Monday, January 14, 2013

SELEMBE AISUBILIA KWA HAMU JKT MGAMBO



Selembe aisubiri kwa hamu JKT Mgambo
Kiungo mshambulia wa pembeni wa timu ya Taifa ya Zanzibar na klabu ya soka ya Coastal Union ya Tanga, Suleiman Kassim amesema kuwa, klabu yake itaifunga kwa mara nyingine timu ya JKT Mgambo inayotokea, wilaya ya Muheza, mkoani humo katika mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom, Tanzania Bara.
” Tuliwafunga, Mgambo kwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza, hatutaishia hapo bali tutawafunga tena katika mchezo wa tarehe 27″ anasema, kiungo huyo wa zamani wa Azam FC, na African Lyon, wakati akiteta na tovuti ya kandanda..
Selembe, ambaye ana uwezo mzuri katika kukimbia na mipira, kutoa pasi za mwisho na kufunga wakati mwingine. Lakini vitu hivyo hufanya sasa akiwa na timu ya Taifa. ” Unajua mimi mara nyingi huwa natengeneza nafasi za kufunga magoli kwa wenzangu, hiyo imekuwa ni kama tabia yangu, lakini ikitokea nafasi ya kufunga basi mara moja nafanya hivyo” anaongeza kiungo huyo ambaye amekuwa akiingia na kutoka katika timu ya Taifa ya Tanzania ( Taifa Stars)

No comments:

Post a Comment