Thursday, January 31, 2013

AFCON 2013: TOGO YAUNGANA NA IVORY COAST ROBO FAINALI!

>>SAFU ROBO FAINALI YAKAMILIKA, KUANZA JUMAMOSI!!
AFCON_2013-NA_KABUMBU_LIANZESAFU YA ROBO FAINALI ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, leo imekamilika baada ya Togo kuungana na Ivory Coast ambao tayari walikuwa wamefuzu kabla ya Mechi za mwisho za leo za KUNDI D ambazo zote mbili zilimalizika kwa sare.
Ivory Coast ndie Mshindi wa KUNDI D na Togo kutwaa nafasi ya Pili kwa kumzidi Tunisia kwa tofauti ya Magoli baada ya kufungana kwa Pointi.
Kwenye Robo Fainali, ambazo zinaanza Jumamosi Februari 2, Ivory Coast watacheza na Nigeria na Togo kuikwaa Burkina Faso.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
ROBO FAINALI
Jumamosi Februari 2
Ghana v Cape Verde [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Afrika Kusini v Mali [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
Jumapili Februari 3
Ivory Coast v Nigeria [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Burkina Faso v Togo [Mbombela Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
TOGO 1 TUNISIA 1
Togo leo wamefanikiwa kuingia Robo Fainali yao ya kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kutoka sare 1-1 na Tunisia na hivyo kuungana na Vinara Ivory Coast kwenye Robo Fainali.
+++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Togo 1
-Gakpe Dakika ya 13
Tunisia 1
-Mouelhi Dakika ya 30 (Penati)
+++++++++++++++++++++++
Emmanuel Adebayor alimtengezea Floyd Ayite alieipa Togo bao lao katika Dakika ya 13 na Tunisia kusawazisha kwa Penati ya Khaled Mouelhi ambae baadae alikosa Penati nyingine waliyopewa Tunisia.
Togo nao walinyimwa Penati ya wazi baada ya Adebayor kuangushwa.
VIKOSI:
Togo: Atsu, Nibombe, Akakpo, Bossou, Mamah, Salifou, Amewou, Wome, Floyd Ayite, Adebayor, Jonathan Ayite
Akiba: Agassa, Mani, Ouro-Akoriko, Segbefia, Romao, Gakpe, Placca, Ametepe, Donou, Djene, Damessi, Tchagouni.
Tunisia: Ben Cherifia, Hichri, Abdennour, Chammam, Khazri, Mouelhi, Traoui, Hammami, Darragi, M'Sakni, Khelifa
Akiba: Ben Mustapha, Ifa, Baratli, Dhaouadi, Gharbi, Harbaoui, Ben Youssef, Ben Yahia, Dhaouadi, Jemaa, Boussaidi, Mathlouthi.
Refa: Daniel Bennet (South Africa)
ALGERIA 2 IVORY COAST 2
Ivory Coast, ambao ndio Washindi wa KUNDI D, leo wametoka nyuma kwa Bao 2-0 na kutoka sare ya Bao 2-2 na Algeria hivyo kuendeleza rekodi yao ya kutofungwa AFCON 2013.
+++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Algeria 2
-Feghouli Dakika ya 64 (Penati)
-Soudani 70
Ivory Coast 2
-Drogba Dakika ya77
-Wilfred 81
+++++++++++++++++++++++
Algeria, ambao walikuwa wameshaaga Mashindano haya hata kabla ya Mechi ya leo, walikosa Penati iliyopigwa na Ryad Boudebouz katika Kipindi cha Kwanza lakini Sofiane Feghouli alifunga Bao lao la kwanza kwa Penati ya Kipindi cha Pili.
Hilal Soudani aliipatia Algeria Bao la pili na kufanya gemu iwe 2-0 lakini Didier Drogba aliipigia Ivory Coast Bao la kwanza na Wilfried Bony kuisawazishia Ivory Coast.
VIKOSI:
Algeria: M'Bolhi, Halliche, Mesbah, Belkalem, Mostefa, Boudebouz, Lemmouchia, Guedioura, Lacen, Soudani, Slimani
Akiba: Doukha, Cadamuro, Feghouli, Bouazza, Medjani, Aoudia, Kadir, Bezzaz, Tedjar, Ghoulam, Rial, Si Mohamed.
Ivory Coast: Yeboah, Boka, Ismael Traore, Toure, Lolo, Romaric, Razak, Kalou, Bony, Kone, Drogba
Akiba: Barry, Zokora, Tiote, Gervinho, Konan, Gradel, Tiene, Lacina Traore, Toure, Eboue, Bamba, Ali Sangare.
Refa: Eric Otogo-Castane (Gabon)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
KUNDI A
1 South Africa Mechi 3 Pointi 5
2 Cape Verde Mechi 3 Pointi 5
3 Morocco Mechi 3 Pointi 3
4 Angola Mechi 3 Pointi 1
KUNDI B
1 Ghana Mechi 3 Pointi 7
2 Mali Mechi 3 Pointi 4
3 Congo DR Mechi 3 Pointi 3
4 Niger Mechi 3 Pointi 1
KUNDI C
1 Burkina Faso Mechi 3 [Tofauti ya Magoli 4] Pointi 5
2 Nigeria Mechi 3 [Tofauti ya Magoli 2] Pointi 5
3 Zambia Mechi 3 Pointi 3
4 Ethiopia Mechi 3 Pointi 1
KUNDI D
1 Ivory Coast Mechi 3 Pointi 7
2 Togo Mechi 3 [Tofauti ya Magoli 1] Pointi 4
3 Tunisia Mechi 3 [Tofauti ya Magoli -2]  Pointi 4
4 Algeria Mechi 3 Pointi 1
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA/MATOKEO:
[SAA za BONGO]
Jumamosi Januari 19
South Africa 0 Cape Verde Islands 0
Angola 0 Morocco 0
Jumapili Januari 20
Ghana 2 Congo DR 2
Mali 1 Niger 0
Jumatatu Januari 21
Zambia 1 Ethiopia 1
Nigeria 1 Burkina Faso 1
Jumanne Januari 22
Ivory Coast 2 Togo 1
Tunisia 1 Algeria 0
Jumatano Januari 23
South Africa 2 Angola 0
Morocco 1 Cape Verde Islands 1
Alhamisi Januari 24
Ghana 1 Mali 0
Niger 0 Congo DR 0
Ijumaa Januari 25
Zambia 1 Nigeria 1
Burkina Faso 4 Ethiopia 0
Jumamosi Januari 26
Ivory Coast 3 Tunisia 0
Algeria 0 Togo 2
Jumapili Januari 27
Morocco 2 South Africa 2
Cape Verde Islands 2 Angola 1
Jumatatu Januari 28
Congo DR 1 Mali 1
Niger 0 Ghana 3
Jumanne Januari 29
Ethiopia 0 Nigeria 2
Burkina Faso 0 Zambia 0
Jumatano Januari 30
Algeria 2 Ivory Coast 2
Togo 1 Tunisia 1
ROBO FAINALI
Jumamosi Februari 2
Ghana v Cape Verde [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Afrika Kusini v Mali [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
Jumapili Februari 3
Ivory Coast v Nigeria [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Burkina Faso v Togo [Mbombela Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
NUSU FAINALI
Jumatano Februari 6
Mshindi RF 3 v Mshindi RF 2 [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi RF 1 v Mshindi RF 4 [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
MSHINDI wa TATU
Jumamosi Februari 9
[Nelson Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
FAINALI
Jumapili Februari 10
[Soccer City Saa 3 Usiku]

No comments:

Post a Comment