MESSI KUSAINI MKATABA BARCELONA.
RAIS wa klabu ya
Barcelona, Sandro Rosell amesema kuwa mshambuliaji nyota wa klabu hiyo
Lionel Messi anatarajiwa kuongeza mkataba wiki ijayo. Mkataba
huo mpya ambao Messi anatarajiwa kusaini utamuweka katika klabu hiyo
mpaka 2018 lakini Rosell alibainisha kuwa hakuna klabu yoyote iliyokuja
kutaka kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Argentina. Rosell
amesema klabu haijapokea maombi yoyote ya mchezaji huyo kutoka vilabu
vingine na ana uhakika kama wapo waliomfuata lazima atakuwa
amewakatalia. Messi
mwenye umri wa miaka 25 anakuwa mchezaji wa tatu ndani ya wiki moja
kukubali kusaini mkataba mpya kufuatia habari kuwa Carles Puyol na Xavi
Hernandez nao kukubali kuongeza mikataba yao na Rosell ana uhakika
golikipa Voctor Valdes naye atafuata nyayo hizo.
No comments:
Post a Comment