Monday, January 7, 2013

MESSI, RONALDO, INIESTA NANI ATASHINDA BALLON D'OR LEO?


MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, mshambuliaji nyota
Nani atatwaa tuzo ya FIFA Ballon d'Or leo?
Barcelona Lionel Messi na Andres Iniesta ni miongoni mwa majina ya wachezaji watatu ambao wanagombea tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2012 maarufu kama Ballon d’Or. Majina hayo matatu ya wachezaji hao yalichujwa kutoka majina 23 yaliyoteuliwa na kamati ya Shirikisho la Soka Duniani ambapo yalipigiwa kura na makocha na manahodha wa timu za taifa ambao ni wajumbe wa FIFA. Baada ya mchujo huo ndio yakachomoza majina ya nyota hao watatu ambao leo usiku katika sherehe zitakazofanyika jijini Zurich, Switzerland mmoja wapo atanyakuwa tuzo hiyo huku jina Messi likipewa kipaumbele ili kuibuka na kidedea. Kama Messi ambaye ni raia wa Argentina akiibuka kidedea atakuwa ameweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kunyakuwa tuzo hiyo mara nne mfululizo. Nyota wengine waliowahi kunyakuwa tuzo hiyo mara nyingi ni pamoja na Ronaldo de Lima na Zinedine Zidane ambao wote kwa pamoja wamenyakuwa tuzo hiyo mara tatu kila mmoja lakini katika vipindi tofauti.

No comments:

Post a Comment