KOCHA wa timu ya taifa
ya Uingereza Roy Hodgson anaamini kuwa changamoto ya mikwaju ya penati
katika michezo ya kirafiki ambayo watatoa sare inaweza kuisadia timu
hiyo kuondokana na jinamizi la kupoteza nafasi katika michuano mikubwa. Uingereza
imekuwa mhanga mkubwa wa kutolewa katika michuano mikubwa kwa
changamoto ya mikwaju ya penati wakiwa wamepoteza mara sita kati ya saba
mara mwisho ikiwa katika robo fainali ya michuano ya Ulaya dhidi ya
Italia iliyofanyika Juni mwaka huu. Wakiwa
katika maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia 2014, Hodgson amesema
kuwa katka mojawapo ya mechi za kirafiki watakazotoka sare atashauri
wapinzani wake wamalize mchezo huo kwa changamoto ya mikwaju ya penati. Amesema
kwa kufanya hivyo kutawaongezea uzoefu zaidi wachezaji mbele ya
mashabiki wengi kuliko kufanya hivyo wakiwa mazoezini peke yake. Mwaka
2013 Uingereza itakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Brazil na baadae
dhidi ya Ireland kabla ya kucheza na Scotland katika mchezo wa kufuzu
Kombe la Dunia.
No comments:
Post a Comment