Wednesday, January 2, 2013

FRANK DOMAYO, MWINYI KAZIMOTO WACHONGANISHWA TUZO YA KIUNGO BORA TANZANIA



KAMATI ya maandalizi ya Fainali ya tuzo za Mwanasoka Bora wa mwaka (Wazalendo Footballer of the Year), imekamilisha mchakato wa kupitisha majina ya wanasoka walioingia katika fainali ya tuzo hizo mwaka 2012.
Taarifa ya Mratibu, Ahadi Kakore imesema katika mchakato huo kamati iliweza kuangalia  vigezo vikuu vinne ambavyo ndivyo vitaendelea kuwa dira na mwongozo hadi siku ya fainali Januari 31 mwaka 2013.
“Awe ni mchezaji wa timu ya taifa,  mchango wake katika klabu yake na timu ya taifa, nidhamu kwa ujumla ndani na nje ya uwanja na asiwe na kashfa ya utumiaji wa dawa zilizopigwa marufuku michezoni ikiwemo dawa za kulevya,”imesema taarifa hiyo.
Taarifa ya Kakore imesema wapo wachezaji ambao hawajaweza kuwa na vigezo vyote lakini akawa navyo viwili kati ya hivyo aliweza kupita. Kwa mfano wapo wachezaji ambao uwezo wao ni wa hali ya juu ambapo wanastahili kucheza timu ya taifa lakini wameshindwa kupata nafasi kutokana na sababu mbalimbali lakini uwezo wake hauna shaka hivyo ni ngumu kumtoa kwenye kinyang’anyiro hiki.
Tuzo hizo zimegawanyika katika makundi tofauti tofauti ambapo jumla ya tuzo zote ni 12 kutokana na ukweli kwamba katika tuzo za maendeleo ya soka la wanawake zipo tuzo mbili ya wanaume na wanawake.
Mgawanyo wa tuzo hizo ni kama ifuatavyo; Kipa Bora, Beki Bora, Kiungo Bora, Mshambuliaji Bora, Mchezaji anayechipukia, Mchezaji Bora wa Kike, Mchezaji Bora Kigeni, Mchezaji bora wa zamani, Maendeleo soka la Wanawake, Mwanasiasa wa Afrika aliyesadia maendeleo ya michezo pamoja na tuzo kubwa ya Mwanasoka Bora wa mwaka 2012. Fainali ya hizo zitafanyika Januari 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
WALIOPITISHWA KUWANIA TUZO:
Kundi A: Kipa Bora
Mwandini Ally- Azam FC, Juma Kaseja- Simba, Shaaban Kado- Mtibwa Sugar, Ally Mustapha-Yanga, Jackson Chove-Coastal Union, Deogratius Munishi- Azam FC
Kundi B: Beki Bora
Nassor Said – Simba, Nadir Haroub – Yanga, Agrey Morris- Azam FC, Amir Maftah- Simba, Kelvin Yondan-Yanga  na Shomari Kapombe-Simba.
Kundi C: Kiungo Bora
Shaban Nditi –Mtibwa, Frank Domayo- Yanga, Mwinyi Kazimoto-Simba, Amri Kiemba-Simba, Chande Mgoja- Mgambo JKT na Abubakar Salum-Azam FC.
Kundi D: Mshambuliaji Bora
John Bocco - Azam FC, Mrisho Ngassa – Simba, Hussein Javu -Mtibwa FC, Amiry Omary-JKT Oljoro, Simon Msuva-Yanga, Nsa Job-Coastal Union.
Kundi E: Mchezaji anayechipukia
Mudasir Yahya-Azam FC, Ramadhan Singano-Simba, Edward Christopher-Simba, Manyika Peter Manyika- Mgambo JKT, Miraji Adam-Simba na Chande Mgoja- Mgambo JKT
Kundi F: Mchezaji Bora wa Kike
Ester Chabruma-Sayari Queens, Mwanahamisi Omar-Mburahati Queens, Mwapewa Mtumwa-Ever Green, Fatuma Mustafa-Sayari Queens, Asha Rashid-Mburahati Queens na Sophia Mwasikili-Luleburgaz Spor Kulubu- Uturuki.
Kundi H: Mchezaji Bora wa mwaka 2012
Mchezaji atakayetwaa tuzo hii atatoka katika makundi yaliyotajwa hapo juu hii ikiwa na maana kwamba kuanzia kundi A-E. hii ni kumaanisha kuwa wanawake hawataingia kwenye kundi hili wala kwa sababu tayari wanayio tuzo yao tayari kama inavyoonekana katika kipengele F.
Kundi I: Mchezaji Bora Kigeni
Haruna Niyonzima-Yanga, Kipre Tchetche-Azam FC, Emmanuel Okwi-Simba,  Felix Sunzu-Simba, Hamis Kiiza-Yanga na Jerry Santo-Coastal Union.
TUZO ZA HESHIMA
Kundi H: Mchezaji bora wa zamani
Madaraka Suleiman – Simba, Edibily Lunyamila-Yanga/Simba/Twiga FC,
Mohamed Mwameja-Simba, Yusuf Macho-Simba/Kagera Sugar, Zamoyoni Mogela-Simba/Yanga na Kenny Mkapa-Yanga.
Kundi I: Maendeleo soka la Wanawake (tuzo mbili Mwanamke na Mwanaume)
Stephania Kubumba-Sayari, Arafa Tamba-Mburahati Queens, Fatma Makambara-Sayari, Pili Kambangwa- Mchangani, Joha Halfan-Vijana Queens, Amin Bakhresa, Frenk Mchaki na  Idd Azan.
Kundi J:Mwanasiasa wa Afrika aliyesadia maendeleo ya michezo
Benjamin Mkapa-Tanzania, Daniel Arap Moi-Kenya na Joachim Chisano-Msumbiji
Katika kipengere hiki ni kwamba kilichoangaliwa ni namna gani mwanasiasa mstaafu alivyweza kusaidia michezo kwa ujumla ikiwemo soka. Hapa inaangaliwa ujewekaji wa miundo mbinu, kama ujezi wa viwanja vya michezo, mafanikio katika klabu na  timu za taifa katika nchi ambayo amekuwa akiiongoza.
Pia kipengere hiki pia kinaangalia katika kipindi kisichozidi miaka 10 ya utawala akiwa kama mkuu wa nchi husika.
Baada ya kufuatilia kwa takriban mwaka mmoja katika nchi zilizopo jirani na Tanzania, imeonekana wazi kuwa viongozi hao wastaafu ndiyo wenye waliofikia viwango ambavyo kamati ilivihitaji.

No comments:

Post a Comment