Thursday, December 20, 2012

LEEDS UNITED NA CHELSEA JANA KATIKA CAPITAL ONE CUP;MOSES APIGA BONGE LA GOLI NJE YA 18 INGIA ULIONEE


 

EUROPA LIGI: DROO RAUNDI YA TIMU 32 HIYOOO!

EUROPA_LIGI_CUP>>MABINGWA wa ULAYA Chelsea v SPARTA PRAGUE!!
>> ZENIT V LIVERPOOL, NEWCASTLE V METALIST KHARKIV, SPURS V LYON
DROO ya Mechi za EUROPA LIGI kwa Raundi ya Mtoano ya Timu 32 imefanyika leo huko Nyon, Uswisi na sambamba na hiyo kila Timu inajua ikifuzu Raundi hiyo na kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 nani watakuwa Wapinzani.
DROO KAMILI:
RAUNDI ya MTOANO TIMU 32:
BATE Borisov v Fenerbache
Inter Milan v Cluj
Levante v Olympiakos
Zenit St Petersburg v Liverpool
Dynamo Kiev v Bordeaux
Bayer Leverkusen v Benfica
Newcastle v Metalist Kharkiv
Stuttgart v Genk
Atletico Madrid v Rubin Kazan
Ajax v Steaua Bucharest
Basel v Dnipro
Anzhi Makhachkala v Hannover
Sparta Prague v Chelsea
Borussia Monchengladbach v Lazio
Tottenham v Lyon
Napoli v Viktoria Plzen
RATIBA ya MECHI:
Mechi ya 1=14 Februari 2013
Mechi ya 1=21 Februari 2013
RAUNDI ya MTOANO TIMU 16:
Napoli au Viktoria Plzen v BATE Borisov au Fenerbache
Leverkusen au Benfica v Dynamo Kiev au Bordeaux
Anzhi Makhachkala au Hannover v Newcastle au Metalist
Stuttgart au Genk v Monchengladbach au Lazio
Tottenham au Lyon v Inter Milan au Cluj
Levante au Olympiakos v Atletico Madrid au Rubin Kazan
Basel au Dnipro v Zenit St Petersburg au Liverpool
Ajax au Steaua Bucharest v Sparta Prague au Chelsea
RATIBA ya MECHI:
Mechi ya 1=7 Machi 2013
Mechi ya 2=14 Machi 2013
+++++++++++++++++++
RATIBA HATUA YA MTOANO
RAUNDI YA TIMU 32:
Mechi ya 1=14 Februari 2013
Mechi ya 1=21 Februari 2013
RAUNDI YA TIMU 16:
Mechi ya 1=7 Machi 2013
Mechi ya 2=14 Machi 2013
ROBO FAINALI:
Mechi ya 1=4 Aprili 2013
Mechi ya 2=11 Aprili 2013
NUSU FAINALI
Mechi ya 1=25 Aprili 2013
Mechi ya 2=2 Mei 2013
FAINALI
15 Mei 2013
UWANJA wa AMSTERDAM ARENA

 

NUSU FAINALI UHAI KESHO



MECHI za Nusu fainali ya michuano ya Kombe la Uhai 2012 inayoshirikisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zitachezwa kesho (Desemba 21 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Nusu fainali ya kwanza ya michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Said Salim Bakhresa kupitia maji Uhai itazikutanisha timu za Mtibwa Sugar ya Morogoro na Azam na itafanyika kuanzia saa 2 kamili asubuhi.
Simba na Coastal Union zitacheza nusu fainali ya pili kuanzia saa 10 kamili jioni kwenye uwanja huo huo. Mtibwa Sugar imepata tiketi ya nusu fainali baada ya kuichapa African Lyon mabao 3-1 wakati Simba iliilaza Oljoro JKT mabao 2-0.
Nayo Azam iliindoa JKT Ruvu kwenye robo fainali kwa bao 1-0 huku Coastal Union ikipata ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mechi ya mwisho ya robo fainali.
Mechi ya fainali na ile ya kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa Jumapili (Desemba 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Mechi ya mshindi wa tatu itaanza saa 2 kamili asubuhi wakati ya fainali itakuwa saa 10 kamili jioni.

TFF YAWAPONGEZA ZEN C NA WENZAKE TWFA


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) linaupongeza uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika jana (Desemba 19 mwaka huu) hoteli ya Midlands mjini Morogoro.
Ushindi aliopata Lina Kessy aliyechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti pamoja na wajumbe wengine wa Kamati ya Utendaji unaonesha jinsi ambavyo wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TWFA walivyo na imani kwao.
TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya TWFA, na kwamba ina changamoto kubwa ya kuhakikisha inaendesha shughuli za chama hicho kwa kuzingatia katiba na kanuni.
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA chini ya Mama Ombeni Zavala na Kamati ya Uchaguzi ya TFF inayoongozwa na Deogratias Lyatto kwa kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa utulivu na kwa kuzingatia Katiba ya TWFA na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Safu mpya ya uongozi wa DRFA inaundwa na Lina Kessy (Mwenyekiti), Rose Kissiwa (Makamu Mwenyekiti), Amina Karuma (Katibu), Zena Chande (Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa TFF) wakati mjumbe wa Kamati ya Utendaji ni Triphonia Temba.

TENGA ATOA NOTISI KWA MUJIBU WA KATIBA

Tenga

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ambaye ndiye Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo tayari ametoa notisi ya mkutano huo utakaofanyika Februari 23 na 24 mwakani jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo utafanyika Februari 23 mwakani na kufuatiwa na ajenda ya uchaguzi siku inayofuata. Ajenda ya uchaguzi iko chini ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Notisi hiyo imetumwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ambao ni kutoka vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki, klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF.
Ajenda za Mkutano Mkuu zitatumwa kwa wajumbe siku 15 kabla ya mkutano huo wenye wajumbe zaidi ya 100.

KIM NA WAANDISHI KESHO

Kim Poulsen
MAKOCHA wa Tanzania (Taifa Stars), Kim Poulsen na Zambia (Chipolopolo) watakuwa na mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika kesho (Desemba 21 mwaka huu) kuzungumzia pambano lao litakalochezwa Jumamosi (Desemba 22 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mkutano huo utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Makocha hao watazungumzia maandalizi yao ya mwisho kabla ya pambano hilo litakalochezeshwa na mwamuzi Sylvester Kirwa kuanzia saa 10 kamili jioni.
Pia makocha hao watajibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari kuhusu pambano hilo litakalokutanisha timu hizo ambazo zimefanya vizuri kwenye orodha ya viwango vya ubora vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) vilivyotolewa jana (Desemba 19 mwaka huu).
Wakati Zambia ambao ni mabingwa wa Afrika wamepanda juu kwa viwango vya ubora kwa nafasi nne, Taifa Stars ambayo katika mchezo uliopita iliifunga Kenya (Harambee Stars) bao 1-0 imepanda kwa nafasi nne.
Taifa Stars ambayo inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini tangu Desemba 12 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo kubwa ya kirafiki inayotarajiwa kuwa ya kuvutia.

MWINGINE AMWAGA MPUNGA MKUTANO TASWA, ITAKUWAJE SIKU HIYO?

Mhando, katibu wa TASWA
KAMPUNI ya Msama Promotions inayoandaa Tamasha la Pasaka imeahidi kutoa Sh. Milioni 1.5 kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utakaofanyika Bagamoyo mkoani Pwani wiki ijayo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ambaye ndiye Mkurugenzi wa kampuni hiyo amesema ushirikiano wake  na wanahabari umemsukuma kusaidia kiasi hicho cha fedha.
Msama ameahidi kuendelea kushirikiana na TASWA kadri awezavyo na kwamba mafanikio ya Tamasha la Pasaka yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na wanahabari.
“Kampuni yangu ya Msama Promotions kupitia Tamasha la Pasaka tumeamua kuungana na wanahabari katika kufanikisha mkutano wenu, tunaamini uhusiano wetu utaendelea kuwa wa kupigiwa mfano,” ilisema sehemu ya taarifa ya TASWA jana ikimkariri Msama.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando alishukuru kwa udhamini huo na kuomba wengine wenye moyo wajitokeze kuwasaidia kwani bajeti yao ni Sh. Milioni 20. Tayari kampuni ya simu za mkononi ya Zantel imeshatangaza udhamini wa Sh. Milioni sita.
Mhando alisema maandalizi ya Mkutano Mkuu wa TASWA utakaofanyika wiki ijayo Bagamoyo mkoani Pwani yanaendelea vizuri na kwamba zaidi ya wanachama 100 wa TASWA na wadau wengine wa TASWA wamethibitisha kushiriki.
Wakati huo huo: TASWA imewapongeza wanachama wake Benny Kisaka na Zena Chande kwa kufanikiwa kuwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Kisaka alishinda wadhida huo wiki iliyopita kupitia uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), wakati Chande alishika Jumatano katika uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake Tanzania (TWFA).
“Tunaamini wajumbe wa Mkutano Mkuu DRFA na wale wa TWFA hawakufanya makosa, wamefanya uamuzi sahihi na wamepata watu sahihi na makini na michango yao itakuwa yenye tija kubwa kwa maendeleo la mpira wa miguu hapa nchini. Tunawatakia kila la heri wanachama wetu hao katika changamoto mbalimbali watakazokutana nazo kwenye nafasi zao hizo walizopata,”amesema Amir Mhando, Katibu Mkuu TASWA.

MESSI CHALI TUZO YA MWANASOKA BORA

ULIZA kikundi cha watu ni mtu gani wanaamini kuwa ndiye mwanamichezo bora duniani, jina la Lionel Messi ndilo utakalolisikia mara nyingi.
Isipokuwa kikundi hicho kikiwa kinaundwa na waandishi wa habari wa Argentina,ambao hawaoni kama Messi ni bora hata kwa nchini mwao tu. Wala nafasi ya piliwanaona hashiki.Ila ni nafasi ya tatu aliyoshika nyota huyo wa Barcelona nyuma ya bondia Sergio Martinez na mpiganaji wa taekwondo, Sebastian Crismanich. 

Pretty good year: Sergio Martinez with his trophy after beating Sebastian Chrismanich and Lionel Messi to the award
Sergio Martinez akiwa na tuzo yake baada ya kumshinda Sebastian Chrismanich na Lionel Messi 
Ready for it: Martinez will fight British boxer Martin Murray in April 2013
Niko tayari: Martinez atapambana na bondia wa Uingereza Martin Murray Aprili 2013

Mafanikio bab'kubwa aliyonayo Messi mwaka huu ya kuvunja rekodi iliyodumu kwa miaka 40 bada ya kufunga magoli 90 hadi sasa haikutosha kumpa tuzo hiyo.Martinez alishinda taji la Olimpia de Oro baada ya kumchapa  Mmexico Julio Cesar Chavez Jr katika taji la ubingwa wa WBC mapema mwaka huu. Atapigana na bondia  Muingereza Martin Murray Aprili 2013.

What, not me? Lionel Messi finished third in the poll of Argentine journalists
What, not me? Lionel Messi amemaliza wa tatu katika tuzo ya waandishi wa habari ya mwanamichezo bora wa Argentina.

Crismanich, yeye, alikuwa mtu pekee wa Argentina aliyeshinda medali ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki ya London 2012."Ni heshima kubwa kushinda tuzo hii ambayo ilikuwa ikiwaniwa na wanamichezo kama Sebastian Crismanich na Leo Messi," Martinez alisema katika sherehe ya tuzo hizo Jumanne usiku.
Lakini kwa kuwa alishashinda tuzo hiyo ya Argentina mwaka 2011 na kwa kuwa anapewa nafasi kubwa zaidi ya kubeba kwa mara ya nne mfululizo tuzo ya Ballon d'Or ya Mwanasoka Bora wa Dunia 2012, Messi hawezi kuwa amefadhaishwa sana.

No comments:

Post a Comment