EURO 2020 KUCHEZWA KATIKA MIJI 13 TOFAUTI.
SHIRIKISHO la Soka
barani Ulaya-UEFA limetangaza kuwa michuano ya Ulaya 2020 itaandaliwa
katika nchi 13 huku nusu fainali na fainali za michuano hiyo zitachezwa
katika uwanja mmoja. Katibu
Mkuu wa UEFA Gianni Infantino amesema hakuna uwanja zaidi ya mmoja
utakaotumika katika nchi ambayo itapewa nafasi kuandaa mechi, katika
timu 24 zinazoshiriki michuano hiyo na viwnaja hivyo vitachaguliwa
Septemba mwaka 2014. UEFA
walipiga kura Desemba mwaka jana kuandaa michuano hiyo katika miji
tofauti kuzunguka bara hilo kuliko ilivyokuwa kawaida ambapo michuano
hiyo imekuwa ikiandaliwa na nchi moja au mbili. Shirikisho
limedai kuwa kufanya hivyo kutasaidia nchi ndogo ambazo hazitaweza
kuzihudumia nchi 24 zinazoshiriki michuano hiyo kupata uhondo kwa
kuandaa mojawapo ya mechi. Rais
wa UEFA Michel Platini amesema uwanja utakaotumika kwa ajili ya mechi
za nusu fainali na fainali unatakiwa kuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki
70,000 na mashabiki 60,000 kwa viwanja vya robo fainali huku hatua ya
makundi ambayo itakuwa na mechi 16 viwanja vyake vinatakiwa kuwa na
uwezo wa kuingiza mashabiki 50,000.
No comments:
Post a Comment