Friday, January 18, 2013

JAMAA WA KAGERA AJITOKEZA KUPAMBANA NA MANJI BODI YA LIGI KUU NANI KUIBUKA KIDEDEA????


Manji anayegombea Uenyekiti wa Bodi, akiwa na Rahim 'Zamunda'

WAOMBAJI watatu wapya wamejitosa katika kinyang’anyiro cha kuwania uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ambayo uchaguzi wake utafanyika Februari 22 mwaka huu.
Walioingia leo (Januari 18 mwaka huu) kwenye kinyang’anyiro hicho ni Hamad Yahya wa Kagera Sugar anayeomba uenyekiti wakati Christopher Peter wa Moro United na Kazimoto Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza wanaoomba ujumbe wa Bodi kuwakilisha klabu za Ligi Daraja la Kwanza.
Orodha kamili ya waombaji uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu ni Hamad Yahya wa Kagera Sugar na Yusuf Manji wa Yanga wanaoomba uenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti aliyeomba ni Said Mohamed wa Azam.
Kwa upande wa wajumbe wawili kuwakilisha klabu za Daraja la Kwanza ni  Christopher Peter Lunkombe wa Moro United ya Dar es Salaam na Kazimoto Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza.

No comments:

Post a Comment