Tuesday, January 29, 2013

EL CLASICO: JUMATANO REAL KUTINGA BILA NYOTA KIBAO!!


>>COPA del REY-NUSU FAINALI: REAL MADRID v BARCELONA!!
>> CASILLAS, PEPE, COENTRAO, DI MARIA & RAMOS NJE!!
REAL MADRID wataingia Uwanjani kwao Santiago Bernabeu Jumatano Usiku kucheza Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe la Mfalme, COPA del REY, dhidi ya Mahasimu wao wakubwa FC Barcelona na bila ya Nyota wao kibao.

COPA del REY
NUSU FAINALI
Jumatano Januari 30
[SAA 5 Usiku]
Real Madrid v Barcelona
Alhamisi Januari 31
[SAA 6 Usiku]
Atletico Madrid v Sevilla
MARUDIANO
Jumatano Februari 27
Sevilla v Atletico Madrid
Barcelona v Real Madrid
++++++++++++++++++++++++++++++++
MESSI_n_RONALDOWakiwa tayari washasalimu amri kuutetea Ubingwa wao wa La Liga kwani wako nyuma ya Vinara Barcelona kwa Pointi 15, Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho, alishatangaza mkazo wao ni kwenye COPA del REY na UEFA CHAMPIONZ LIGI lakini sasa wataingia ndani ya Kombe hilo la Mfalme bila ya Kipa na Nahodha wao Iker Casillas ambae atakuwa nje kwa Miezi mitatu baada ya kuvunjika mfupa wa mkononi.
Pia hawana Beki Pepe ambae bado anauguza enka huku Mabeki Sergio Ramos na Fabio Coentrao pamoja na Winga Angel Di Maria wataikosa Mechi na Barca kwa vile wapo Kifungoni.
Hata hivyo Staa wao mkubwa na mashine yao ya Magoli, Cristiano Ronaldo, ametamka: “Ni Mechi muhimu na ngumu. Tunacheza nyumbani na ni nafasi nzuri kwetu. Tunawakosa Wachezaji muhimu kadhaa lakini hilo si kisingizio. Inabidi tucheze vizuri kwani Barca ni Timu ya kushangaza!”
Lakini hali ndani ya Kambi ya Real pia si shwari kwani kuna tetesi kuna msuguano huku ikidaiwa Casillas na Ramos wametishia kuondoka ikiwa Mourinho hatatimuliwa lakini hayo yamekanushwa vikali na Rais Wa Real Florentino Perez.
Mara baada ya kupata pigo la kumkosa Kipa Casilla kwa muda mrefu, Real haraka haraka ikamsaini Kipa kutoka Sevilla, Diego Lopez, ingawa inaaminika Kipa Nambari mbili, Antonio Adan, ndie atakuwa akipata namba.
++++++++++++++++++++++++++++++
USO kwa USO:
MECHI RASMI:
Real Madrid wameshinda 88
Sare 47
Barcelona wameshinda 86
MAGOLI:
Real Madrid 372
Barcelona 358
++++++++++++++++++++++++++++++
Hivi karibuni, Real ndio wamekuwa wakiwa na rekodi nzuri kupita Barca walipowashinda mwanzoni mwa Msimu huu kwenye Spanish Super Cup kwa Magoli ya ugenini baada ya kutoka sare ya 4-4 na pia kwenye Mechi ya kwanza ya La Liga Msimu huu waliocheza huko Nou Camp walitoka 2-2.
Na Ronaldo nae ana rekodi nzuri kwenye El Clasico kwa kufunga Bao 7 katika Mechi 6 za Mahasimu hao.
Mbali ya Mechi hii kuwakutanisha Mahasimu Real na Barca pia inawakutanisha Wachezaji Bora Duniani, Ronaldo wa Real na Messi wa Barca, ambao vitu vyao Uwanjani Siku zote huleta ushindani mkubwa kwao na Mashabiki wao.
Kwenye La Liga, Jumapili Ronaldo aliipigia Real Hetitriki walipoikung’uta Getafe 4-0 na baadae Siku hiyo Messi akaifungia Barca Bao 4 walipowatandika Osasuna Bao 5-1.
Kwenye La Liga, Messi ndie anaongoza kwa kufunga Bao 33 na Ronaldo anafuata akiwa na Mabao 21.
Mwaka jana, Barca waliwatoa Real kwa Jumla ya Mabao 4-3 katika Robo Fainali ya COPA del REY na hatimae kulinyakua.
Katika Nusu Fainali nyingine ya COPA del REY, Atletico Madrid watakuwa Uwanja wa Nyumbani Calderon kwa kucheza na Sevilla Alhamisi Usiku huku wakiwa na matumaini ya kumchezesha Straika wao hatari Radamel Falcao ambae amezikosa Mechi kadhaa kwa kuwa majeruhi.

No comments:

Post a Comment