Friday, January 18, 2013

ULAYA: BUNDESLIGA YAREJEA, LA LIGA & SERIE A ZAENDELEA!!


>>NAPOLI YARUDISHIWA POINTI 2 ILIZONYANG’ANYWA!!
BORUSSIA_DORTMUND_JUKWAABUNDESLIGA, Ligi ya huko Ujerumani, leo inaanza tena baada ya kuwa Vakesheni ya Krismasi na Mwaka mpya na huko Spain na Italy, zile Ligi maarufu za La Liga na Serie A kwa Mechi Wikiendi hii.
ZIFUATAZO ni RATIBA na TAARIFA ya LIGI HIZO:
Barca wawania kuyoyoma!
Wakiwa kileleni, Pointi 11 mbele ya Timu ya Pili Atletico Madrid na 18 mbele ya Timu ya 3 Real Madrid ambao pia ndio Mabingwa watetezi, Barcelona watakuwa ugenini kucheza na Real Sociedad.
Atletico Madrid watakuwa nyumbani kucheza na Levante na Real Madrid wapo ugenini kucheza na Valencia, Timu ambayo waliifunga 2-0 hivi Juzi huko Santiago Bernabeu katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya COPA del REY.
RATIBA:
Ijumaa Januari 11
Espanyol v Mallorca
Jumamosi Januari 19
Granada v Rayo Vallecano
Real Sociedad v Barcelona
Getafe v Sevilla
Malaga v Celta Vigo
Jumapili Januari 20
Osasuna v Deportivo la Coruna
Valladolid v Zaragoza
Atletico Madrid v Levante
Valencia v Real Madrid
Jumatatu Januari 21
Real Betis v Athletic Bilbao
SERIE A
Uongozi wa Juve hatarini toka kwa Napoli, Lazio
Uongozi wa Juventus wa Ligi Serie A upo hatarini toka kwa Napoli na Lazio ambazo ziko Pointi 3 tu nyuma ya Juve ambao watakuwa nyumbani kucheza na Timu ngumu Udinese na huenda wakaingia kwenye Mechi hiyo bila ya Viungo wao muhimu, Andrea Pirlo na Arturo Vidal ambao wana maumivu.
Lazio watakuwa ugenini kucheza na Palermo na Napoli, ambao wamerudishiwa Pointi zao 2 na FIGC, Shirikisho la Soka Italy, baada ya kushinda Rufaa yao dhidi ya Upangaji Matokeo Mechi, pia wapo ugenini kucheza na Fiorentina.
RATIBA:
Jumamosi Januari 19
Palermo v Lazio
Juventus v Udinese
Jumapili Januari 20
Fiorentina v Napoli
Atalanta v Cagliari
Chievo v Parma
Genoa v Catania
Milan v Bologna
Pescara v Torino
Siena v Sampdoria
Roma v Inter
BUNDESLIGA
Baada ya kuwa Vakesheni tangu kabla ya Krismasi, BUNDESLIGA leo inarejea kilingeni kwa Mechi moja kati ya Schalke na Hannover na Jumamosi, Vinara wa Ligi, Bayern Munich watakuwa kucheza na Greuther Fürth.
Bayern Leverkusen, ambao wapo nafasi ya Pili Pointi 9 nyuma ya Bayern Munich, watakuwa nyumbani kucheza na Eintracht Frankfurt.
Mabingwa watetezi Borussia Dortmund, ambao wako nafasi ya 3 Pointi 3 nyuma ya Bayer Leverkusen, watakuwa ugenini kucheza na Werder Bremen.
RATIBA
Ijumaa Januari 18
Schalke - Hannover [22:30]
Jumamosi Januari 19
Bayern Munich- Greuther Fürth [17:30]
Hoffenheim - Monchengladbach [17:30]
Leverkusen – Eintracht Frankfurt  [17:30]
Mainz - Freiburg [17:30]
Wolfsburg - Stuttgart [17:30]
Werder Bremen - Dortmund [20:30]
Jumapaili Januari 20 Bottom of Form

Nurnberg - Hamburg [17:30]
Fortuna Dusseldorf - Augsburg [19:30]
MSIMAMO-Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 17]
1.  Bayern  Pointi 42
2.  Leverkusen  33
3.  Dortmund  30
4.  Eintracht  30
5.  Freiburg  26
6.  Mainz  26
7.  Schalke  25
8.  Monchengladbach
9.  Stuttgart  25
10.  Hamburg  24

No comments:

Post a Comment