Friday, January 18, 2013

NGULI WA SOKA WA ZAMANI WA UJERUMANI MUELLER AJIVUNIA KUWA NA JEZI YA MESSI.


NGULI wa soka wa Ujerumani, Gerd Mueller amesema anajivunia kuwa na jezi ya mchezaji bora duniani baada ya kupokea fulana hiyo kutoka kwa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi. Mueller alitoa kauli hiyo jana wakati akimkabidhi fulana hiyo bosi wa klabu ya Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge ili iweze kuwekwa katika jumba la makumbusho la klabu hiyo ya Ujerumani. Messi ambaye amenyakuwa tzuo ya mchezaji bora wa dunia mara nne mfululizoalimtumia Muelller jezi hiyo baada ya kuvunja rekodi yake ya kufunga mabao mengi zaidi kwa msimu mmoja mwaka uliopita. Nyota huyo alifunga jumla ya mabao 91 mwaka jana kwa klabu yake na timu ya taifa na kuvunja rekodi ya Mueller ya kufunga mabao 85 aliyoweka mwaka 1972 kwa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani.

No comments:

Post a Comment