Kim Poulsen |
KOCHA Mkuu
wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameondoka leo mchana (Januari 18 mwaka huu) kwa
ndege ya South African Airways kwenda Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Ivory
Coast na Morocco zinazoshiriki Fainali za 29 za Mataifa ya Afrika (AFCON)
zinazoanza kesho (Januari 19 mwaka huu) nchini humo.
Ivory Coast
na Morocco ziko kundi moja na Tanzania (Taifa Stars) katika kinyang’anyiro cha
kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani
nchini Brazil.
Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na inayoshika nafasi ya pili
katika kundi hilo ambalo pia lina timu ya Gambia itacheza na Morocco, Machi 24
mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment