Monday, February 4, 2013

TPBC YATAKA MABINGWA WATETEE MATAJI NDANI YA MIEZI SITA


Ngowi

KAMISHENI ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), imewataka mabingwa wake wote wawe wametetea mikanda yao ya ubingwa ifikapo tarehe 30 Marchi kwaka huu ili kuepuka kunyanganywa.
Rais wa TPBC, Onesmo Ngowi amesema kwa kipindi kirefu mabingwa kadhaa wamekuwa wanakaa na mikanda bila kuitetea, hivyo wanataka ieleweke kuwa muda wa kukaa na ubingwa wa TPBC ni miezi sita, tu na sio mwaka mmoja.
Amesema bingwa wa kweli anatakiwa awe anafuata sheria, kanuni na taraibu za ubingwa alionao na sio kujiita bingwa wakati hufuati masharti yaliyowekwa.
Amesema katika kipindi hiki cha mwaka 2013 tunawataka mabondia waheshimu sheria za mikataba wanayotiliana sahihi na mapromota. “Tunataka ngumi ziboreshwe kakini pamoja na changamoto nyingi zilizoko, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa wadhamini, mabondia wakiheshimu mikataba yao mchezo wa ngumi utakua na kuwavutia wadhamini,”amesema.
Ngowi ameongeza wanapenda pia kuwaomba wenye mapenzi mema na nchi hii wajitolekeze kwa wingi ili kushirikiana nao, ili kuiweka Tanzania kwenye chati ya dunia kama zilivyo nchi nyingine.

No comments:

Post a Comment