Tuesday, January 29, 2013

SCHOLES ALIZWA GARI, QPR YAMTAKA SAMBA, BECKHAM YUPO ARSENAL!


GIGGS_n_SCHOLESLEO asubuhi huko Jijini Manchester, Staa  wa Manchester United, Paul Scholes, aliibiwa Gari lake la thamani nje ya Nyumba yake na toka Jijini London zipo taarifa QPR wametoa ofa kumnunua Chris Samba toka Anzhi Makhachkala wakati Arsene Wenger alithibitisha David Beckham yuko pamoja na Kikosi cha Arsenal.
Scholes
Paul Scholes aliliacha Gari lake Chevrolet Captiva lenye thamani ya Pauni 30,000 nje ya nyumba yake baada ya kuwasha Injini na yeye kurudi ndani lakini Dakika chache baadae aliporudi nje Gari likawa limeyeyuka.
Polisi wa Jiji la Manchester wamethibitisha wizi huo uliotokea kati ya Saa 1 Dakika 45 na Saa 2 Asubuhi leo Asubuhi.
Klabu ya Man United inadhaminiwa na Kampuni ya Magari ya Chevrolet na Wachezaji wa Klabu hiyo huchagua Gari wanalotaka toka Kampuni hiyo.
Scholes, mwenye Miaka 38 na ambae ameichezea Man United maishani mwake mote akicheza zaidi ya Mechi 700, anaishi Nyumbani kwake pamoja na Mkewe na Watoto wao watatu.
QPR
Queens Park Rangers imetoa Ofa ya Pauni Milioni 10 kumnunua Sentahafu wa Anzhi Makhachkala ya Urusi huku wakiwa wana imani Beki huyo aliewahi kuichezea Blackburn Rovers anaweza kuwasaidia wasishuke Daraja kutoka Ligi Kuu England ambako sasa ndio Timu ya mkiani kwenye Msimamo wa Ligi.
Wakati Samba yupo Urusi Familia yako muda wote imebakia London na inaaminika mwenyewe anapenda arudi England.
Beckham
Kiungo na Nahodha wa zamani wa England David Beckham amekuwa akifanya mazoezi na Timu ya Arsenal kama ilivyothibitishwa na Meneja wa Timu hiyo Arsene Wenger ambae, hata hivyo, amekanusha habari za kutaka kumsaini Mkongwe huyo.
Wenger amesema Beckham aliwasiliana nae akiomba kujiweka fiti na akamkubalia.
Hivi sasa Beckham hana Klabu yeyote baada ya kung’atuka kuichezea Los Angeles Galaxy inayocheza Ligi ya MLS huko USA mwishoni mwa Mwaka jana.
Beckham alijitengenezea jina lake alipokuwa na Manchester United na baadae kuichezea Real Madrid na pia AC Milan.
Kwa sasa Beckham ana Umri wa Miaka 37

No comments:

Post a Comment