Monday, November 19, 2012

HIVI NDIVYO SIMBA NA AZAM WALIVYOFANYA BIASHARA YA OWINO


Joseph Owino anarudi nyumbani Msimbazi
AZAM FC wanataka Sh. Milioni 10 pamoja na kiungo Uhuru Suleiman kutoka Simba, ili wawape beki Mganda Joseph Owino.
Habari za ndani, ambazo  tumezipata  kutoka Azam, zinasema kwamba tayari makubaliano yamefikiwa lakini, Simba inaonekana kusuasua kutekeleza makubaliano hayo.
Azam wanadai wamekubaliana na Simba walipe fedha hizo Sh Milioni 10 na kumuidhinisha Uhuru kuhamia Chamazi, lakini suala la fedha bado halijatekelezwa.
“Tena hapo bado kuna kesi ya fedha nyingine, Sh. Milioni 5, ambazo Simba wanadaiwa na Uhuru, sisi tumekubali kumpa fedha hizo Uhuru, halafu wao tutawakata kwenye mapato ya mlangoni katika mechi yetu na wao ya marudiano,”kilisema chanzo kutoka Azam.
Lakini upande wa Simba nao wanasema fedha zote, Sh Milioni 15 walikubaliana zikatwe katika mapato ya milangoni.
Simba imeamua kumrejesha Owino, ili kuimarisha safu yake ya ulinzi, ambayo imeonekana kuyumba katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Lakini pia hiyo ni nafuu kwa beki huyo Mganda, ambaye ameshindwa kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha Azam chini ya makocha wote, kuanzia Mserbia Boris Bunjak aliyefukuzwa na huyu wa sasa Muingereza, Stewart Hall aliyerejeshwa kazini.

NYAMLANI AULA CAF

Athumani Nyamlani
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani ameteuliwa kuwemo kwenye Ujumbe rasmi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) utakaosimamia Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Januari mwakani nchini Afrika Kusini.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, uteuzi huo umefanywa na Rais wa CAF, Issa Hayatou na Kamati yake ya Utendaji. Ujumbe huo wa CAF kwa ajili ya fainali hizo zitakazoanza Januari 19 na kumalizika Februari 10 mwaka huu una jumla ya watu 148.
Wambura amesema Nyamlani atakuwa miongoni mwa wajumbe watatu, watakaoshughulikia masuala ya rufaa kwenye mashindano hayo. Wajumbe wengine ni Prosper Abega kutoka Cameroon na Pierre-Alain Monguengui wa Gabon. Nyamlani ni mjumbe wa Bodi ya Rufani ya CAF yenye watu 12.

CHAGUZI ZA TFF...


MCHAKATO wa uchaguzi wa Chama cha Soka Katavi (KAREFA), umefutwa kutokana na wagombea watano kati ya nane vyeti vyao vya elimu ya sekondari kuwa na utata. Mchakato wa uchaguzi huo utaanza upya Novemba 21 mwaka huu.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo amesema leo kwamba, mchakato wa uchaguzi wa Chama cha Wataalamu wa Tiba ya Michezo Tanzania (TASMA) utaanza upya Novemba 26 mwaka huu baada ya mchakto wa sasa kupata wagombea kwenye nafasi mbili tu za Kamati ya Utendaji ya chama hicho.
Mchakato wa uchaguzi wa RUREFA utaanza Novemba 26 mwaka huu na Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA itapewa maelekezo ya usimamiaji wa uchaguzi huo baada ya mchakato wa awali kuwa umefutwa kutokana na kufanyika bila kuzingatia kanuni za uchaguzi.
Wakati huo huo TFF, itakuwa na mkutano na Waandishi wa Habari utakaofanyika keshokutwa, saa 6:00 mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa shirikisho hilo.

 UCHAGUZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA KATAVI (KAREFA)  

 Mchakato wa uchaguzi wa KAREFA umefutwa kutokana na wagombea watano kati ya nane vyeti vyao vya elimu ya sekondari kuwa na utata. Mchakato wa uchaguzi huo utaanza upya Novemba 21 mwaka huu.

 
UCHAGUZI WA TASMA  
Mchakato wa uchaguzi wa Chama cha Wataalamu wa Tiba ya Michezo Tanzania (TASMA) utaanza upya Novemba 26 mwaka huu baada ya mchakto wa sasa kupata wagombea kwenye nafasi mbili tu za Kamati ya Utendaji ya chama hicho.

UCHAGUZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA RUKWA (RUREFA)  
Mchakato wa uchaguzi wa RUREFA utaanza Novemba 26 mwaka huu na Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA itapewa maelekezo ya usimamiaji wa uchaguzi huo baada ya mchakato wa awali kuwa umefutwa kutokana na kufanyika bila kuzingatia kanuni za uchaguzi.

 

NYINGINEZO:
++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za Juu:
1 Yanga Mechi 13 Pointi 29
2 Azam FC Mechi 13 Pointi 24
3 Simba Mechi 13 Pointi 23
4 Coastal Mechi 13 Pointi 22
++++++++++++++++++++++++++
Kwa sasa VPL imemesimama baada ya kumalizika kwa Mzunguko wa Kwanza na itarudi tena kilingeni Januari 26.
++++++++++++++++++++++++++
RAUNDI YA PILI
26TH JAN. 2013 - 18TH MAY, 2013.
Januari 26
African Lyon v Simba [National Stadium, Dar es Salaam]
Mtibwa Sugar v Polisi Morogoro [Manungu, Morogoro]
Coastal Union v Mgambo JKT [Mkwakwani, Tanga]
Ruvu Shootings v JKT Ruvu [Mabatini, Pwani]
Azam v Kagera Sugar [Azam Complex, Dar es Salaam]
JKT Oljoro v Toto Africans [Sheikh Amri Abeid, Arusha]
Januari 27
Yanga v Tanzania Prisons [National Stadium, Dar es Salaam]

SERENGETI BOYS WAINGIZA MILIONI 23 TU

Farid Mussa Shah wa Serengeto kulia akichuana na beki wa Kongo Brazzaville Tmouele Ngampio katika mechi hiyo

MECHI ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kati ya Tanzania, Serengeti Boys na Kongo Brazzaville iliyochezwa juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza Sh. 23,021,000.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo amesema  leo kwamba, mapato hayo yametokana na washabiki 18,022 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 10,000, sh. 5,000, sh. 2,000 na sh. 1,000. Washabiki 15,850 walikata tiketi za sh. 1,000.
Amesema asilimia 18 ya mapato hayo ambayo ni sh. 3,511,677.97 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh. 5,956,635), usafi na ulinzi (sh. 2,350,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing Construction (sh. 2,000,000), umeme (sh. 300,000) na ulinzi wa mechi (sh. 3,500,000).
Kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 1,000,537, asilimia 10 ya uwanja sh. 500,269, asilimia 5 ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) sh. 250,134, asilimia 45 ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,251,209, asilimia 20 ya TFF (sh. 1,000,537) na Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) sh. 50,027.

MWANASOKA BORA TANZANIA KUPATIKANA DESEMBA 30

Athimani Iddi 'Chuji' wa Yanga kulia akiwa katika moja ya mechi za Ligi Kuu dhidi ya Mgambo JKT. Je, ataingia kwenye orodha ya wachezaji wa kuwanai tuzo ya Mwanasoka Bora Tanzania?

FAINALI ya tuzo za Mwanasoka Bora wa mwaka Tanzania, zinazotolewa na Kampuni ya Wazalendo Bright Media zinatarajiwa kufanyika Desemba 30 mwaka huu mjini Dar es Salaam katika sehemu, ambayo itatangazwa baadaye.
Mratibu wa mchakato huo, Ahadi Kakore amesema leo kwamba, mchakato wake ulianza tangu Agosti mosi mwaka huu kwa wanamichezo kupigiwa kura na mashabiki kupitia mitandao mbalimbali ikiwemo ile ya kijamii (face book, Twitter na Blogs) na wengine kwa njia ya simu za mikononi kwa kupitia namba maalum.
Amesema kwa sasa kamati ipo kwenye mchakato ya kuchuja majina ambayo yamependekezwa na  mashabiki wa soka kupitia kura zao ambapo zaidi ya wachezaji 93 wanaocheza Ligi Kuu Tanzania Bara majina yao yameweza kuonekana ambapo kati ya majina hayo yataopunguzwa na kufikia 30.
Amesema kabla ya kufanyika kwa fainali hiyo wale wachezaji ambao wataingia kwenye fainali watapatiwa semina ya uwezekezaji na ujasiriamali ili kujiandaa na maisha ya baadaye baada ya kustaafu.
Amesema sababu za kufanya semina hii ni kuhakikisha kuwa wachezaji wetu wanapata elimu ya uwezekaji na ujasiriamali ili kuwekeza kwenye sekta mbalimbali kwa ajili ya siku zijazo hasa ikizingatiwa kwamba wachezaji wengi wa Tanzania bado ni masikini.
Kakore amesema kwenye semina hiyo watakuwepo wataalam waliobobea kwenye mambo ya uchumi na fedha ambao watatoa elimu ya uwekezaji, kwa kufanya hivi itawapa nafasi wachezaji hawa kuelewa na kutambua umuhimu wa uwekezaji.
Amesema semina hiyo inatarajiwa kufanyika Desemba 19 na  20 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam. Pamoja semina ambayo itakwenda sambamba na  utoaji wa elimu ya afya kwa washiriki wa semina hiyo ambao watakuwa wachezaji pekee. Amesema mshindi wa tunzo hiyo anatarajiwa kupata tuzo, fedha taslim, medali na cheti.

KILIMANJARO STARS WAKIJIFUA KWA TUSKER CHALLENGE 2012

Beki wa timu ya taifa ya Bara, Kilimanajro Stars, Kevin Yondan (kushoto) akiwa mazoezini kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, kujiandaa na mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge yanayotarajiwa kufanyika mjini Kampala, Uganda kuanzia Jumamosi wiki hii. Timu hii inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Bara, Kilimanajro Stars wakiwa mazoezini kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, kujiandaa na mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge yanayotarajiwa kufanyika mjini Kampala, Uganda kuanzia Jumamosi wiki hii. Timu hii inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.

 

NIYONZIMA, KAVUMBANGU KWAHERI YANGA

Haruna Niyonzima anakwenda El Merreikh

KLABU ya Yanga imepokea ofa kutoka klabu mbili tofauti, moja ya Asia na moja ya hapa hapa Afrika zikiwahitaji wachezaji wao mahiri wa kigeni, kiungo Haruna Niyonzima kutoka Rwanda na mshambuliaji Didier Kavumbangu kutoka Burundi.
Habari za ndani kutoka Yanga, zimesema kwamba, Niyonzima anatakiwa na klabu ya El Merreikh ya Sudan, wakati Kavumbangu anatakiwa na klabu moja ya Qatar.   
Tayari barua rasmi za kuwahitaji wachezaji hao zimekwishawasilishwa Yanga na hivi sasa klabu inaingia kwenye majadiliano ya bei na klabu hizo.
Klabu ya Qatar, ilitangaza ofa ya dola za Kimarekani 100,000 (zaidi ya Sh. Milioni 150), lakini Yanga imekataa dau hilo na inataka dola 300,000 (zaidi ya Sh. Milioni 450) kwa ajili ya Kavumbangu.
Kuhusu Niyonzima, Merreikh imeomba itajiwe bei ya mchezaji huyo na Yanga. “Merreikh wana fedha, hatuna wasiwasi nao, sisi tutaanzia dola 300,000 na hata tukishuka, si chini ya 200,000, hawa wachezaji ni lulu”kilisema chanzo kutoka Yanga.
Didier Kavumbangu anakwenda Qatar
Haruna alisajiliwa msimu uliopita Yanga kutoka APR ya Rwanda, wakati Kavumbangu amesajiliwa msimu huu kutoka Atletico Olympic ya Burundi.
Kavumbangu kwa sasa ndiye anaongoza kwa mabao katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara akiwa ametikisa nyavu mara nane, sawa na Kipre Tcheche wa Azam FC.
Wataalamu wa usajili wa Yanga, Seif Ahmad ‘Magari’ na Abdallah Ahmad ‘Bin Kleb’ tayari wanajiandaa kwenda Kampala, Uganda itakapofanyika michuano ya Kombe la Challenge kutafuta wachezaji wa kuziba nafasi za Kavumbangu na Niyonzima.
Lakini habari zaidi zinasema nafasi ya Niyonzima itazibwa na Kabange Twite kutoka APR ya Rwanda, ndugu wa mchezaji mwingine wa Yanga, Mbuyu Twite.  

 

 

 

 

 

 

 

FRIENDS OF SIMBA WAKUTANA KUJADILI MAMBO KLABUNI

Hans Poppe
KUNDI la Friends of Simba (F.O.S.) linatarajiwa kukutana kesho jioni kujadili mustakabali wa klabu kwa ujumla na kutoa msimamo wao mbele ya wanachama na wapenzi wa klabu hiyo.
Hamkani si shwari Simba kwa sasa baada ya timu kumaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ikitoka kuongoza kwa wastani wa pointi saba.
Mwenyekiti wa F.O.S., Zacharia Hans Poppe alisema jana kwamba, watakuwa na Mkutano kesho kujadili hali ya mambo klabuni kwao.
“Sisi kazi yetu ni kusapoti uongozi uliopo madarakani, kuhakikisha timu yetu inafanya vizuri, sasa hali inayoendelea sasa inatutia shaka kuelekea mwakani, ambako tutakuwa na mtihani wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na pia Ligi ya Mabingwa.
Kwa hivyo tutakutana, tutazungumza kwa mapana marefu sana, ili tujue undani na ukweli wa matatizo yaliyopo klabuni na baada ya hapo na sisi tutatoa mtazamo wetu,”alisema kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, Kamati ya Utendaji ya Simba, chini ya Mwenyekiti wake, Alhaj Ismail Aden Rage ilikutana na kufikia maamuzi ya kuvunja Kamati zote ndogondogo za klabu pamoja na kulifuta tawi la wanachama wakorofi, Mpira Pesa la Magomeni, waliomtukana kipa Juma Kaseja na kuendesha harakati za mapinduzi.  
Lakini pia wasiwasi umeingia kutokana na kuvunjwa pia kwa Kamati ya Usajili, iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Hans Poppe katika kipindi hiki kigumu ambacho klabu inatakiwa kurekebisha usajili kuelekea mzunguko wa pili na Ligi ya Mabingwa.
Mbali na hivyo, kuna suala la mchezaji Emanuel Okwi ambaye amemaliza mkataba wake kwenye klabu hiyo na alikuwa kwenye majadiliano na Kamati ya Usajili, ambayo yalifikia pazuri, lakini kwa kuvunjwa kwa Kamati hizo, maana yake mazungumzo hayo hayawezi kuendelea.  

YAW BERKO BADO YUPO YUPO SANA YANGA SC


Yaw Berko
KIPA Mghana, Yaw Berko hataachwa katika klabu ya Yanga kama ambavyo magazeti mengi nchini yamekuwa yakiandika.
Habari  kutoka ndani ya Yanga, zimesema kwamba Berko ambaye mkataba wake unamalizika Mei mwakani, ataendelea kuitumikia klabu hiyo hadi mwisho wa mkataba huo.
Kipa huyo anayelipwa mshahara wa Sh. Milioni 1.5 kwa mwezi, amerudishwa benchi siku za karibuni baada ya kufululiza kufungwa mabao rahisi, jambo ambalo lilimkera kocha Mholanzi, Ernie Brandts.
Kwa sababu hiyo, vyombo vya habari vikaanza kubashiri kwamba ataachwa mwezi ujao kwa sababu pia, tayari klabu hiyo imesajili mchezaji mwingine wa kigeni, Kabange Twite kutoka APR ya Rwanda.
Kanuni za Usajili za Ligi Kuu zinataka wachezaji watano tu wa kigeni kwa kila klabu, na Yanga tayari inao Yaw Berko, Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima kutoka Rwanda, Hamisi Kiiza kutoka Uganda na Didier Kavumbangu kutoka Burundi.
Lakini habari zaidi zinasema Kabange atachukua nafasi moja kati ya mbili zinazotarajiwa kuachwa na wachezaji wawili wa klabu hiyo, ambao watauzwa hivi karibuni, Niyonzima na Kavumbangu. 


JUVENTUS YAMUWINDA DROGBA.

KLABU ya Juventus ya Italia inapanga kumsajili mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Ivory Coast Didier Drogba anayecheza kwenye klabu ya Shanghai Shenhua ya China katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari mwakani. Mabingwa hao wa Serie A wamekuwa sokoni kwa kipindi kirefu wakitafuta mshambuliaji ambapo katika kipindi cha karibuni wamekuwa wakihusishwa na Fernando Llorente na Pablo Asvaldo na hivi sasa wamehamishia nguvu zao kumsajili Drogba mwenye umri wa miaka 34. Drogba alijunga na kabu hiyo inayoshiriki Ligi kuu nchini China kutoka Chelsea katika kipindi cha usajili cha majira ya kiangazi lakini anaonekana hana furaha na ana nia ya kurejea Ulaya tena. Sababu ya Drogba ambaye analipwa euro milioni 12 kwa mwaka ni kutofurahishwa na mazingira ya klabu hiyo kumcheleweshea mshahara wake zaidi ya mara moja toka alipohamia huko. Hatahivyo Juventus wanakabiliwa na wakati mgumu wa kumsajili mchezaji huyo kwa kuwa wamepanga kupunguza mshahara wake kama akikubalia kujiunga nao na kumlipa euro milioni 4.5 kwa mwaka pamoja na posho nyingine.

HUGHES KUBAKIA QPR.

MENEJA wa Queens Park Rangers, Mark Hughes atabakia kuinoa klabu hiyo ambayo inasuasua katika mstari wa kushuka daraja kufuatia mkutano aliofanya na Ofisa Mkuu wa klabu hiyo Philip Beard. Kuna taarifa zilizosambaa kuwa Hughes ambaye amewahi kuwa kocha wa Wales alifukuzwa baada ya wawili kukutana katika uwanja wa mazoezi jana lakini mwakilishi wa kocha huyo Kia Joobchian alikanusha tetesi hizo na kudai sio za kweli. Hughes amekuwa na matokeo mabaya toka mwanzoni mwa msimu huu akiwa ameambulia alama nne pekee katika michezo 12 ambayo timu hiyo imecheza msimu huu hivyo kushika mkia katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 49 ambaye amewahi kuzifundisha klabu za Blackburn Rovers, Manchester City na Fulham amesisitiza kuwa hawezi kujiuzulu kibarua hicho kufuatia kufungwa nyumbani mabao 3-1 na Southampton ambao wote wanapigania kutoshuka daraja.

KAGAWA KUKAA NJE WIKI NNE ZAIDI.

KIUNGO nyota wa klabu ya Manchester United, Shinji Kagawa ameongezewa wiki zingine nne kukaa nje ya uwanja kutokana na majeruhi yanayomsumbua. Kiungo huyo wa kimataifa wa Japan mwenye umri wa miaka 23 aliumia mguu wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ambao timu yake ilishinda kwa mabao 3-2 dhidi ya Braga Oktoba 23 mwaka huu. Meneja wa United Sir Alex Ferguson alimtegemea mchezaji huyo kupona katika kipindi cha wiki nne mpaka tano lakini nyota huyo ameonekana kupona taratibu hivyo kuna uwezekano wa kukaa nje ya uwanja kwa nyingine nne nyingine. Pamoja na habari mbaya kuhusu Kagawa lakini Ferguson amefarijika baada ya beki wake nyota Phil Jones kurejea katika kikosi chake baada ya kuumia mgongo wakati maandalizi ya msimu mpya wa ligi hiyo. Beki huyo mwenye umri wa miaka 20 anatarajiwa kuwepo katika mchezo wa kundi H leo ambapo United watakuwa wageni wa Galatasaray ya Uturuki.

BECKHAM KUIKACHA GALAXY MWISHONI MWA MSIMU.

Nahodha wa zamani wa Uingereza, DAVID BECKHAM anatarajiwa kuondoka katika klabu ya Los Angeles Galaxy mwezi ujao baada miaka sita kucheza katika Ligi Kuu nchini Marekani maarufu kama Major League. Nyota huyo amepanga kuikacha klabu hiyo baada ya msimu wa ligi hiyo kumalizika Desemba 1 mwaka huu. Katika taarifa yake BECKHAM mwenye umri wa miaka 37 amesema kuwa anahitaji changamoto nyingine kabla ya kuamua rasmi kustaafu soka. Klabu ya Melbourne Heart ya Australia imedai kuwa ipo katika mazungumzo na nyota huyo ili wamsajili kwa ajili ya mechi 10 nyota huyo pamoja na mwenyewe kudai kuwa hana mpango wa kucheza soka katika Ligi Kuu ya nchini humo maarufu kama A League. BECKHAM alianza kucheza soka katika klabu ya Manchester United ambapo akiwa hapo alifanikiwa kushinda taji la Ligi Kuu nchini Uingereza mara sita pamoja na taji moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kutua Real Madrid mwaka 2003 na baadae Marekani mwaka 2007.

KESI YA PARK KUSIKILIZWA LEO.

Kesi ya mchezaji soka wa kimataifa wa Korea Kusini ambaye aliyeleta msuguano wa kidiplomasia na Japan baada ya kupeperusha bango lenye maandishi ya kisiasa katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika London, Uingereza inatarajiwa kusikilizwa tena na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Kamati hiyo ambayo itaamua kama mchezaji huyo aitwaye PARK JONG-WOO atakabiliwa na adhabu ya kufungiwa kutokana na kitendo chake hicho alichokifanya mwishoni mwa mchezo wa kugombea nafasi ya tatu dhidi ya Japan, imekuwa ikishindwa kutoa uamuzi wakati ilipokutana Octoba kusikiliza kesi hiyo. Msemaji wa FIFA amesema kuwa hata kama uamuzi utafikiwa hii leo hautatangazwa kwa siku kadhaa mpaka ripoti kamili iweze kuandikwa na kutafsiriwa kabla ya kutolewa kwa wandishi wa habari. Kiungo huyo alishika bango lenye ujumbe ambao unaokumbushia tofauti za mipaka kati Korea Kusini na Japan wakati akishangilia ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya mahasimu wao hao. PARK alizuiwa kuhudhuria sherehe za kukabidhiwa medali ya shaba waliyopata lakini Chama cha Soka cha Korea-KFA mwezi uliopita kilitoa taarifa kuwa wametumiwa ujumbe kupitia kamati ya nchi iliyoandaa michuano ya olimpiki ikithibitisha kuwa mchezaji huyo atapokea medali yake. 

FIFPro na FIFA zatangaza Makipa 5 kugombea kuwemo Kikosi Bora Duniani 2012

FERGUSON_KUBADILI_KIPA_KILA_MECHIChama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa Duniani, FIFPro, pamoja na FIFA leo wametangaza Majina ya Makipa watano ambao watakuwemo ndani ya Listi ya mwisho ya Wachezaji 55 watakaotangazwa huko Mjini Sao Paulo, Brazil hapo Novemba 29 kugombea kuwemo kwenye ile Timu Bora Duniani, rasmi kama FIFA/FIFPro World XI 2012.
Listi hiyo ya Wachezaji 55, ambayo leo imeanza kwa Makipa, itaongezwa Mabeki, Viungo na Mafowadi ambao watatangazwa kwa awamu kwa kuanzia Mabeki, watakaotajwa Novemba 22, Viungo hapo Novemba 26 na Mafowadi Novemba 29 na kukamilisha Wagombea 55 ambao watapigiwa Kura kupata Kikosi Bora cha Wachezaji 11 kikiundwa na Kipa, Mabeki wanne, Viungo watatu na Mafowadi watatu.
+++++++++++++++++++++++
MAKIPA 5 WALIOTEULIWA:
-Gianluigi Buffon (Italy, Juventus)
-Iker Casillas (Spain, Real Madrid)
-Petr Cech (Czech Republic, Chelsea)
-Joe Hart (England, Manchester City)
-Manuel Neuer (Germany, Bayern Munich).
+++++++++++++++++++++++
Wachezaji 50,000, ambao ni Wanachama wa FIFPro, wamesambaziwa Fomu za kupigia Kura hicho Kikosi Bora.
Washindi watatangazwa Januari 7, 2013 kwenye Tafrija maalum ya kumpata Mchezaji Bora Duniani, Mshindi wa Tuzo ya the FIFA Ballon d’Or, itakayofanyika huko Zurich, Uswisi.
 

UEFA CHAMPIONS LIGI: NI patashika Juventus v Chelsea!

>>USHINDI MUHIMU kwa kila Timu, au BALAA!
>>MECHI: Novemba 20 UWANJA: Juventus Arena, Turin, Italy
Mabingwa wa Ulaya, Chelsea, wanaikwaa Juventus, Mabingwa wa Italy, na kila mmoja anataka ushindi ili ajihakikishie anatinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI lakini hii ni Mechi isiyotabirika ukizingatia Mwezi Septemba, ndani ya Stamford Bridge, Chelsea waliongoza Bao 2-0, kwa Bao za Oscar, lakini Juve wakazinduka na kusawazisha kwa Mabao ya Arturo Vidal na Fabio Quagliarella na kutoka 2-2.
++++++++++++++++++++++++++
KUNDI E
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Shakhtar Donetsk Pointi 7
2 Chelsea 7
3 Juventus 6
4 Nordsjaelland 1 [NJE]
FAHAMU: Timu mbili za juu toka kila Kundi zinaingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na Timu itakayomaliza nafasi ya 3 itaingizwa EUROPA LIGI.
++++++++++++++++++++++++++
JUVENTUS-Claudio_MarchisioIkiwa Chelsea hawatafungwa na Juventus ni wazi watafuzu kwani Mechi yao ya mwisho ni nyumbani Stamford Bridge dhidi ya Nordsjaelland ambayo imeshatupwa nje ya Mashindano na ambayo Chelsea waliibonda Bao 4-0 huko kwao Denmark.
Chelsea wataingia kwenye Mechi hii bila ya nguzo yao kubwa, Nahodha wao John Terry, ambae ni majeruhi lakini Mabingwa hawa wa Ulaya nguzo yao kubwa zaidi ni Mashambulizi wakitegemea kasi na ushirikiano wa kina Ramires, Eden Hazard, Oscar, Juan Mata kumlisha Straika wao Fernando Torres.
Juve, wakiongozwa na Mkongwe Andrei Pirlo kwenye Kiungo na ambao walitoka sare Mechi zao zote 3 za kwanza za Kundi hili na kuzinduka tu katika Mechi ya 4 walipowaponda vibonde Nordsjaelland Bao 4-0, wana Wachezaji wengine hatari kama vile Kiungo Claudio Marchisio [Pichani], Mirko Vucinic, Arturo Vidal na Fabio Quagliarella.
Hawa wanatisha hasa ukizingatia Chelsea, chini ya Kocha Roberto Mancini, ina Difensi  ‘nyanya’ ambayo imevujisha Mabao 17 katika Mechi zao 8 zilizopita.
Katika Mechi za Ligi zao za Wikiendi hii iliyopita, Chelsea walichapwa 2-1 na WBA na Juventus kuambua sare ya 0-0 walipocheza na Lazio bila ya kuwa na nguzo yao kubwa Andrei Pirlo ambae alikuwa kifungoni.
Juve, ambao wapo chini ya Kocha Angelo Alessio kwa vile Kocha wao Antonio Conte yuko kifungoni, wameshatamka hii ni ‘Mechi yao ya Mwaka.’
Hakika ni patashika.
++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Mechi zote kuanza SAA 4 DAK 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
Jumanne Novemba 20
FC Nordsjælland v FC Shakhtar Donetsk
Juventus v Chelsea FC
FC BATE Borisov v LOSC Lille [SAA 2 Usiku]
Valencia CF v FC Bayern München
FC Spartak Moskva v FC Barcelona [SAA 2 Usiku]
SL Benfica v Celtic FC
Galatasaray A.S. v Manchester United FC
CFR 1907 Cluj v SC Braga
Jumatano Novemba 21
FC Porto v GNK Dinamo
FC Dynamo Kyiv v Paris SaintvGermain FC
Arsenal FC v Montpellier Hérault SC
FC Schalke 04 v Olympiacos FC
FC Zenit St. Petersburg v Málaga CF [SAA 2 Usiku]
RSC Anderlecht v AC Milan
AFC Ajax v Borussia Dortmund
Manchester City FC v Real Madrid CF
++++++++++++++++++++++++++++++++

UEFA CHAMPIONZ LIGI: Man United bila Mastaa kibao yaenda Uturuki!

>>KUIVAA Galatasaray bila Rooney, RVP, Rio, Evra, De Gea, Giggs, Scholes!!
>>MECHI: Novemba 20 UWANJA: Turk Telecom Arena, Istanbul, Turkey
Manchester United, ambao wameshafuzu toka Kundi H la UEFA CHAMPIONZ LIGI wakiwa Nambari Wani huku wana Mechi mbili mkononi, leo wamesafiri kwenda Uturuki kucheza na Galatasaray bila Mastaa wao wengi.
++++++++++++++++++++++++++
KUNDI H
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Man United Pointi 12 [IMEFUZU]
2 Galatasaray 4
3 CFR Cluj-Napoca 4
4 Braga 3
FAHAMU: Timu mbili za juu toka kila Kundi zinaingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na Timu itakayomaliza nafasi ya 3 itaingizwa EUROPA LIGI.
++++++++++++++++++++++++++
MAN_UNITED-ANDO_RVP_SHINJI_EVRAMastaa ambao hawakuwemo kwenye msafara ni Wayne Rooney, Robin van Persie, Rio Ferdinand, Ryan Giggs, Paul Scholes, Patrice Evra, Valencia na David de Gea pamoja na majeruhi Nani (Musuli ya Paja), Shinji Kagawa (Goti) na Jonny Evans (Nyonga).
Kikosi ambacho kimeenda Uturuki kinao Chipukizi 7 ambao hawajacheza Mechi za Ulaya ambao ni pamoja na Nick Powell, Larnell Cole, Davide Petrucci, Joshua King, Marnick Vermijl,  na Ryan Tunnicliffe na wawili ambao hawajacheza hata Mechi moja ya Kikosi cha Kwanza ni Kiungo Tom Thorpe na Kipa Sam Johnstone.
Rooney na De Gea hawakucheza Mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu England ambayo Man United walifungwa 1-0 na Norwich City  na wote waliripotiwa ni Wagonjwa lakini leo walifanya mazoezi kama kawaida Kituo cha Carrington huko Jijini Manchester.
Inasadikiwa Bosi wa Man United Sir Alex Ferguson, akijua Timu yake imeshafuzu, ameamua kuwapumzisha Mastaa wake.
KIKOSI KAMILI KILICHOSAFIRI: Sam Johnstone, Anders Lindegaard; Rafael, Alexander Buttner, Phil Jones, Tom Thorpe, Marnick Vermijl, Scott Wootton, Michael Carrick, Davide Petrucci, Larnell Cole, Tom Cleverley, Darren Fletcher, Anderson, Nick Powell, Ashley Young, Ryan Tunnicliffe, Javier Hernandez, Joshua King, Danny Welbeck, Federico Macheda.
++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Mechi zote kuanza SAA 4 DAK 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
Jumanne Novemba 20
FC Nordsjælland v FC Shakhtar Donetsk
Juventus v Chelsea FC
FC BATE Borisov v LOSC Lille [SAA 2 Usiku]
Valencia CF v FC Bayern München
FC Spartak Moskva v FC Barcelona [SAA 2 Usiku]
SL Benfica v Celtic FC
Galatasaray A.S. v Manchester United FC
CFR 1907 Cluj v SC Braga
Jumatano Novemba 21
FC Porto v GNK Dinamo
FC Dynamo Kyiv v Paris SaintvGermain FC
Arsenal FC v Montpellier Hérault SC
FC Schalke 04 v Olympiacos FC
FC Zenit St. Petersburg v Málaga CF [SAA 2 Usiku]
RSC Anderlecht v AC Milan
AFC Ajax v Borussia Dortmund
Manchester City FC v Real Madrid CF
++++++++++++++++++++++++++++++++


BPL: Inaelekea patamu!!

BPL_LOGO>>MTANANGE WIKIENDI IJAYO STAMFORD BRIDGE: Chelsea v Man City!
Mabingwa watetezi, Manchester City, wametwaa uongozi wa BPL, Barclays Premier League, Ligi Kuu England, baada ya Wikiendi hii iliopita kuitwanga Aston Villa Bao 5-0 huku waliokuwa vinara Manchester United wakichapwa 1-0 na Norwich City na Chelsea wakipigwa bao 2-1 na WBA lakini Ligi hii sasa ndio kumekucha na Mechi mfululizo zitaziandama Klabu zikiwemo zile za UEFA CHAMPIONZ LIGI, EUROPA LIGI na CAPITAL ONE CUP kwa baadhi ya Klabu huku Chelsea, ambaio ndio Mabingwa wa Ulaya, wakiwa na safari ya kwenda Japan Mwezi Desemba kucheza Mashindano ya FIFA kusaka Klabu Bingwa Duniani.
Wikiendi ijayo, Jumapili Novemba 25, Uwanja wa Stamford Bridge utawaka moto kwa mtanange mkali kati ya Chelsea na Man City.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
1 Man City Mechi 12 Pointi 28
2 Man United Mechi 12 Pointi 27
3 Chelsea Mechi 12 Pointi 24
4 WBA Mechi 12 Pointi 23
5 Everton Mechi 12 Pointi 20
6 Arsenal Mechi 12 Pointi 19
7 West Ham Mechi 11 Pointi 18
8 Tottenham Mechi 12 Pointi 17
9 Fulham Mechi 12 Pointi 16
10 Swansea Mechi 12 Pointi 16
11 Liverpool Mechi 12 Pointi 15
+++++++++++++++++++++++
Wakati Stamford Bridge ikiwaka, Jumamosi Novemba 24, Old Trafford itashuhudia Man United  wakitaka kutwaa tena uongozi watakapocheza na Timu ya mkiani QPR.
+++++++++++++++++++++++
RATIBA ZA BPL kwa VIGOGO:
MAN CITY
MAN UNITED
CHELSEA
Nov 25 Chelsea v Man City
Nov 28 Wigan v Man City
Des 1 Man City v Everton
Des 9 Man City v Man Utd
Des 15 Newcastle v Man City
Des 22 Man City v Reading
Des 26 Sunderland v Man City
Des 29 Norwich v Man City
Jan 1 Man City v Stoke
Nov 24 Man Utd v QPR
Nov 28 Man Utd v West Ham
Des 1 Reading v Man Utd
Des 9 Man City v Man Utd
Des 15 Man Utd v Sunderland
Des 23 Swansea v Man Utd
Des 26 Man Utd v Newcasctle
Des 29 Man Utd v WBA
Jan 1 Wigan v Man Utd
Nov 25 Chelsea v Man City
Nov 28 Chelsea v Fulham
Des 1 West Ham v Chelsea
Des 8 Sunderland v Chelsea
Des 23 Chelsea v Aston Villa
Des 26 Norwich v Chelsea
Des 30 Everton v Chelsea
Jan 2 Chelsea v QPR
RIPOTI mechi ya Jumapili Novemba 18
Fulham 1 Sunderland 3
Jumapili Novemba 18, Uwanjani Craven Cottage, wenyeji Fulham walicheza Mtu 10 kwa Saa nzima baada ya Beki wao wa kutumainiwa Brede Hangeland kupewa Kadi Nyekundu kwa rafu mbaya na hilo liliwafanya wakubali kichapo cha Bao 3-1 toka kwa Sunderland huo ukiwa ushindi wa pili wa Sunderand katika Mechi 18 za BPL, Ligi Kuu England.
MAGOLI:
Fulham 1
-Petric 62′
Sunderland 3
-Fletcher 50′ Cuellar 65′ Sessegnon 70′
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumatatu Novemba 19
[SAA 5 Usiku]
West Ham V Stoke
Jumamosi Novemba 24
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Sunderland V West Brom
[SAA 12 Jioni]
Everton V Norwich
Man Utd V QPR
Stoke V Fulham
Wigan V Reading
[SAA 2 Dak 30 Usiku]
Aston Villa V Arsenal
Jumapili Novemba 25
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Swansea V Liverpool
[SAA 12 Jioni]
Southampton V Newcastle
[SAA 1 Usiku]
Chelsea V Man City
Tottenham V West Ham
Jumanne Novemba 27
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Sunderland V QPR
[SAA 5 Usiku]
Aston Villa V Reading
Jumatano Novemba 28
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea V Fulham
Everton V Arsenal
Southampton V Norwich
Stoke V Newcastle
Swansea V West Brom
Tottenham V Liverpool
Man Utd V West Ham
[SAA 5 Usiku]
Wigan V Man City

No comments:

Post a Comment