Tuesday, July 2, 2013

KIJANA MACHACHARI NEYMAR, ALBA KUFANYIWA UPASUAJI.


MSHAMBULIAJI mpya wa Barcelona, Neymar na beki Jordi Alba wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kuondoa mafindofindo Ijumaa na wanatarajiwa kupona baada ya siku 10. Upasuaji huo ulipangwa kufanyika baada ya fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho iliyofanyika jijini Rio de Janeiro Jumapili iliyopita ambapo Brazil iliisambaratisha Hispania kwa mabao 3-0. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo Neymar anatarajiwa kufanyiwa upasuaji huo huko Rio na baadhi ya madaktari wa Barcelona wanakuwepo kusaidia. Wakati Alba mwenye miaka 24 yeye atafanyiwa upasuaji wake siku hiyohiyo lakini katika kliniki iliyopo karibu na jiji la Barcelona na wote wanatarajiwa kupona ndani siku 10 baada ya upasuaji huo.

No comments:

Post a Comment