NITAPIGANIA NAMBA YANGU - CASILLAS.
NAHODHA wa klabu ya Real
Madrid, Iker Casillas amesisitiza kuwa ameongeza muda wa kujifua
mazoezini ili aweze`kupata namba tena katika kikosi cha kwanza cha timu
hiyo. Casillas
mwenye umri wa miaka 31 alienguliwa katika kikosi cha kwanza wakati
Madrid ilipokubali kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Malaga na kocha wake
Jose Mourinho na nafasi yake kuchukuliwa na golikipa namba mbili Antonio
Adan. Hatahivyo
akiongea na waandishi wa habari baada ya mazoezi ya kwanza ya Madrid
baada ya mapumziko ya kipindi cha baridi, golikipa huyo amesema
anajitahidi kufanya kila awezalo ili aweze kupigania namba yake katika
kikosi cha kwanza. Casillas
amesema kocha ndio mwenye maamuzi ya kuamua nani acheze na asicheze
katika mchezo unaofuata na wote wanamuunga mkono Mourinho na wana imani
naye kwa maamuzi atakayochukua. Madrid
kwasasa iko katika nafasi ya tatu katika msimamo wa La Liga kwa tofauti
ya alama 16 na mahasimu wao Barcelona ambao wanaongoza msimamo wa ligi
hiyo.
No comments:
Post a Comment