USALAMA NI JAMBO LINALOPEWA KIPAUMBELE - VALCKE.
MAOFISA wa ngazi za juu
wa michezo wamesisitiza kuwa usalama litakuwa jambo linalopewa
kipaumbele nchini Brazil katika michuano ya Kombe ya Dunia na Olimpiki
ikiwa ni tahadhari kufuatia moto uliozuka katika klabu moja ya usiku na
kuua watu wapatao 231. Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Jerome Valcke amesema kuwa
ajali iliyotokea huko Santa Maria mji uliopo kusini mwa nchi hiyo ni
mojawapo ya ajali mbaya zaidi kuwahi kutokea. Hatahivyo
Valcke amesema ajali hiyo ya moto haihusiani na usalama ndani ya viwanj
ambavyo vitatumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho
inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi June 15 hadi 30 mwaka huu pamoja na
ile ya Kombe la Dunia mwakani. Amesema
katika michuano hiyo wameandaa watu na kuwapa mafunzo ya kutosha na
kuwa na uwezo kuwaondoa watu waliojaa uwanjani katika muda wa dakika
nane pindi tukio la hatari linapotokea. Naye
mkurugenzi wa mawasiliano wa kamati ya maandalizi ya michuano ya
Olimpiki 2016, Carlos Vilanova amesema tukio la moto lililotokea
linaweza kutokea mahala popote duniani na wala halihusiani na uwezo wa
Brazil kuandaa mashindano makubwa. Vilanova
amesema nchi hiyo imekuwa ikiandaa matamasha makubwa kwa miaka mingi
kama Rio Carnaval na mafataki yanayorushwa katika kipindi cha mwaka mpya
kwenye ufukwe wa Copacabana ambao hukusanya watu zaidi ya milioni mbili
lakini hakujawahi kutokea tukio lolote baya.
No comments:
Post a Comment