mchezo wa mwisho utakuwa kati ya polisi mara vs moran fc katika dimba lakarume mara kule.
Raundi ya tano ya ligi daraja la kwanza FDLjana iliendelea katika miji mitatu ,tabora,dodoma na mwanza katika KUNDI C .katika uwanja wa ally hassan mwinyi kulikuwa na mechi kati ya polisi tabora na vibonde wa rhino rangers timu ya kanembwa FC ambayo mchezo uliopita ilitandikwa kwa mara ya kwanza toka ligi ianze na wanajeshi wa tabora kwa bao 3-1. Na timu ya kanembwa wameibamiza kwa hasira timu ya maafande wa polisi kwa mabao 4-1 mabao ya kanembwa JKT yamefungwa na ally bilali mwese aliyekuwa mwiba kwa mabeki wa polisi tabora kafunga mabao 3 dakika ya 46,60,na 89 na bao la nne limefungwa na bulian akilimali dakika ya 49.
Na bao la kufutia machozi la polisi tabora limefungwa na ibrahimu musa dakika ya 86 na hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika refarii salehe mmang'ora anapuliza kipenga cha mwisho timu ya JKT kanembwa ilitoka kifua mbele ya mabao 4-1 na kuendelea kuongoza kundi c ikifikisha jumla ya pointi 12 kwa michezo 5.
Kule dodoma kulikuwa na mchezoo kati ya maafande wa polisi dodoma na polisi mara na wametoka sare ya bila kufungana 0-0 na mchezo wa mwisho ulikuwa kati ya pamba na morani FC katika dimba la CCM KIRUMBA mwanza na matokeo bado hatujayapata.Na kesho novemba 8 kutakuwa na mchezo mmoja kati ya rhino rangers na mwadui katika dimba la ally hassan mwinyi na ni mchezo wa mwisho wa raundi ya tano katika kundi C.
MATOKEO TOKA LIGI IANZE oktoba 24
===Kanembwa vspolisi dodoma 3-0
===pamba vs polisi mara 3-2
===rhino rangers vs polisi tabora 2-1
mwadui vs moran 3-0
oktoba 27
====polisi tabora vs polisi dodoma 0-1
====mwadui vs polisi mara 3-0
====kanembwa JKT vs moran 2-0
====pamba vs rhino rangers 1-1
oktoba 31
====polisi mara vs rhino rangers 0-0
====moran vs polisi tabora 1-1
====polisi dodoma vs pamba2-0
====kanembwa vs mwadui 3-2
novemba 4
===polisi mara vs polisi tabora 1-1
===moran vs polisi dodoma1-1
===rhino rangers vs kanembwa JKT 3-1
===mwadui vs pamba...2-0......
AZAM YAFUKUZA KIPA NA MABEKI KWA TUHUMA ZA KUHUJUMU DHIDI YA SIMBA, YANGA
Said Morad, kweli kahujumu timu? |
AZAM FC imewasimamisha wachezaji wake watatu wa safu ya
ulinzi, kipa Deo Munishi ‘Dida’ na mabeki Said Mourad na Erasto Nyoni kwa
tuhuma za kuihujumu timu hiyo katika mechi zake za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara dhidi ya vigogo Simba na Yanga hivi karibuni.
Azam ilifungwa na Simba mabao 3-1 Oktoba 27, mwaka huu kabla
ya kufungwa mabao 2-0 na Yanga Novemba 4, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam katika mechi za Ligi Kuu.
Baada ya kufungwa na Simba, Azam FC ilimfukuza kocha wake
Mserbia, Boris Bunjak na kumrejesha Muingereza, Stewart Hall.
Habari kutoka ndani ya Azam zimesema kwamba baada ya kupata
taarifa hizo, uongozi ulizifanyia kazi taratibu na kujiridhisha kabisa wachezaji
hao watatu walikula njama za kuihujumu timu katika mechi hizo.
Kwa sababu hiyo, uongozi kwanza umewasimamisha wachezaji hao na
hatua zaidi zitafuatia baadaye.
Hata hivyo, Dida hakucheza mechi hata moja kati ya hizo,
kwani Oktoba 27, kikosi cha Azam kilikuwa; Mwadini Ali, Ibrahim Shikanda, Samir Hajji Nuhu, Said Mourad,
Aggrey Morris, Abdulhalim Humud, Jabir Aziz aliyempisha Abdi Kassim, Himid Mao
aliyempisha Kipre Balou, John Bocco ‘Adebayor’ aliyempisha Khamis Mcha ‘Vialli’,
Kipre Herman Tcheche na Salum Abubakar.
Siku hiyo, Azam
walitangulia kufunga dakika ya nne, kupitia kwa Adebayor ambaye alimtoka beki
Mkenya Paschal Ochieng na kumchambua Juma Kaseja, kabla ya Felix Mumba Sunzu Jr.,
kuisawazishia Simba dakika mbili baadaye, akiunganisha kwa kichwa krosi
maridadi ya Mrisho Khalfan Ngassa kutoka wingi ya kulia.
Okwi
aliifungia Simba bao la pili dakika ya 40, baada ya kutokea kizaazaa langoni
mwa Azam kufuatia mpira uliopigwa langoni mwa timu hiyo na Mwinyi Kazimoto na dakika
tano tu tangu kuanza kipindi cha pili, Mganda huyo tena akawainua vitini
mashabiki wa Simba, akifumua shuti la umbali wa mita 19, baada ya kuwatoka
mabeki wa Azam.
Katika mechi
na Yanga, kikosi cha Azam kilikuwa; Mwadini Ally, Erasto Nyoni aliyempisha Samir
Hajji Nuhu, Ibrahim Shikanda, Aggrey Morris na Said Mourad, Jabir Aziz aliyempisha
Ibrahim Mwaipopo, Kipre Balou, Khamis Mcha ‘Vialli’ aliyempisha Abdi Kassim
‘Babbi’, Salum Abubakar, John Bocco na Kipre Tcheche.
Siku hiyo,
mabao ya Yanga yalitiwa kimiani na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Didier
Kvumbangu aliyeunganisha krosi ya Simon Msuva kutoka wingi ya kulia dakika ya
tisa na Mganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ dakika ya 68, akiunganisha krosi ya
Athumani Iddi ‘Chuji’ kutoka wingi ya kulia.
Habari zaidi
zinasema kwamba, uchunguzi unaendelea kufanywa juu ya wachezaji wengine
wanaotuhumiwa kuwa katika mkumbo huo wa kuihujumu timu na ikithibitika ni
ukweli, watachukuliwa hatua pia bila kujali majina yao.
Azam tayari
iko Tanga tangu saa 8:00 mchana wa leo kwa ajili yao ya mchezo wao wa mwisho wa
mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara keshokutwa dhidi ya
Mgambo JKT, Uwanja wa Mkwakwani.
TASWA WAWASHITAKI LIGI KUU MOAT
Mhando kulia akiwa na Mwenyekiti wake, Pinto |
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA)
kimeamua kulipeleka kwa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania
(MOAT), suala la kuzuiwa kwa vituo vya Televisheni na Redio nchini kutangaza
moja kwa moja michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara pamoja na wapiga
picha za Televisheni kuchukua picha kwa ajili ya kutumia kwenye habari.
Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando amesema leo kwamba, hatua hiyo ina lengo la kuomba mwongozo kwa chama
hicho ambacho ndio kinachomiliki vyombo vya habari kuhusiana na suala hili
ambalo limekuwa likilalamikiwa kwa kiasi kikubwa na wanachama wake.
Tayari TASWA imefanya mazungumzo ya awali na MOAT, ambayo
imeridhia iandikiwe barua rasmi ili jambo hilo lijadiliwe kwenye vikao vyake na
baada ya hapo TASWA itapewa mwongozo ambao itautoa kwa waandishi wa habari za
michezo.
“Kwa kuwa Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto pia ni mjumbe wa
MOAT, basi suala hilo tunaamini litafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo, hivyo
tunawaomba waandishi wa habari za michezo waendelee kuwa watulivu na wavumilivu
kipindi hiki na wafanye majukumu yao kama kawaida,”alisema Mhando.
“Siku zote chama chetu kimekuwa na uhusiano mzuri na
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na wadau wengine wote na TASWA haitaki ifike
mahali iwe na mgogoro na chama chochote cha michezo, lakini pia haitakuwa
tayari kuona wanachama wake wakishindwa kutekeleza majukumu yao,”aliongeza.
Wiki iliyopita kulifanyika kikao cha Kamati ya Ligi na baadhi
ya klabu zinazoshiriki ligi hiyo na kuzuia Televisheni na Redio kutangaza moja
kwa moja michezo ya Ligi Kuu pamoja na wapiga picha za Televisheni kuchukua
picha kwa ajili ya kutumia kwenye habari.
Katika kikao hicho ambacho Mwenyekiti wa TASWA, Juma
Pinto alihudhuria kulitoka maelezo
mbalimbali ambayo baadhi ya Wana Habari hawakubaliani nayo na wamekuwa wakitaka
TASWA ichukue hatua uamuzi mgumu.
Mhando amesema sekreterieti ya TASWA imeona si vizuri
kukurupuka kuchukua uamuzi wowote ule kwa sasa kwani yenyewe haina chombo cha
habari, lakini wanaofanya kazi kwenye vyombo vya habari ndiyo wanachama wake,
hivyo amesema itawasilisha MOAT maazimio ya kikao cha Kamati ya Ligi kuhusiana
na jambo hili, tuna hakika tutalimaliza.
Kuhusu Mkutano Mkuu wa TASWA, Mhando amesema Jumatano ya Novemba
16, mwaka huu Kamati ya Utendaji ya TASWA itakutana Dar es Salaam kupitia
ajenda za Mkutano huo na Novemba 18 Mwenyekiti wa TASWA, Juma Abbas Pinto atakutana
na Waandishi Habari kutangaza mdhamini wa mkutano huo pamoja na tarehe rasmi na
mahali utakapofanyika.
“Kutokana na kuandaliwa kwa ajenda mpya ya kuboresha chama na
maslahi ya wanachama wake, TASWA inaendelea kutafuta wadhamini zaidi ili
kuufanya mkutano huo uwe wa siku mbili,”alisema Mhando.
BALOZI WA HENNESSY KUTUA JUMATATU KUTOKA PARIS
MSHINDI EBSS KUPATIKANA KESHO DIAMOND JUBILEE
Washiriki wa EBSS Salma Yussuf Abushir,
Nsami Nkwabi, NshomaNghangasamala, Walter Chilambo na Wababa Mtuka wakiwa na
Ritha Poulsen. Je, nani ataondoka na kitita cha Sh. Milioni 50 kesho?
|
BAADA ya miezi mitatu ya mchuano mkali hatimaye mshindi wa
shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search atapatikana leo katika fainali
kali inayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Mshindi atajinyakulia shilingi milioni hamsini pamoja na
mkataba wa kurekodi kutoka kwa wadhamini pekee wa shindano hilo kampuni ya simu
za mikononi ya Zantel.
Washiriki walioingia kwenye fainali hizo ni EBSS06: Nsami
Nkwabi, EBSS07: Nshoma Ng’hangasamala, EBSS09: Salma Abushiri, EBSS11: Wababa
Mtuka (Dar) na EBSS12: Walter Chilambo (Dar).
Wasanii watakaoburudisha ni Rich Mavoko, Omi Dimpoz, Ben
Paul, Lina, Amini, Mzee Yusuf, Haji Ramadhan, Mwasiti, Ditto, Laila Rashid,
Linex na Barnaba.
Akizungumzia fainali hizo, jaji mkuu wa shindano hilo, Madam
Ritha Paulsen, aliwashukuru watanzania kwa ushirikiano waliowapa toka shindano
limeanza mpaka leo wanahitimisha kwa fainali.
‘Kama mlivyoona
shindano hili toka lilipoanza mwaka huu limekuwa la kimataifa zaidi, hivyo
tarajieni fainali za kipekee na zitakazoweka rekodi kwenye tasnia ya burudani
na ni matarajio yetu kwamba mshindi wa usiku huu atafanya vizuri kwenye muziki’
alisema Madam Ritha.
Kwa upande wake Afsa Biashara mkuu wa Zantel, bwana Sajid
Khan alisisitiza utayari wa kampuni yake katika kuwaendeleza vijana wa
kitanzania kufikia ndoto zao lakini aliomba pia wadau wengine wa sanaa kuwapa
washirikiano washiriki wote.
‘Zantel, pamoja na kumpa mshindi zawadi ya milioni hamsini
lakini pia tutampa mkataba wa kurekodi, na washiriki wengine watapewa nafasi ya
kurekodi wimbo mmoja mmoja lakini juhudi hizi zitafanikiwa ikiwa tutapata
ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wadau’ alisema Khan.
Shindano hilo limekuwa likirushwa hewani na kituo cha runinga
cha ITV, lilianza mwezi wa sita kwa kufanya usaili mikoani, ambalo mwaka huu
lilienda mikoa nane-Mbeya, Dodoma, Mwanza, Tanga, Dar es Salaam, Zanzibar,
Lindi pamoja na Arusha.
Kwa mara ya kwanza pia shindano hilo liliweza kufanya usaili
kwa njia ya simu ili kuwapa nafasi vijana zaidi ambao hawakufikiwa na majaji.
Epiq Bongo Star Search ni kipindi cha televisheni ambacho
huibua vipaji vya muziki kwa vijana wa kitanzania na kinatengenezwa na Benchmark
Productions, na toka kimeanzishwa mwaka 2006 kimekuwa ni kipindi kinachotazamwa
zaidi Afrika mashariki kwa kufikisha watu milioni 3 wanaotazama kwa kila
kipindi.
Mwaka huu kinadhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi ya
Zantel, na mshindi atapata zawadi ya shilingi milioni 50 pamoja na mkataba wa
kurekodi.
FILAMU YA SHUJAA KUMPONGEZA RAIS KIKWETE KUZINDULIWA DESEMBA
Mwigizaji wa filamu hiyo, Henry Babuu kushoto na Barbra
Kalugira kulia, Meneja Masoko na Mratibu wa filamu hiyo
|
Isakwisa Kanyenyela kushoto na Adam Semkwiji ‘Snare’ na
Innocent Nyika, waliohusika katika idara za kitaalamu kwenye kutayarisha filamu
hiyo.
|
KAMPUNI ya Afronode Films, imeandaa filamu maalum
iliyopachikwa jina la Shujaa ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Jakaya Kitwete kwa kuhamasisha wananchi kupima ukimwi kwa hiyari.
Akizungumza mjini Dar es salaam leo, Meneja Masoko wa kampuni
hiyo, Barbra Kalugira, alisema kuwa kila kitu kimekamlika ambapo uzinduzi wake
utafanyika Desemba mosi ambayo ni siku ukimwi duniani.
Kalugira alisema kuwa katika filamu hiyo itazungumzia watu
kwenda kupima kwa hiyari kama alivyofanya Rais wa Tanzania ambaye ndiye
kiongozi pekee katika ukanda wa Afrika kuhamasisha kupima ukimwi.
"Ni kitendo cha kumpongeza sana Rais wetu kwa kwenda
kupima kwa hiyari na kuhamasisha wananchi wote wajitokeze kupima hivyo tunazindua
filamu hiyo ambayo inazungumzia janga la ukimwi na madhara ya
kutopima"alisema Kalugira.
Pia Kalugira alisema kuwa katika filamu hiyo itamzungumzia
kijana mmoja ambaye alikataa kwenda kupima alipokutana na msichama ambaye ni
muadhirika wa ukimwi.
Alisema mpaka kukamilika kwa filamu hiyo jumla ya sh.milioni
35 zimetumika katika kukamilisha.
Kalugira alisema kuwa mpaka wiki ijayo watakuwa wamejua ni
wapi watafanya uzinduzi huo.
"Filamu yetu inaitwa Shujaa ambayo tutazindua Desemba Mosi
(2012), lakini bado hatujajua ni wapi tutafanyia uzinduzi huo ambao unaujumbe
mkubwa kwa jamii kuhusiana na janga zima la Ukimwi"alisema Kalugira.
POULSEN AAMBIWA AMECHEMKA KUTOMUITA BARTHEZ STARS
Barthez |
KOCHA wa makipa wa Yanga, Mfaume Athumani Samatta
ameshangazwa na kitendo cha kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars,
Mdenmark Kim Poulsen kuwaita kwenye kikosi cha Bara makipa Juma Kaseja wa Simba
na Deo Munishi ‘Dida’ ambao wote hawako vizuri kwa sasa, huku akimuacha Ally
Mustafa ‘Barthez’ ambaye yuko vizuri.
Akizungumza jana, Samatta alisema
Dida alidaka mechi mbili tu mwanzoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, lakini baada ya hapo amekuwa akisugua benchi na Mwadini Ally
ndiye amekuwa akidaka mechi zote za Azam.
Kuhusu Kaseja, Mfaume alisema kipa huyo kwa sasa hayuko
vizuri na amekuwa akiruhusu mabao rahisi sana, tofauti na Barthez ambaye yuko
vema mno.
“Barthez huku anapokezana na Yaw Berko kudaka, lakini amedaka
mechi zetu tatu mfululizo zilizopita na hajaruhusu bao hata moja, amedaka na
Polisi tumeshinda 3-0, amedaka na JKT Oljoro tumeshinda 1-0 na amedaka na Azam
tumeshinda 2-0 na anafanya kazi ambayo wananchi wanaiona na wanakubali,”.
“Kwa kweli mimi maoni yangu katika nafasi ya kipa, kocha
kachemka sana, tena sana. Ameita hao watu kwa sababu ya mazoea tu, hajazingatia
viwango vyao vya sasa, kwangu mimi ilipofikia Barthez ndiye Tanzania One na
hakuna ubishi,”alisema Mfaume.
Mfaume Athumani |
Jana Paulsen amemuorodhesha Kaseja katika kikosi cha wachezaji
22 watakaounda kikosi cha Bara, Kilimanjaro Stars kitakachomenyana na Kenya,
Harambee Stars katika mchezo wa kirafiki ulio katika kalenda ya FIFA
(Shirikisho la Soka la Kimataifa) Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wiki ijayo.
Mbali na Kaseja wa Simba, Kim aliyepandishwa kutoka timu ya
vijana mwaka huu akirithi mikoba ya Mdenmark mwenzake, Jan Borge Poulsen
amemuita pia kipa Deogratius Mushi wa Azam FC.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Mwanza jana, Paulsen
aliwataja wachezaji wengine ni mabeki Kevin Yondan wa Yanga, Aggrey Morris,
Erasto Nyoni wa Azam FC, Issa Rashid, Nassoro Masoud ‘Cholo’, Shomari Kapombe
na Amir Maftah wa Simba, wakati viungo ni Salum Abubakar ‘Sure Boy’ wa Azam FC,
Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Ramadhan Singano ‘Messi’ na Mrisho Ngassa wa
Simba, Athuman Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo wa Yanga na Shaaban Nditi wa Mtibwa
Sugar.
Washambuliaji walioitwa na Paulsen ni John Bocco ‘Adebayor’ wa
Azam FC, Simon Msuva wa Yanga, Christopher Edward wa Simba, Mbwana Samatta na
Thomas Ulimwengu wa Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC).
Hata hivyo, Poulsen hakuchukua wachezaji wengi wa Zanzibar kwa
sababu nao watakwenda kujiunga na timu ya Zanzibar, inayojiandaa na michuano ya
Kombe la CECAFA Tusker Challenge mwishoni mwa mwezi huu mjini Kampala, Uganda. Alisema
hicho ndio kikosi anachotarajia kukutumia katika Challenge. Kambi ya timu hiyo
itakuwa mjini Mwanza, kwa kuwa ni jirani na Uganda.
KIKOSI KILI STARS;
Makipa; Juma Kaseja
(Simba SC) na Deogratius Mushi ‘Dida’
Mabeki; Kevin Yondan (Yanga), Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam
FC), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Nassoro Masoud ‘Cholo’, Shomari Kapombe na
Amir Maftah (Simba).
Viungo; Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Amri Kiemba,
Mwinyi Kazimoto, Ramadhan Singano ‘Messi’ na Mrisho Ngassa (Simba), Athuman
Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo (Yanga) na Shaaban Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji; John Bocco ‘Adebayor’ (Azam FC), Simon Msuva (Yanga),
Christopher Edward (Simba), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa (TPM, DRC).HODGSON ATEUA Timu England kwa Kirafiki na Sweden!!
>>WAMO Wilshere, Sterling, Shelvey & Osman!!
>>GERRARD kufikisha MECHI 100, ni mmoja Wachezaji 6 tu!!!
Akitangaza
Kikosi cha cha Timu ya Taifa ya England ambacho Jumatano ijayo
kitacheza na Sweden, Kocha wa England Roy Hodgson amemchukua tena Kiungo
wa Arsenal Jack Wilshere kwenye Kikosi hicho kwa mara
ya kwanza baada ya kuwa nje nacho kwa zaidi ya Mwaka mmoja kufuatia
kufuatia kuumia kwake.
Pia yumo Beki wa Arsenal Carl Jenkinson
ambae aliwahi kuzichezea Timu za Taifa za Vijana za Finland na sasa
anasubiri Kibali cha FIFA aruhusiwe kuichezea England.
Wengine walioitwa kwa mara ya kwanza ni
Kiungo wa Evertno, Leon Osman, Miaka 31, na pia wamo Chipukizi Wachezaji
wa Liverpool Raheem Sterling, 17, na Jonjo Shelvey, 20.
Steven Gerrard, Nahodha wa Liverpool na
England, yupo kundini na akicheza hiyo Mechi ya Jumatano na Sweden basi
atafikisha Mechi 100 na kujumuika na Wachezaji 6 wengine waliowahi
kuichezea England mara 100.
+++++++++++++++++++
MARA 100 ENGLAND:
-Peter Shilton - 125
-David Beckham - 115
-Bobby Moore - 108
-Bobby Charlton - 106
-Billy Wright - 105
+++++++++++++++++++
Uteuzi wa Hodgson una mabadiliko ya
Wachezaji 10 na kile kilichocheza Mechi za Mchujo za Kombe la Dunia
dhidi ya Ukraine na Poland Mwezi uliopita.
Walioachwa ni Ashley Cole, ambae
ameichezea England mara 99, kwa vile ni majeruhi pamoja na Joleon
Lescott, Adam Johnson, James Milner, Andy Carroll, Kieran Gibbs, Michael
Carrick, Frank Lampard, Alex Oxlade-Chamberlain na Jermain Defoe.
Winga wa Manchester United Ashley Young
nae amerudishwa Kikosini baada ya kuzikosa Mechi za Mwezi uliopita
alipokuwa kaumia goti lililomweka nje kwa Wiki mbili.
Kikosi hicho cha Ebgland kitapiga Kambi Jijini Manchester kuanzia Jumapili na kisha kusafiri kwenda huko Sweden.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Fraser Forster (Celtic), Joe Hart (Manchester City), John Ruddy (Norwich City).
MABEKI: Leighton Baines
(Everton), Ryan Bertrand (Chelsea), Gary Cahill (Chelsea), Steven
Caulker (Tottenham), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Liverpool),
Ryan Shawcross (Stoke City), Kyle Walker (Tottenham).
VIUNGO: Tom Cleverley
(Manchester United), Steven Gerrard (Liverpool), Aaron Lennon
(Tottenham), Leon Osman (Everton), Jonjo Shelvey (Liverpool), Raheem
Sterling (Liverpool), Theo Walcott (Arsenal), Jack Wilshere (Arsenal),
Ashley Young (Manchester United).
MAFOWADI: Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Chelsea), Daniel Welbeck (Manchester United).
Celtic wailaza CHALI BARCA, Man United wasonga, Chelsea wasogea, Bayern waua!
>>MAN UNITED wafuzu, NI TIMU PEKEE YENYE USHINDI MECHI 4!!
Manchester
United, ilitoka nyuma kwa Bao 1-0, ikastahamili umeme kukatika, na
kuibuka washindi wa Bao 3-1 walipocheza huko Ureno na Braga na kuwachapa
Bao 3-1 na kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 kwa kishindo wakiwa Timu
pekee kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI iliyoshinda Mechi zake zote 4.
Huko Celtic Park, Glasgow, Celtic leo walitoa kishindo kikubwa kwa kuichapa Barcelona Bao 2-1.
Nako Stamford Bridge, Chelsea iliichapa Shakhtar Donetsk Bao 3-2 na kuweka hai matumaini yao kusonga mbele.
+++++++++++++++++++++++++++++++
MATOKEO:
Jumatano Novemba 7
Juventus 4 FC Nordsjælland 0
Chelsea FC 3 FC Shakhtar Donetsk 2
Valencia CF 4 FC BATE Borisov 2
FC Bayern München 6 LOSC Lille 1
SL Benfica 2 FC Spartak Moskva 0
Celtic 2 Barcelona 1
CFR 1907 Cluj 1 Galatasaray 3
SC Braga 1 Manchester United 3
+++++++++++++++++++++++++++++++
KUNDI H
BRAGA 1 MAN UNITED 3
===============
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
Manchester United Pointi 12
CFR Cluj 4
Galatasaray 4
Braga 3
===============
MAGOLI:
Braga: Alan, 49, Penati
Man United: Robin van Persie, 80, Rooney, 84, [Penati], Chicharito, 90
VIKOSI:
Braga: Beto; Leandro Salino, Nuno André Coelho, Douglão, Elderson; Alan, Custodio, Hugo Viana, Rúben Amorim; Rúben Micael; Eder
Akiba: Quim, Mossoró, Hélder Barbosa, Baiano, Ismaily, Djamal, Zé Luis.
Man United: De Gea; Valencia, Smalling, Evans, Evra; Anderson; Nani, Giggs; Rooney; Hernández, Welbeck
Akiba: Lindegaard, Rafael, Ferdinand, Carrick, Young, Van Persie, Cleverley.
Refa: Felix Brych (Germany).
KUNDI G
CELTIC 2 BARCELONA 1
===============
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
Barcelona Pointi 9
Celtic 7
Spartak Moscow 4
Benfica 3
===============
MAGOLI:
Celtic: Victor Wanyama, 21, Watt, 83
Barcelona: Messi, 90
VIKOSI:
Celtic: Forster; Matthews, Ambrose, Wilson, Mulgrew, Lustig,
Commons, Ledley, Wanyama, Miku, Samaras.
Barcelona: Victor Valdes, Danil Alves, Mascherano, Bartra, Jordi Alba, Xavi, Iniesta, Song, Alexis Sanchez, Messi, Pedro
Refa: N Kuipers (Holland)
KUNDI E
CHELSEA 3 SHAKHTAR DONETSK 2
===============
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
Shakhtar Donetsk 7
Chelsea Pointi 7
Juventus 6
Nordsjaelland 1
===============
MAGOLI:
Chelsea: Torres, 6, Oscar, 40, Moses, 90
Shakhtar: Willian, 9 & 47
VIKOSI:
Chelsea:
Petr Cech, Branislav Ivanovic, David Luiz, Gary Cahill, Ryan Bertrand;
Ramires, John Obi Mikel; Juan Mata, Oscar, Eden Hazard; Fernando Torres
Akiba: Turnbull, Romeu, Moses, Marin, Sturridge, Terry, Azpilicueta.
Shakhtar Donetsk:
Andriy Pyatov; Darijo Srna, Olexandr Kucher, Yaroslav Rakytskiy, Razvan
Rat; Fernandinho, Tomas Hubschman; Henrik Mkhitaryan, Willian, Alex
Teixeira, Luiz Adriano
Akiba: Kanibolotskiy, Stepanenko, Eduardo, Shevchuk, Douglas Costa, Chygrynskiy, Ilsinho.
Refa: Carlos Velasco Carballo (Spain)
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumanne Novemba 20
FC Nordsjælland v FC Shakhtar Donetsk
Juventus v Chelsea FC
FC BATE Borisov v LOSC Lille
Valencia CF v FC Bayern München
FC Spartak Moskva v FC Barcelona
SL Benfica v Celtic FC
Galatasaray A.S. v Manchester United FC
CFR 1907 Cluj v SC Braga
Jumatano Novemba 21
FC Porto v GNK Dinamo
FC Dynamo Kyiv v Paris SaintvGermain FC
Arsenal FC v Montpellier Hérault SC
FC Schalke 04 v Olympiacos FC
FC Zenit St. Petersburg v Málaga CF
RSC Anderlecht v AC Milan
AFC Ajax v Borussia Dortmund
Manchester City FC v Real Madrid CF
Jumanne Desemba 4
GNK Dinamo v FC Dynamo Kyiv
Paris SaintvGermain FC v FC Porto
Montpellier Hérault SC v FC Schalke 04
Olympiacos FC v Arsenal FC
Málaga CF v RSC Anderlecht
AC Milan v FC Zenit St. Petersburg
Borussia Dortmund v Manchester City FC
Real Madrid CF v AFC Ajax
Jumatano Desemba 5
FC Shakhtar Donetsk v Juventus
Chelsea FC v FC Nordsjælland
LOSC Lille v Valencia CF
FC Bayern München v FC BATE Borisov
FC Barcelona v SL Benfica
Celtic FC v FC Spartak Moskva
Manchester United FC v CFR 1907 Cluj
SC Braga v Galatasaray A.S.
No comments:
Post a Comment