Saturday, January 19, 2013

YANGA YAICHAPA BLACK LEOPARD YA BONDENI 3-2!

YANGA_MJENGO
>>WIMBI LA TEGETE KUCHEKA NA NYAVU LAMPA JINA “MTURUKI!”
>>TFF YAAHIRISHA UCHAGUZI WA VIONGOZI TAFCA!!
Vinara wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga, ambao pia ndio Mabingwa wa Soka Afrika Mashariki na Kati, leo wakicheza Mechi yao ya kwanza tangu warejee kutoka Antalya, Uturuki waliko piga Kambi ya Mazoezi ya Wiki mbili, wameichapa Black Leopard ya Afrika Kusini Bao 3-2 katika Mechi ya Kimataifa ya Kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Yanga 3
-Tegete Dakika ya  32 & 73
-Domayo 63
Black Leopard 2
-Khoza Dakika ya 47
-Rodney  89 
++++++++++++++++++++
Nyota wa Mechi hii alikuwa Jerry Teget aliefungia Yanga Bao 2 akiendeleza wimbi la kufunga aliloanza huko Uturuki katika Mechi za kujipima nguvu kiasi ambacho Washabiki wa Yanga wameanza kumpachika Jina ‘Mturuki!’.
KIKOSI cha YANGA:
1.Ally Mustafa 'Barthez'
2.Mbuyu Twite
3.Oscar Joshua
4.Nadir Haroub 'Cannavaro'
5.Kelvin Yondani
6.Athumani Idd 'Chuji'
7.Kabange Twite
8.Frank Domayo
9.Didier Kavumbagu
10.Jerson Tegete
11.Haruna Niyonzima
Akiba:
1.Said Mohamed
2.Godfrey Taita
3.Stephano Mwasika
4.Ladislaus Mbogo
5.Shadrack Nsajigwa
6.Nurdin Bakari
7.Saimon Msuva
8.Omega Seme
9.Said Bahanuzi
10.George Banda
11.David Luhende
12.Rehani Kibingu
13.Nizar Khalfani
14.Juma Abdul
Release No. 08TFF_LOGO12 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
Januari 19, 2013 
UCHAGUZI WA VIONGOZI TAFCA WAAHIRISHWA
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeahirisha uchaguzi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) uliokuwa ufanyike leo (Januari 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Uchaguzi umeahirishwa kwa vile ulitaka kufanyika bila kuzingatia Katiba ya TAFCA Ibara ya 32(1) na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF Ibara ya 10(6) na 26(2), hivyo Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeahirisha uchaguzi huo kwa vile nafasi zilizoombwa kugombewa na idadi ya waombaji uongozi haikidhi matakwa ya Katiba ya TAFCA.
Pia taratibu za kikanuni ikiwa ni pamoja na kuwaarifu waombaji uongozi ambao hawakukidhi matakwa ya Katiba ya TAFCA hazikukamilika kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Licha ya upungufu huo, TAFCA haikuwasilisha taarifa za mchakato mzima kama ilivyoombwa na TFF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA kuandaa uchaguzi mpya utakaokidhi matakwa ya Kamati ya TAFCA baada ya Uchaguzi Mkuu wa TFF.
TFF inaishauri TAFCA kutumia fursa ya Mkutano Mkuu wa leo (Januari 19 mwaka huu) kujadili mustakabali wa TAFCA kwa kuwa chama hicho kimeshindwa mara mbili kupata idadi ya wagombea wanaokidhi akidi ya Kamati ya Utendaji.
Pia TAFCA haijawahi kufanya mikutano ya Kamati ya Utendaji na Mkutano Mkuu kwa karibu miaka minne.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:

Post a Comment