Monday, January 21, 2013

WENGER AHOFIA KUKOSA ULAYA, RVP ASEMA NI SAHIHI KUIKACHA ARSENAL!

>>RVP OLD TRAFFORD: MECHI 28, GOLI 22, BPL NI BORA KWA GOLI 18!!
WENGER_AHIMIZA12BOSI wa Arsenal, Arsene Wenger, mara baada ya kufungwa mara mbili mfululizo na Manchester City na Chelsea kwenye Ligi Kuu England, amekiri wapo hatarini kukosa kucheza Ulaya Msimu ujao lakini Nahodha wake wa zamani, Robin van Persie, ametamka kuwa uamuzi wake kuihama Arsenal na kutua Manchester United ulikuwa ni uamuzi sahihi na wa wakati muafaka.
WENGER
Arsene Wenger amekiri kuwa kipigo cha Bao 2-1 mikononi mwa Chelsea Siku ya Jumapili kimewaacha pagumu katika azma yao ya kufuzu ya kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.
++++++++++++++++++++++
BPL:
MSIMAMO-Timu zaJuu:
1 Man United Mechi 23 Pointi 56
2 Man City  Mechi 23 Pointi 51
3 Chelsea  Mechi 23 Pointi 45
4 Tottenham  Mechi 23 Pointi 41
5 Everton  Mechi 22 Pointi 37
6 Arsenal  Mechi 22 Pointi 34
7 Liverpool  Mechi 23 Pointi 34
8 West Brom Mechi 23 Pointi 34
9 Swansea  Mechi 23 Pointi 33
10 Stoke Mechi 23 Pointi 29
++++++++++++++++++++++
Arsenal wapo Pointi 7 nyuma ya Timu ya nafasi ya nne Tottenham ambayo ndio nafasi ya mwisho kufuzu kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.
Arsenal, wakitoka kufungwa na Man City 2-0 Jumapili Januari 13 na 2-0 na Chelsea Jumapili Januari 20, kumemfanya Wenger aungame: “Tebo ni Tebo. Tumefungwa Gemu mbili Wiki iliyopita na hilo limetuharibia katika Msimamo wetu wa Ligi na ni ngumu kukubali. Hatuweza kupoteza Pointi zaidi kama tunataka tuwe 4 Bora.”
RVP
Robin van Persie ana hakika kuwa ulikuwa wakati muafaka kwake kuihama Arsenal na kutua Manchester United.RVP_in_RED2
Straika huyo hatari ambae ameifungia Man United Mabao 22 katika Mechi 28 huku Bao 18 zikiwa kwenye Ligi Kuu England alihamia Old Trafford mwanzoni mwa Msimu huu.
Van Persie, akifurahia mwanzo mzuri na Man United, ametamka: “Arsenal ni Klabu kubwa na Siku zote nilijisikia vizuri kuwa nao lakini baada ya Miaka 8 nilijisikia nitafute changamoto nyingine. Changamoto hii nimeipata Manchester United. Nimezungukwa na Mabingwa.”
Aliongeza: “Nahisi huu ni wakati muafaka kuhamia hapa. Kila Siku inaniambia nilifanya uamuzi sahihi. Sidhani ingekuwa safi kuja mapema. Nimekuja hapa kupata changamoto kubwa. Hakuna kitu kibaya kuhusu Arsenal. Hakuna Mchezaji mkubwa kuliko Klabu, Arsenal Siku zote itakuwepo kugombea Makombe na kuwa juu. Lakini baada ya Miaka 8 nilikuwa tayari kuondoka na kujaribu kitu kipya.”
Akizungumzia kuhusu hali yake tangu atue Old Trafford, Robin van Persie amesema kila Mtu amekuwa mwema kwake na imemsaidia sana kujisikia nyumbani.
Amesema: “Nasikia furaha. Naona vitu ambavyo sijaviona muda mrefu. Nilipotua Arsenal kwa mara ya kwanza niliona vitu toka kwa Dennis Bergkamp na Thierry Henry ambavyo nilikuwa sijaviona maishani. Sasa naviona vitu hivyo tena na hilo linanifanya niwe na furaha.”

No comments:

Post a Comment