YANGA SASA TISHA MBAYA, SIMBA CHUPUCHUPU MOROGORO
Msuva kushoto na Domayo kulia, wakimpongeza Kavumbangu kufunga bao la pili |
YANGA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara baada ya jioni ya leo kuichapa Mgambo JKT ya Handeni,
Tanga mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, unaifanya Yanga sasa iwe na pointi sawa na
mabingwa watetezi, Simba SC waliotoa sare ya 1-1 na Polisi mjini Morogoro leo,
ingawa inazidiwa bao moja tu katika wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-0,
yaliyotiwa kimiani na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na mshambuliaji Didier
Kavumbangu.
Cannavaro alifunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Oscar
Joshua dakika ya pili kutoka wingi ya kulia, wakati Kavumbangu alimalizia pasi
ya Hamisi Kiiza dakika ya 39.
Pamoja na kutoka uwanjani wamelowa kipindi cha kwanza, lakini
Mgambo JKT walicheza soka ya kuvutia na mara mbili walikaribia kufunga kupitia
kwa Juma Mwinyimvua.
Yanga walicheza vema dakika 45 za kipindi cha kwanza, tofauti
sana na mechi za awali ambazo wamekuwa ‘wakichezewa’ sana na wapinzani.
Ilishuhudiwa katika kipindi hicho, Yanga wakimiliki zaidi
mpira na kupeana pasi za uhakika, ingawa mashambulizi yao mengi walipitisha
pembeni, hasa upande wa kulia.
Hamisi Kiiza, Msuva na Kavumbangu walicheza kwa uelewano
mkubwa pale mbele na kulitia misukosuko haswa lango la Mgambo.
Kipindi cha pili, Yanga walirudi na moto wao tena na
kuendelea kuwachachafya Mgambo.
Hata hivyo, iliwachukua Yanga dakika 34 kupata bao la tatu,
mfungaji akiwa ni Jerry Tegete aliyeingia dakika ya 68 kuchukua nafasi ya
Kavumbangu.
Tegete alifunga bao hilo akiunganisha krosi maridadi ya beki
wa kushoto, Oscar Joshua.
Pamoja na kufungwa, Mgambo waliendelea kusukuma mashambulizi
langoni mwa Yanga, ingawa leo mabeki wa timu hiyo, inayofundishwa na Mholanzi,
Ernie Brandts walicheza kwa uelewano mkubwa na kudhibiti hatari zote langoni
mwao.
Mgambo inayofundishwa na Mohamed Kampira, ilipata pigo dakika
ya 85, baada ya beki wake wa kulia, Salum Mlima kutolewa kwa kadi nyekundu ya
moja kwa moja kwa kumchezea rafu mbaya Mbuyu Twite.
Baada ya mchezo huo, Brandts alisema dakika 10 za mwanzo timu
yake ilikuwa inashindwa kumalizia vizuri mashambulizi yake, lakini baadaye
ikatulia na hatimaye kupata ushindi huo, ambao ameufurahia kwani unamuweka
katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Kwa upande wake, Kampira wa Mgambo alisema kufungwa ni sehemu
ya mchezo, akawasifu Yanga kwa kutumia nafasi walizopata, huku akijutia nafasi
walizopoteza wachezaji wake leo.
Kikosi cha Yanga leo kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’,
Nsajigwa Shadrack/Kevin Yondan dk 46, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Nadir Haroub
‘Cannavaro’, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Frank Domayo/Nurdin Bakari dk
76, Didier Kavumbangu/Jerry Tegete dk68, Hamisi Kiiza na Haruna Niyonzima.
Mgambo JKT; Godson Mmasa, Salum Mlima, Yassin Awadh, Salum
Kipanga/Godfrey Komba dk80, Bakari Mtama, Ramadhani Malima, Chande Magoja,
Mussa Ngunda, Issa Kandulu/Nassor Gumbo dk 60, Fully Maganga na Juma Mwinyimvua/Omar
Matwiko dk76.
Katika mchezo wa utangulizi, timu ya vijana chini ya umri wa
miaka 20 ya Yanga, imeifunga Mgambo JKT ya vijana pia 1-0, bao hilo pekee la
Clever Charles dakika ya 65.
Katika mechi nyingine, Simba ilitoka sare ya 1-1 Polisi
kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, wenyeji wakitangulia kupata bao dakika ya
35 kupitia kwa Mokili Rambo kabla ya Amri Kiemba kusawazisha dakika ya 57. SIRI YA BUNJAK KUFUKUZWA AZAM HII HAPA
Bunjak |
WACHEZAJI wa
Azam ndio waliomponza kocha Mserbia, Boris Bunjak kufukuzwa kazi jana, baada ya
kuuandikia barua uongozi, wakisema hawaridhishwi na ufundishaji wa kcoha huyo
na hawamtaki.
Pamoja na
kumchongea kwa uongozi Mserbia huyo, habari za ndani kutoka Azam zimesema kwamba,
ni wachezaji hao hao waliopendekeza katika barua yao kurejeshwa kwa aliyekuwa
kocha wa timu hiyo, Muingereza Stewart Hall.
Habari zilizopatikana
jana kutoka Azam FC, zilisema kwamba, sababu za kufukuzwa kwa Mserbia huyo ni
kushuka kwa kiwango cha timu, hali iliyosababisha sasa ianguke hadi nafasi ya
nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Tayari
Bunjak amekwishapewa haki zake zote na ataondoka kesho, siku ambayo Stewart anaweza
kuwasili kuanza tena kazi Azam FC.
Bunjak
anaondoka Azam baada ya kuiongoza timu katika mechi 16, akifungwa nne tu, zote
dhidi ya Simba ikiwemo ya juzi ya Ligi Kuu, waliyofungwa 3-1 na kutoa sare
tatu.
Bunjak
mwenye leseni ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), alitua Azam, Agosti 7, mwaka
huu akitokea FC Damac ya Saudia Arabia aliyoanza kuifundisha mwaka jana na
kabla ya hapo alifundisha klabu kibao za kwao, zikiwemo FK Sloga Kraljevo, FK
Javor Ivanjica, Crvena Zvezda Gnjilane, FK Radnicki Nis, FC Uralan Elista, FK
Mladi Radnik, FK Crvena Zvezda Beograd, Al-Shaab, FK Hajduk Kula na Al-Nasr.
Awali,
Bunjak aliyezaliwa Novemba 17, mwaka 1954 ( miaka 57), alicheza soka katika
klabu za FK Sloga (Kraljevo), FK Vozdovac (Beograd), FK Radnicki (Kragujevac),
FK Olimpia (Ljubljana), FK Sumadija (Arandjelovac), FK Sloga (Kraljevo), FK
Borac (Cacak) na FK Sloga (Kraljevo).
Stewart
alifukuzwa kwa kosa la kukaidi maagizo ya Bodi ya Ukurugenzi ya klabu hiyo,
kumpanga Mrisho Khalfan Ngassa katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya Yanga.
Mserbia huyo
anakuwa kocha wa tano kufukuzwa Azam, ndani ya miaka minne tangu ianze kucheza
Ligi Kuu, 2008 baada ya Stewart, Mbrazil Neider dos Santos, Sylvester Marsh na
Itamar Amorin, Mbrazil mwingine.
Lakini Stewart
angalau aliacha kumbukumbu ya taji na Medali Azam, baada ya kuiwezesha kutwaa
Kombe la Mapinduzi Januari, kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Aprili,
kabla ya kushika nafasi ya pili Kombe la Urafiki na Kagame mwezi uliopita,
mambo ambayo bila shaka yamemfanya afikiriwe tena.
Stewart ana
sifa ya kutokuwa mbinafsi na mwenye kuwaamini watu wa chini yake, kwa mfano
namna ambavyo alikuwa akimpromoti Kali Ongala. Alimkuta Kali kama mchezaji,
lakini kwa sababu ya umri kumtupa mkono, akashauriana naye awe Kocha Msaidizi
na mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga, akakubali.
Chini ya
Stewart, Kali alikuwa akiachiwa timu aiongoze ili kumjengea kujiamini zaidi na
mwezi uliopita aliachiwa timu kwenye Kombe la Urafiki, akaifikisha fainali,
ambako ilifungwa na Simba kwa penalti kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika
90.
REKODI YA BORIS BUNJAK AZAM
Azam 2-1
Polisi (BancABC)
Azam 1-2
Simba B (BancABC)
Azam 8-0
Trans Camp (Kirafiki)
Azam 1-0
Prisons (Kirafiki)
Azam 2-0
Coastal Union (Kirafiki)
Azam 2-3
Simba SC (Ngao ya Jamii)
Azam 1-0
Kagera Sugar (Ligi Kuu)
Azam 2-2
Toto African (Ligi Kuu)
Azam 3-0 JKT
Ruvu (Ligi
Kuu)
Azam 1-0
Mtibwa Sugar (Ligi Kuu)
Azam 1-0
African Lyon (Ligi Kuu)
Azam 2-3
Simba SC (Kirafiki)
Azam 1-0
Polisi (Ligi Kuu)
Azam 0-0 Prisons (Ligi Kuu)
Azam 1-1
Ruvu Shooting (Ligi Kuu)
Azam 1-3
Simba (Ligi Kuu)YANGA B WAITILIA UBANI YANGA A, WAYACHAPA KIDUDE MAKINDA YA MGAMBO
Timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Yanga, imeifunga
Mgambo JKT ya vijana pia, bao 1-0 katika mchezo wa utangulizi, Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam, kabla ya kuanza kwa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,
baina ya kaka zao, Yanga A dhidi ya Mgambo JKT ya Handeni, Tanga. Bao hilo
pekee lilitiwa kimiani na Clever Charles dakika ya 65.
Zuberi Amiri wa Yanga B, akichuana na Charles Domayo wa JKT Mgambo |
Joseph Banda wa Yanga B (25) akipasua ukuta wa Mgambo |
Meshack Ramadhani wa Yanga kushoto akigombea mpira na beki wa Mgambo |
Banda akifumua shuti mbele ya mabeki wa Mgambo, mmoja akijaribu kuzuia |
Notikel Masasi wa Yanga B akiwa chini ya ulinzi wa mabeki wa Mgambo |
Kocha Ernie Brandts akifuatilia vipaji Yanga B ikicheza na Mgambo |
Notikel Masasi wa Yanga B, akichuana na mchezaji wa Mgambo |
Clever Charles, mfungaji wa bao la Yanga B leo, akiwa benchi baada ya kupumzishwa. Kulia kwake ni Said Manduta. |
MILIONEA SEIF MAGARI AKUBALI KUGOMBEA UENYEKITI DRFA
Seif Ahmad 'Magari' |
Wadau wa soka Dar es Salaam tangu wiki iliyopita wamekuwa
wakimbembeleza Seif kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo, wakiahidi kumuunga
mkono mfanyabiashara huyo wa magari na fedha za kigeni kwa asilimia 100 ashinde
nafasi hiyo.
Seif amesema leo kwamba amekubali
wito huo wa wana Dar es Salaam na atachukua fomu ya kuwania nafasi hiyo.
Lini? “Itakapokuwa tayari nitakuambia, ila jambo la msingi tu
nimekubali,”alisema Seif. Seif amekuwa kwenye Kamati za Yanga tangu wakati wa
uongozi wa Francis Mponjoli Kifukwe miaka saba iliyopita na pia amewahi kuwa mmiliki
mshiriki wa klabu ya Moro United iliyokuwa Ligi Kuu.
Seif ameendelea kuwa ndani ya Kamati za Yanga katika zama za
viongozi waliomfuatia Kifukwe katika klabu hiyo, Imani Madega, Lloyd Nchunga na
sasa Yussuf Manji.
Iwapo Seif atachukua fomu, kuna uwezekano mpinzani wake mkuu
akawa, Mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Evans Aveva
ambaye naye pia ana uzoefu wa kutosha katika uongozi wa soka.
Aveva, aliyekuwa Meneja wa Hoteli ya Embassy na sasa mfanyabiashara
mwenye maduka kibao ya simu, amekuwa kwenye Kamati mbalimbali za uongozi Simba
tangu enzi za Yussuf Hazali, Mwenyekiti wa klabu hiyo na ameendelea pia hata
katika zama za viongozi waliofuatia akina Juma Salum (sasa marehemu) na Hassan
Daalal.
Aveva pia amewahi kuwa mmoja wa viongozi wa iliyokuwa
Tanzania Stars, timu iliyokuwa ikiundwa na wachezaji wakongwe nchini, ambayo
mwaka 1998 na 1999 ilicheza Kombe la Washindi Afrika.
Uchaguzi wa DRFA utafanyika Desemba 8, mwaka huu na fomu za
kugombea nafasi mbalimbali zilianza kutolewa tangu jana, wakati Novemba 4 hadi
8, Kamati ya Uchaguzi, chini ya Mwenyekiti wake, Juma Simba itapitia fomu za
walioomba uongozi.
Novemba 9 hadi 13 utakuwa muda wa pingamizi kwa wagombea,
ambazo zitajadiliwa Novemba 14 hadi 16, wakati Novemba 17 hadi 19 watatoa fursa
ya kukata rufaa, ambazo zitasikilziwa Novemba 20 hadi 24 na baada ya hapo,
Novemba 25 yatatangazwa majina ya wagombea waliopitishwa.
Uchaguzi wa DRFA utafanyika siku chache tu kabla ya uchaguzi
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mwishoni mwa Desemba, mwaka huu. FA YASUBIRI TAARIFA KUTOKA SERBIA JUU YA KUFUNGIWA WACHEZAJI WAKE KUTOKANA NA VURUGU.
CHAMA cha Soka nchini
Uingereza-FA kimethibitisha kuwa hawajapewa taarifa juu ya uamuzi wa
maofisa wa polisi nchini Serbia kuwahusisha wachezaji wawili wa timu ya
taifa chini ya miaka 21 ya Uingereza kwa vurugu.
Shirikisho
la Soka nchini Serbia liliwafungia viungo Nokla Ninkovic na
mshambuliaji Ognjen Mundrinski kucheza katika timu za taifa lakini
mamlaka ya kisheria ilitangaza kuwashitaki watu 12 katika vurugu hizo
yakiwemo majina mawili ya Uingereza.
Katika
taarifa ya FA ilithibitisha kuwa hawajapata taarifa rasmi zozote kuhusu
kufungiwa kwa wachezaji wake na shirikisho la soka ya Serbia na kwamba
wanasubiri maelezo zaidi kuhusiana na sakata hilo.
Taarifa
hiyo ilimalizwa kwa kusema FA itawapa msaada wachezaji pamoja na
viongozi waliokumbana na sakata hilo nchini Serbia wiki mbili
zilizopita.
DJOKOVIC AJIHAKIKISHIA KUMALIZA NAMBA MOJA.
Djokovic alipoteza nafasi yake hiyo kwa Federer mwenye umri wa miaka 31 baada ya kunyakuwa michuano ya Wimbledon lakini Federer ambaye anatoka Switzerland hataweza kutetea taji la Paris Masters.
Kutokuwepo kwa Federer katika michuano hiyo mikubwa ya dunia ya mwisho kwa mwaka huu ambayo itafanyika Novemba 5 kunampa nafasi Djokovic kurejea katika kiti chake.
Djokovic mwenye umri wa miaka 25 anakuwa nyota wa kwanza kumaliza mwaka katika nafasi ya kwanza mfululizo toka Federer alipofanya hivyo kuanzia mwaka 2004 mpaka 2007.
CAPITAL ONE CUP: MECHI YA MIGOLI 12, Arsenal yashinda 7-5!!
>>THEO WALCOTT APIGA HETITRIKI!!
Katika Mechi za Raundi ya 4 ya Mtoano ya
CAPITAL ONE CUP zilizochezwa Jumanne Usiku, Mechi ya ajabu na vuta
nikuvute ni ile iliyochezwa Uwanja wa Madejski ambapo Reading waliongoza
4-0, mapumziko kuwa 4-1 mbele lakini Arsenal wakasawazisha na kuifanya
gemu iwe 4-4 hadi Dakika 90 na katika Dakika 30 za nyongeza Arsenal
walikwenda mbele 5-4, Reading wakarudisha na kuwa 5-5 na hatimae Arsenal
kuibuka Mshindi 7-5 huku Theo Walcott akipiga hetitriki.
+++++++++++++++++++++++++
CAPITAL ONE CUP-MATOKEO:
RATIBA RAUNDI ya 4:
Jumanne Oktoba 30
Sunderland 0 Middlesbrough 1
Swindon 2 Aston Villa 3
Wigan 0 Bradford 0 [Baada Dakika 120, Mshindi Bradford 4-2 kwa Mikwaju ya Penati]
Leeds 3 Southampton 0
Reading 4 Arsenal 4 [Baada Dakika 120, Mshindi Arsenal Bao 7-5]
+++++++++++++++++++++++++
READING 5 ARSENAL 7
MAGOLI:
Reading
-Jason Roberts, 12
-Koscielny, 19
-Leigertwood, 20
-Hunt, 37
-Pogrebnyak, 115
Arsenal
-Walcott, 45, 90 & 120
-Giroud, 64
-Koscielny, 89
-Chamakh, 103 & 120
VIKOSI:
Reading: Federici, Gunter, Gorkss, Morrison, Shorey, Tabb, McCleary, Leigertwood, Robson-Kanu, Roberts, Hunt
Akiba: Stuart Taylor, Pearce, Pogrebnyak, Le Fondre, McAnuff, Church, Harte.
Arsenal: Martinez, Jenkinson, Koscielny, Djourou, Miquel, Arshavin, Frimpong, Coquelin, Walcott, Chamakh, Gnabry
Akiba: Shea, Giroud, Squillaci, Bellerin, Eisfeld, Meade, Yennaris.
Refa: Kevin Friend
WIGAN 0 BRADFORD 0
Bradford washinda kwa Penati 4-2 baada ya sare ya 0-0 katika Dakika 120.
VIKOSI:
Wigan: Al Habsi, Ramis, Watson, Lopez, Stam, Fyvie, Jones, Redmond, Gomez, Boselli, McManaman
Akiba: Pollitt, Kone, Maloney, Beausejour, Golobart, Kiernan, Orsula.
Bradford: Duke, Darby, McHugh, McArdle, Meredith, Hines, Thompson, Doyle, Atkinson, Wells, Hanson
Akiba: McLaughlin, Connell, Gary Jones, Baker, Brown, Bass, Swain.
Refa: Roger East
SUNDERLAND 0 MIDDLESBROUGH 1
MFUNGAJI: McDonald, 39
VIKOSI:
Sunderland: Westwood, Bardsley, O'Shea, Cuellar, Colback, Johnson, Cattermole, Vaughan, Sessegnon, Fletcher, Saha
Akiba: Mignolet, Campbell, Wickham, McFadden, Kilgallon, Meyler, McClean.
Middlesbrough: Steele, Hoyte, Hines, Bikey, Friend, Ledesma, Leadbitter, Bailey, Haroun, Miller, McDonald
Akiba: Leutwiler, Zemmama, Halliday, Parnaby, Park, Reach, Smallwood.
Refa: Phil Dowd
SWINDON 2 ASTON VILLA 3
MAGOLI:
Swindon
-Sorey, 78 & 81
Villa
-Benteke, 30 & 90
-Agbonlahor, 39
VIKOSI:
Swindon: Foderingham, Devera, McCormack, Flint, McEveley, Ritchie, Miller, Ferry, Roberts, Benson, Collins
Akiba: Bedwell, Archibald-Henville, Nathan Thompson, Williams, Louis Thompson, Storey.
Aston Villa: Given, Lowton, Herd, Vlaar, Lichaj, Weimann, Ireland, El Ahmadi, Bannan, Agbonlahor, Benteke
Akiba: Guzan, Bent, Albrighton, Holman, Delph, Stevens.
Refa: Stuart Attwell
LEEDS 3 SOUTHAMPTON 0
MAGOLI:
-Tonge, 35
-El Hadj Diouf, 88
-Becchio, Penati, 90
VIKOSI:
Leeds: Ashdown, Peltier, Lees, Pearce, White, Byram, Austin, Brown, Tonge, Varney, Diouf
Akiba: Kenny, Drury, Green, Becchio, Pugh, Norris, Gray.
Southampton: Kelvin Davis, Butterfield, Hooiveld, Seaborne, Reeves, Mayuka, Chaplow, De Ridder, Ward-Prowse, Lee, Do Prado
Akiba: Gazzaniga, Shaw, Stephens, Chambers, Hoskins, Sinclair, Isgrove.
Refa: Chris Foy
+++++++++++++++++++++++++
CAPITAL ONE CUP
RATIBA RAUNDI ya 4:
Mechi kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku, Bongo Taimu
Jumatano Oktoba 31
Norwich v Tottenham
Liverpool v Swansea [SAA 5 Usiku]
Chelsea v Manchester United
No comments:
Post a Comment