Monday, January 7, 2013

SIMBA FANS YAPASULIWA 7 - 3 NA YANGA FANS!!

>>RIPOTI NA Mpeli Jr Ngonywike [Yanga Team Manager]
YANGA_MTANDAONITimu ya Soka ya Mashabiki wa Yanga wa Mtandaoni, Yanga Facebook Fans, jana January 6, 2013 waliipasua timu ya Simba wa Mtandaoni, Simba Facebook Fans, Mabao 7 - 3 katika mchezo mkali wa Bonanza uliofanyika Viwanja vya Airwing, Ukonga Jijini Dar es Salaam.SIMBA_MTANDAONI
Katika mchezo huo, Yanga waliizidi Simba kila idara hali iliyopelekea mchezo kuwa Mabao 5 - 1 mpaka mapumziko.
Pia katika mchezo huo Simba walipata penati mbili na zote walikosa.
Walipata penati ya kwanza na mpigaji wao akakosa lakini YANGA_MTANDAONI2Refa akaamuru irudiwe na kukosa tena kitu kilichomfanya huyo Mchezaji apandishe hasira na kuamua kumtukana Refa ambae alimzawadia Kadi Nyekundu.
Hata hivyo, Refa huyo alishindwa kumzawadia Kadi Nyekundu Mohamed Mashango wa Simba ambaye alimchezea rafu ya "Boban kwa Yondan" Mchezaji wa Yanga.
Yanga iliwakilishwa na  1.Juma Yakuti, 2. Harrison Chadema 3. Korroso Samwel 4.Mucky's Zayumba, 5.Hassan Msafiri, 6.Stanley Kulola, 7.Khalid Likhanga, 8.Valerian Lihega 9.Ombeni,  10.Osama Yanga na 11.Castor William
Magoli yao yalifungwa na Kulola, Harrison Chadema, Likhanga na Valerian Egitho aliyeingia kipindi cha pili.
Majina ya Simba hayakuweza kupatikana mara moja baada ya kusambaratika na kukataa kutoa ushirikiano baada ya mechi. Walitambulika wawili tu ambao ni Dulla Jane na Mohamed Mashango.
Picha zilizoambatanishwa ni vikosi vya timu zote mbili na jezi walizovaa Yanga zikionyesha kabisa ni Yanga FB Fans

No comments:

Post a Comment