Friday, January 18, 2013

BAADA YA KUTWAA KOMBE LA HISANI KULE KONGO NA KOMBE LA MAPINDUZI WANALAMBA LAMBA AZAM KUJIFUA UWANJA WA NYAYO CITY


Azam FC
TIMU ya Azam FC imewasili salama jijini Nairobi nchini Kenya jana usiku tayari kwa kuanza michezo yake wa kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa ajili ya ligi kuu ya Tanzania mzunguko wa pili pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Akizungumzia program nzima ya maandalizi kocha wa Azam FC, Stewart Hall amesema timu itacheza mechi tatu za kirafiki na kufanya mzoezi ya siku mbili katika viwanja vya Nyayo na City.
Alisema wachezaji wote wamefika salama, timu itaacheza mchezo wake wa kwanza kesho ‘Jumamosi’ saa 3:30 (15:30hrs) dhidi ya A.F.C Leopard, kwenye Uwanja wa Nyayo.
Azam FC leo ‘Ijumaa’ jioni itafanya mazoezi yake ya kwanza katika Uwanja wa Nyayo uliopo katikati ya jijini la Nairobi.
“Tutacheza michezo mitatu, michezo yetu itahusisha timu zenye viwango vizuri katika ligi ya Kenya ambazo ni A.F.C Leopard, Sofapaka na K.C.B, mechi hizo zitasaidia kuimarisha timu yangu” alisema Stewart.
Kocha Stewart alisema watafanya mazoezi na kucheza mechi katika viwanja aina mbili vyenye nyasi za kawaida na zenye nyasi bandia kwa kuwa katika michezo ya ligi viwanja hivyo vinaendana na mazingira ya Tanzania.
Azam FC iliyoko nchini hapa bila ya washambuliaji wake John Bocco na Tchetche Kipre na mchezaji Waziri Salum wanaosumbuliwa na majeruhi, siku ya Jumapili itacheza mechi yake ya pili ya kirafiki dhidi ya SOFAPAKA kwenye uwanja huo huo.
Baada ya mchezo huo kikosi hicho kitapumzika siku ya Jumatatu Jan 21, 2013 ambapo watatumia siku hiyo kufanya mazoezi katika Uwanja wa City wenye nyasi bandia.
Azam FC itamaliza safari yake ya maandalizi na mechi za kirafiki siku ya Jumanne Jan 22 ambapo watacheza dhidi ya K.C.B kwenye Uwanja wa City mchezo ambao utakamilisha safari hiyo ya siku saba.
Wachezaji walioko jijini Nairobi ni Mwadini Ally, Aishi Manula, Jackson Wandwi, Himid Mao, Samih Haji Nuhu, David Mwantika, Luckson Kakolaki, Jockins Atudo, Michael Bolou, Humphrey Mieno, Khamis Mcha, Gaudence Mwaikimba, Uhuru Selemani, Brain Umony, Malika Ndeule, Omary Mtaki, Abdi Kassim ‘Babi’, Abdalah Seif, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo na Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
PROGRAMU YA AZAM NAIROBI:
Januari 17, 2013: Kuwasili
Januari 18, 2013: Mazoezi Uwanja wa Nyayo (Saa 10:00 jioni)
Januari 19, 2013: Azam FC Vs AFC Leopard Uwanja wa Nyayo (Saa 9:30 Alasiri)
Januari 20, 2013: Azam FC Vs Sifapaka Uwanja wa Nyayo (Saa 9:30 Alasiri)
Januari 21, 2013: Mazoezi Uwanja wa City (Saa 10:00 jioni)
Januari 22, 2013:  Azam FC Vs KCB Uwanja wa City (Saa 10:00 jioni)

No comments:

Post a Comment