Tuesday, July 2, 2013

MAANDAMANO YACHELEWESHA KUTANGAZWA KWA BEI ZA TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA.


SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limechelewa kutangaza bei za tiketi kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 kufuatia maandamano yasiyokoma yanayoendelea nchini Brazil. FIFA ilikuwa imepanga kutoa bei na maelezo kuhusiana na tiketi kwa ajili ya michuano hiyo Jumatatu lakini wameghairisha mpaka Julai 19 mwaka huu. Katibu Mkuu wa FIFA Jerome Valcke amedai kuwa wamefikia uamuzi huo ili kuepusha kuongeza vurugu zaidi za maandamano nchini humo ambapo maelfu ya watu wamekuwa wakiponda hatua ya serikali kutumia fedha nyingi kujenga viwanja na kuboresha miundo mbinu wakati kuna huduma nyingi za kijamii zilitakiwa kupewa kipaumbele. Pamoja na maandamano hayo rais wa FIFA Sepp Blatter alisifu michuano ya Kombe la Sgirikisho iliyomalizika Jumapili kwamba ilikuwa na mafanikio makubwa kimichezo na kuwashukuru wote waliofanikisha hilo.

No comments:

Post a Comment