KINNAH PHIRI ATIMULIWA TIMU YA TAIFA YA MALAWI THE FLAMES.
SHIRIKISHO la Soka
nchini Malawi-FAM limemtimua kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Kinnah
Phiri kufuatia kipigo cha mabao 3-1 ilichokipata timu hiyo kutoka kwa
Afrika Kusini mwezi uliopita. FAM
ilitangaza kumtimua kocha huyo na msaidizi wake Young Chimodzi pamoja
na Mkurugenzi wa Ufundi Jack Chamangwana baada ya kutumikia miezi sita
katika mkataba wa miaka miwili walioongezewa. Katika
taarifa yake FAM imesema ilifikia uamuzi huo kufuatia mwenendo mbovu wa
timu ya taifa katika kikao cha dharura cha kamati ya utendaji
walichokaa Januari 12 mwaka huu. Kinnah
alikiongoza kikosi cha nchi hiyo kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika
mwaka 2010 kwa mara ya kwanza baada ya miaka 26 kupita lakini timu hiyo
imekuwa ikiporomoka kiwango toka kipindi hicho.
No comments:
Post a Comment