Monday, January 7, 2013

TOURE APATIWA MATIBABU ABU DHABI.


57247935.jpgMCHEZAJI bora wa mwaka wa Afrika Yaya Toure anapatiwa matibabu ya homa na kifua katika kliniki moja jijini Abu Dhabi ambapo timu ya taifa ya Ivory Coast imeweka kambi kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika. Wachezaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo waliwasili katika mji mkuu huo wa Umoja wa Falme za Kiarabu-UAE Jumamosi wakitokea Ufaransa ambapo walijiunga na maofisa kutoka Abidjan kabla ya safari yao ya mwisho kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya michuano hiyo. Toure hakuonekana katika mazoezi ya timu hiyo jana wakati timu ya madaktari wa timu hiyo wakijaribu kuhakikisha afya ya nyota huyo inatengemaa ingawa haijajulikana ni muda gani atarejea mazoezini na wenzake. Ivory Coast ilianza mazoezi rasmi kwa ajili ya kujiandaa na michuano hiyo katika Uwanja wa Mohammed Bin Zayed chini ya kocha Sabri Lamouchi ambaye ana matumaini makubwa ya kufanya vizuri kutokana na uzoefu wa wachezaji alionao. Kabla ya michuano hiyo Ivory Coast inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri Januari 14 kabla ya kusafiri kuelekea nchini Afrika Kusini siku mbili baadae.

No comments:

Post a Comment