Thursday, January 31, 2013

COPA CLASICO: NGOMA NGUMU, SARE 1-1, SI CR7 WALA MESSI WAFUNGAJI!

>>NUSU FAINALI NYINGINE ALHAMISI ATLETICO MADRID v SEVILLA

Barcelona's Cesc Fabregas (L) celebrates scoring
MECHI ya kwanza ya Nusu Fainali ya COPA del REY iliyochezwa Santiago Bernabeu kati ya Mahasimu wakubwa huko Spain, Real Madrid na Barcelona, ilikwisha kwa sare ya Bao 1-1 na wafungaji wa Bao hizo si wale tuliowazoea, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, na Timu itakayotinga Fainali itajulikana huko Nou Camp hapo Februari 27 katika marudiano.Level pegging: Raphael Varane (left) celebrates after scoring the equaliser

COPA del REY
NUSU FAINALI
Jumatano Januari 30
Real Madrid 1 Barcelona 1
Alhamisi Januari 31
[SAA 6 Usiku]
Atletico Madrid v Sevilla
MARUDIANO
Jumatano Februari 27
Sevilla v Atletico Madrid
Barcelona v Real Madrid

Barcelona ndio walitangulia kupata Bao alilofunga Cesc Fabregas Dakika ya 50 baada ya pasi ya Messi.
Real Madrid walisawazisha kwa Bao la kichwa la Beki kutoka Ufaransa Raphael Varane katika Dakika ya 81.
VIKOSI:
Real Madrid (Mfumo 4-2-3-1): Diego López; Essien, Varane, Carvalho, Arbeloa; Khedira, Alonso; Callejón, Özil, Ronaldo; Benzema.
Akiba: Adán, Kaká, Marcelo, Albiol, Modric, Higuaín, Morata.
Barcelona (Mfumo 1-8-1): Pinto; Alves, Piqué, Puyol, Alba; Sergio; Xavi, Fàbregas; Pedro, Messi, Iniesta.
Akiba: Valdés, Villa, Alexis, Thiago, Mascherano, Adriano, Song.

No comments:

Post a Comment