LA LIGA: Wiki ngumu kwa Barca kuelekea EL CLASICO na Real!
Jumamosi, 29 Septemba 2012 13:40

Jumamosi Septemba 29

Valencia v Real Zaragoza
Malaga v Real Betis
Real Sociedad v Athletic Bilbao
Sevilla v Barcelona
Jumapili Septemba 30
Granada v Celta Vigo
Real Valladoid v Rayo Vallecano
Osasuna v Levante
Real Madrid v Deportivo La Coruna
Espanyol v Atletico Madrid
Oktoba 1
Getafe v Real Mallorca
++++++++++++++++++++++++++
LEO, FC Barcelona, Kikosi cha Tito
Vilanova, kinaanza Wiki yao ngumu kwa kucheza ugenini kwenye Mechi ya La
Liga na Sevilla ambayo haijafungwa Msimu huu, Jumanne wako ugenini
kucheza na Benfica kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI na Jumapili Oktoba 7 wapo
kwao Nou Camp kuwavaa Mahasimu wao Real Madrid kwenye EL CLASICO ya La
Liga.
Hadi sasa Barcelona ndio wanaongoza La
Liga wakiwa Pointi 8 mbele ya Mabingwa Real Madrid ambao Jumapili
watacheza nyumbani na Deportivo La Coruna na kufuatiwa na Mechi yao ya
UEFA CHAMPIONZ LIGI ugenini na Ajax Amsterdam hapo Oktoba 3.
Ingawa wapo juu ya Real Madrid,
Barcelona hawaichukulii kimzaha tripu yao ya kwenda kucheza na Sevilla
ambao Msimu huu kwenye Ligi wameshinda Mechi 3 na kutoka sare mbili
katika Mechi zao 5.
Lakini Real Madrid, licha ya kuanza kwa
kusuasua, sasa wanaonyesha wameirudisha kampeni yao ya kutetea Taji lao
kwenye reli baada ya Rayo Vallecano bao 2-0 katika Mechi yao ya mwisho
ya Ligi Jumatatu iliyopita.
Nao Atletico Madrid, ambao wako Pointi
mbili nyuma ya Barcelona, wakiingozwa na anaetamba kwa kufunga bao
nyingi, Radamel Falcao, mwenye bao 7, watacheza ugenini na Espanyol
ambao wako nafasi ya pili toka mkiani.
na tano juma
LEO Arsenal v Chelsea: NI DABI ya LONDON yenye Takwimu kibao!
Jumamosi, 29 Septemba 2012 10:43

LEO ndani ya Emirates, katika Mechi ya
Ligi Kuu England, Arsenal, walio nafasi ya 5 na Pointi 4 nyuma,
wanapambana na vinara wa Ligi Chelsea katika Dabi ya Timu za London huku
ikimpambanisha Meneja wa Arsenal Arsene Wenger na wa Chelsea, Roberto
Di Matteo ambae ni Meneja wa 10 tangu himaya ya Wenger ianze Miaka 16
iliyopita huko Emirates.
Kwa mara ya kwanza katika Miaka 8,
Arsenal inaingia Uwanjani bila kukutana na ‘Muuaji wao Mkuu’ Straika wa
Chelsea Didier Drogba ambae amehamia Uchina.
+++++++++++++++++++++++++++++++
TAKWIMU Mechi zinazomhusu Drogba v Arsenal:
Katika Mechi 33 za Ligi Kuu
England kati ya Arsenal na Chelsea, rekodi ya Chelsea ikiwa na Drogba ni
nzuri ni bora kupita ikicheza bila ya yeye:
WAKIWA na DROGBA: W7 D3 L1
BILA DROGBA: W0 D9 L13
+++++++++++++++++++++++++++++++
Katika Mechi 40 walizocheza za Ligi zama
za Ligi Kuu, kumekuwa na jumla ya Mabao 108 yaliyofungwakatika Mechi
zao yakiwemo Mabao 8 yaliyofungwa Mwezi Oktoba Mwaka jana Arsenal
ilipoibamiza Chelsea 5-3 Uwanjani Stamford Bridge.
+++++++++++++++++++++++++++++++
MAMENEJA wa Chelsea zama za Wenger:
-Ruud Gullit: 1996 - 1998
-Luca Vialli: 1998 - 2000
-Claudio Ranieri: 2000 - 2004
-Jose Mourinho 2004 -2007
-Avram Grant 2007 - 2008
-Luiz Felipe Scolari 2008 -2009
-Guus Hiddink 2009
-Carlo Ancelotti 2009 - 2011
-Andre Villas-Boas 2011 - 2012
-Roberto Di Matteo 2012 – hadi sasa
+++++++++++++++++++++++++++++++
Arsenal, wakicheza Uwanja wao wa nyumbani, wameifunga Chelsea Mechi 36 kati ya 75 walizocheza huku Chelsea wakishinda 19 tu.
Ikiwa Arsenal watashinda leo, kwa Meneja Arsene Wenger huu utakuwa Ushindi wake wa 350 katika Mechi za Ligi Kuu England.
na tano juma
UBAGUZI: Anton Ferdinand afunguka!
Jumamosi, 29 Septemba 2012 10:09
>>FERGIE aona Kifungo kwa Terry chepesi, hategemei RIO kuitwa England!!

Anton Ferdinand, Beki wa QPR, ametoboa
kwenye Mtandao wa Twitter akiwajibu wale waliomponda kuhusu msimamo wake
Mahakamani kwenye Jopo Huru la FA lililosikiliza Kesi hiyo.
Amesema: “Watu lazima wawe wakweli na wasinitumie posti za kipuuzi kuhusu mimi, watazame Mkanda wa Tukio, Video haidanganyi!”
Katika Mkanda huo wa Video, Terry
ananaswa akitukana ingawa mwenyewe amejitetea kuwa maneno hayo alikuwa
akirudia kile anachodhani Ferdinand alisema akimtuhumu yeye Terry
kukisema.
Ingawa Mahakamani John Terry alishinda
Kesi lakini FA imempata na hatia na sasa ana Siku 14 kukukubali au
kukataa adhabu hiyo na kukata Rufaa.
Wakati huo huo, Meneja
wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, anaamini kifungo cha Mechi 4
kwa John Terry ni chepesi lakini pia kujiuzulu kwa Terry kuchezea Timu
ya Taifa hakumfungulii njia kwa Rio Ferdinand, Kaka wa Anton Ferdinand,
kuitwa tena kuichezea England.
+++++++++++++++++++++++
MASENTAHAFU ENGLAND:
•Rio Ferdinand (Man United) - Mechi 81
•Joleon Lescott (Man City) - Mechi 23
•Phil Jagielka (Everton) - Mechi 14
•Gary Cahill (Chelsea) - Mechi 10
•Phil Jones (Man United) - Mechi 5
•Chris Smalling (Man United) - Mechi 3
•Ryan Shawcross (Stoke) - Mechi 0
•Steven Caulker (Spurs) - Mechi 0
•Steven Taylor (Newcastle) - Mechi 0
+++++++++++++++++++++++
Ingawa Meneja wa England, Roy Hodgson,
amekuwa akidai hajamwita Rio Ferdinand kuichezea England kwa sababu za
Kisoka tu, lakini wengi wanaamini kutoitwa kwake kunahusiana na
kufarakana kwa John Terry na Anton Ferdinand.
Kuhusu Terry, Ferguson, ambae
alishuhudia hivi juzi Mchezaji wake Patrice Evra na Luis Suarez
wakipeana mikono baada ya Suarez kugoma kufuatia kufungiwa Mechi 8 kwa
kumkashifu kibaguzi Evra, amesema ni heri Terry akachukulia kifungo
hicho kuwa ni chepesi na kuacha kukata Rufaa ili kurefusha jambo ambalo
limedumu muda mrefu.
Amesema: “Kuna hatari jambo hili kuibuka
upya kwa sababu limechukua muda mrefu. Yeye amefungiwa Mechi 4 na
Suarez 8 ni bora akaachana nalo na kukubali hizo Mechi 4!”
Pia Ferguson amesema, ingawa hajaongea
na Rio Ferdinand, hategemei Beki wake huyo kuitwa England baada ya Terry
kujiuzulu kuichezea England.
Ferguson ameeleza: “Sidhani ataitwa. Roy
Hodgson alifanya uamuzi wake kabla EURO 2012 na sioni kama atabadilika.
Itakuwa ngumu kwa yeye sasa kubadilika na kumwita Rio.”
na tano juma
No comments:
Post a Comment