KIIZA DIEGO AREJEA KUONGEZA NGUVU YANGA
Kiiza |
HAMISI Friday
Kiiza maarufu Diego Milito, amerejea jana Dar es Salaam na leo anaingia
kambini, Uplands Hotel, Changanyikeni kuungana na wenzake kujiandaa na mchezo
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting Jumamosi wiki hii
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kiiza alikuwa Uganda, kuichezea timu yake ya taifa, The
Cranes katika mchezo wa marudiano wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe
la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Afrika Kusini.
Uganda ilitolewa na Zambia kwa mikwaju ya penalti baada ya
sare ya jumla ya 1-1, Zambia wakianza kushinda nyumbani 1-0 na Uganda wakashinda
kwao 1-0 pia mwishoni mwa wiki, hivyo mchezo kuhamia kwenye mikwaju ya penalti,
ambako timu ya Kiiza ilitolewa.
Pamoja na kuweka kambi Changanyikeni, lakini Yanga inafanya
mazoezi kwenye Uwanja wa shule ya sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam.
Beki Kevin Yondan aliyeumizwa na kiungo wa Simba, Haruna
Moshi ‘Boban’ katika mechi baina ya wapinzani hao wa jadi, Oktoba 3, mwaka huu,
anaendelea vizuri na mazoezi mepesi sawa na mshambuliaji Said Bahanuzi
aliyekuwa anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.
Bahanuzi
‘Spider Man’ alichanika nyama za paja la mguu wa kulia katika mechi ya Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba
Jumatatu wiki iliyopita.
Bahanuzi
aliumia dakika ya 23, baada ya kugongana na beki Benjamin Effe wa Kagera Sugar
na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Jerry Tegete
katika mechi ambayo Yanga ililala 1-0, beo pekee la Themi Felix.
Bahanuzi
ndiye tegemeo la mabao la Yanga kwa sasa, kwani tangu ajiunge na timu hiyo
akitokea Mtibwa Sugar msimu huu, ameifungia mabao 12 katika mechi 13, ikiwemo
ile dhidi ya Kagera aliyocheza kwa dakika 23 kabla ya kuumia na kutoka.
Yanga kwa
sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 11,
baada ya kucheza saba, kushinda tatu, sare mbili na kufungwa mbili.
Simba
iliyocheza mechi nane, inaongoza ligi hiyo kwa pointi zake 18, ikifuatiwa na
Azam FC yenye pointi 17, iliyocheza mechi saba.
MILOVAN: IMENISIKITISHA, LAKINI NDIYO SOKA, TUNAGANGA YAJAYO
Simba na Kagera jana |
PROFESA Milovan Cirkovick, amesema sare mbili mfululizo
ambazo timu yake imezipata katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ni kweli
zimemsononesha, lakini hayo ni mambo ya kawaida katika soka.
Akizungumza baada ya sare ya jana dhidi ya Kagera Sugar
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam alisema matokeo hayo yamemsikitisha kwa ujumla
na hana jinsi zaidi ya kukubali kwa kuwa hiyo ndiyo soka.
Alipotoka 0-0 na Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga
alisema ni kwa sababu ya Uwanja mbaya na kuwakosa nyota wake kadhaa, wakiwemo
Emmanuel Okwi na Mrisho Ngassa, lakini jana alikuwa katika Uwanja mzuri na
alikuwa na nyiota wake hao pia.
“Ni soka, katika soka yanatokea mambo haya, sasa najipanga
kwa ajili ya mchezo ujao, ili tusiendelee na matokeo haya,”alisema Milovan,
ambaye Jumapili anarudi kwenye Uwanja mbaya, Mkwakwani kukipiga na JKG Mgambo
katika mfululizo wa ligi hiyo.
Simba jana ililazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Kagera
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hiyo ikiwa sare ya pili mfululizo kwa
Wekundu hao wa Msimbazi, baada ya Jumamosi pia kulazimishwa sare ya bila
kufungana na Coastal Union mjini Tanga.
Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 18 na kuendelea
kuongoza Ligi Kuu, kutokana na Azam FC kulazimishwa sare ya bila kufungana na
Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0,
lililotiwa kimiani na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu
Jr. dakika ya nane, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’
kutoka wingi ya kulia.
Kwa ujumla kipindi cha kwanza timu zote zilishambuliana kwa
zamu, ingawa ni Simba walioonekana kufanya mashambulizi ‘yenye akili’ zaidi.
Kipindi cha pili Simba ilirudi na moto tena na katika dakika
ya 51, Mrisho Khalfan Ngassa aliifungia timu hiyo bao la pili kwa shuti kali
lililowababatiza mabeki wa timu hiyo na kutinga nyavuni.
Hilo lilikuwa bao la tatu kwa Ngassa tangu ajiunge na Simba
katika mechi tisa alizoichezea timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi.
Baada ya hapo, Kagera walizinduka na kuanza kulishambulia
lango la Simba kupitia pembeni na katika dakika ya 64 Themi Felix aliunganisha
kwa kichwa krosi ya George Kavilla na kuifungia Kagera bao la kwanza.
Bao liliwazindua Kagera, ambao waliongeza kasi ya
kulishambulia lango la Simba na katika dakika ya 66, Juma Nyosso alimkwatua
kwenye eneo la hatari Paul Ngwai na Salum Kanoni akaenda kumtungua Juma Kaseja,
akiisawazishia Kagera.
Baada ya hapo timu zilianza kushambuliana kwa zamu na mpira
ulinoga zaidi kutokana na mashambulizi ya pande zote mbili.
Katika mechi nyingine, Mgambo imeshinda mechi ya tatu
mfululizo, baada ya kuifunga Toto African 2-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani,
Tanga. JKT Ruvu imezinduka baada ya kuifunga Polisi Morogoro 2-0 kwenye Uwanja
wa Jamhuri, Morogoro na JKT Oljoro imetoka 0-0 na African Lyon.
Simba SC;
Juma Kaseja (Nahodha), Nassor Masoud ‘Chollo’/Uhuru
Suleiman, Amir Maftah, Paschal Ochieng, Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto,
Amri Kiemba, Haruna Moshi/Jonas Mkude, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi
na Mrisho Ngassa.
Kagera Sugar; Andrew Ntala, Salum Kanoni, Martin Muganyizi, Amandus
Nesta (Nahodha), Benjamin Effe/Themi Felix, Malegesi Mwangwa, Daudi Jumanne/Kamana
Salum, George Kavilla, Shijja Mkinna, Enyinna Darlington na Wilfred Ammeh/Paul
Nwai.
Katika mchezo wa awali, Simba B iliifunga Moro United mabao
3-0 katika mchezo wa utangulizi kabla ya mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara kati ya Simba na Kagera Sugar, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mabao ya Simba B inayofundishwa na Suleiman Matola,
akisaidiwa na Amri Said ‘Stam’ yalipatikana yote kipindi cha pili, wafungaji
Ramadhan Salum dakika ya 65 na 70 na Miraj Athumani dakika ya 85. Moro United inajiandaa na Ligi Daraja la
Kwanza, inayotarajiwa kuanza Oktoba 24, mwaka huu.
KIBADENI AFICHUA SIRI YA KUWAKAMATIA MBAVUNI SIMBA
Kibadeni |
KOCHA wa Kagera Sugar, Abdallah Athumani Seif ‘Kibadeni’
amesema kwamba alijua ataifunga Simba jana, lakini bahati mbaya ikawa sare na
ameridhika na matokeo hayo pia kwa ilikuwa mechi ya ugenini.
Kibadeni alisema kwamba katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara, kilichompa matumaini ya kuifunga Simba ni kwa sababu
anamjua vizuri kocha wa timu hiyo, Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick kwa kuwa
alifanya naye kazi.
“Mimi nilijua tu nitawapa tabu Simba, kwa sababu Milovan
ninamjua, nimefanya naye kazi mimi Simba, ufundishaji wake naujua,”alisema
Kibadeni.
Kagera jana ilitoka nyuma kwa mabao 2-0 na kupata sare ya 2-2
na Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hiyo ikiwa sare ya pili
mfululizo kwa Wekundu hao wa Msimbazi, baada ya Jumamosi pia kulazimishwa sare
ya bila kufungana na Coastal Union mjini Tanga.
Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 18 na kuendelea
kuongoza Ligi Kuu, kutokana na Azam FC kulazimishwa sare ya bila kufungana na
Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0,
lililotiwa kimiani na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu
Jr. dakika ya nane, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’
kutoka wingi ya kulia.
Kwa ujumla kipindi cha kwanza timu zote zilishambuliana kwa
zamu, ingawa ni Simba walioonekana kufanya mashambulizi ‘yenye akili’ zaidi.
Kipindi cha pili Simba ilirudi na moto tena na katika dakika
ya 51, Mrisho Khalfan Ngassa aliifungia timu hiyo bao la pili kwa shuti kali
lililowababatiza mabeki wa timu hiyo na kutinga nyavuni.
Hilo lilikuwa bao la tatu kwa Ngassa tangu ajiunge na Simba
katika mechi tisa alizoichezea timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi.
Baada ya hapo, Kagera walizinduka na kuanza kulishambulia
lango la Simba kupitia pembeni na katika dakika ya 64 Themi Felix aliunganisha
kwa kichwa krosi ya George Kavilla na kuifungia Kagera bao la kwanza.
Bao liliwazindua Kagera, ambao waliongeza kasi ya
kulishambulia lango la Simba na katika dakika ya 66, Juma Nyosso alimkwatua
kwenye eneo la hatari Paul Ngwai na Salum Kanoni akaenda kumtungua Juma Kaseja,
akiisawazishia Kagera.
Baada ya hapo timu zilianza kushambuliana kwa zamu na mpira
ulinoga zaidi kutokana na mashambulizi ya pande zote mbili.
Katika mechi nyingine, Mgambo imeshinda mechi ya tatu
mfululizo, baada ya kuifunga Toto African 2-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani,
Tanga. JKT Ruvu imezinduka baada ya kuifunga Polisi Morogoro 2-0 kwenye Uwanja
wa Jamhuri, Morogoro na JKT Oljoro imetoka 0-0 na African Lyon.
Simba SC;
Juma Kaseja (Nahodha), Nassor Masoud ‘Chollo’/Uhuru
Suleiman, Amir Maftah, Paschal Ochieng, Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto,
Amri Kiemba, Haruna Moshi/Jonas Mkude, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi
na Mrisho Ngassa.
Kagera Sugar; Andrew Ntala, Salum Kanoni, Martin Muganyizi, Amandus
Nesta (Nahodha), Benjamin Effe/Themi Felix, Malegesi Mwangwa, Daudi Jumanne/Kamana
Salum, George Kavilla, Shijja Mkinna, Enyinna Darlington na Wilfred Ammeh/Paul
Nwai.
Katika mchezo wa awali, Simba B iliifunga Moro United mabao
3-0 katika mchezo wa utangulizi kabla ya mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara kati ya Simba na Kagera Sugar, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mabao ya Simba B inayofundishwa na Suleiman Matola,
akisaidiwa na Amri Said ‘Stam’ yalipatikana yote kipindi cha pili, wafungaji
Ramadhan Salum dakika ya 65 na 70 na Miraj Athumani dakika ya 85. Moro United inajiandaa na Ligi Daraja la
Kwanza, inayotarajiwa kuanza Oktoba 24, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment