MESSI AZUNGUMZA ASEMA MABAO YANGU SIO MUHIMU KAMA TIMU HAISHINDI - MESSI.
MSHAMBULIAJI nyota wa
Barcelona, Lionel Messi amesisitiza kuwa mabao anayofunga hayatakuwa na
maana yoyote kama timu yake itakuwa haiwezi kushinda`mechi zake. Mshambuliaji
huyo amekuwa katika kiwango kizuri miezi 12 ambapo amefunga mabao 91 na
kuipita rekodi iliyowekwa miaka 40 iliyopita na Gerd Muller aliyefunga
mabao 85 katika kipindi cha mwaka mmoja lakini nyota huyo amesema
ushindi wa timu yake ndio wenye umuhimu kuliko rekodi binafsi. Messi
ambaye yuko nchini kwao Argentina kwa mapumziko ya kipindi cha baridi
katika La Liga amesema amefurahi kufunga mabao mengi na kuvunja rekodi
lakini mwaka ungekuwa mzuri zaidi kama wangishinda mataji kwani siku
zote amekuwa akisisitiza mabao hayani maana yoyote kama timu haishindi
chochote. Messi
ambaye pia mwaka huu alipata mtoto wake wa kwanza aitwae Thiago amesema
ujio wa mtoto huyo umemfanya awe mtu mwenye furaha na kuwashukuru
wapenzi wote wa soka wa Argentina ambao husafiri kwenda kumshangilia
wakati akicheza.
No comments:
Post a Comment