Monday, December 17, 2012

UCHAGUZI WA WANAWAKE TWFA MKOA WA TABORA WAFANYIKA HII LEO KATIKA UKUMBI WA TAASISI



Uchaguzi wa wanawake mkoa wa tabora TWFA umefanyika leo tarehe 17/12/2012 kuanzia saa tatu asubuhi  katika ukumbi wa shule ya taasisi mkoani tabora kusaka viongozi ambao watauwakilisha  mkoa wa tabora ngazi ya mpira wa miguu kwa wanawake.

Uchaguzi huo ulihudhuriwa na wajumbe kumi kutoka  ambao walipiga kura kutoka wilaya ya igunga wajumbe 3.wilaya ya uyui wajumbe 2,wilaya ya nzega wajumbe 3 na wilaya ya tabora mjini wajumbe 2.


Viongozi waliopitishwa katika usaili ni wagombea wanane nao ni ANNA MWINGIRA ambaye alikuwa pekee yake katika  nafasi ya mwenyekiti amepata kura  10 za ndiyo na kura za hapana hakuna,REHEMA ADAM RAJABU naye alikuwa pekee katika  nafasi ya katibu mkuu alipata kura 10 za ndiyo na kura za hapana hakuna,

Wengine ni CHRISTINA WILLIAM FUNGAMEZA ambaye alikuwa anajinafasi pekee yake kwenye nafasi ya katibu msaidizi amepata kura za ndiyo kura 10 na kura za  hapana hakuna ,CATHERINE BUNDALA nafasi ya mkutano mkuu TWFA taifa alikuwa pekee na alijinyakulia kura zote za wajumbe kura 10 za ndiyo na kura za hapana hakuna .

Katika nafasi ya wajumbe wa TWFA mkoa ilikuwa na wagombea wanne na wagombea waliokuwa wanahitajika ni wagombea wanne nao ni  ELEONORA BRUNO LUZIGA aliyepata kura za ndiyo kura 9 na kura za hapana kura 1 ,FATUMA JORAM PELEZI naye alipata kura za ndiyo kura 10 na kura za hapana hakuna ,ZENA MWAKASANGA  alipata kura za ndiyo kura 9 na kura moja ya hapana na nafasi ya mwisho ilikuwa kwa MWANAIDI OMARY katika nafasi ya mjumbe  wa TWFA mkoa wa tabora naye alipata kura 8 za ndiyo na kura 2 za hapana na kupita wote bila mpizani kwani walikuwa wamefikisha idadi iliyokuwa inahitajika ya wajumbe wa TWFA mkoa wa tabora .

Akitangaza matokeo haya mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa TWFA mkoa wa tabora bw. MUSSA NTIMIZI ambaye pia ni mgombea wa uenyekiti wa TAREFA ngazi ya mkoa alisema uchaguzi umefanyika kwa mujibu wa kanuni na taratibu za uchaguzi za TWFA kitaifa .

Wakati huo huo alifafanua kuhusu uchaguzi wa TWFA kitaifa kuwa mikoa iliyotajwa na TFF mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Rukwa, Shinyanga na tabora kuwa haitashiriki katika uchaguzi wa TWFA kitaifa unaotarajia kufanyika desemba 19 mjini morogoro amesema mkoa wa tabora haumo kwani uchaguzi umefanyika.


UCHAGUZI wa chama cha soka la wanawake Tanzania (TWFA) unatarajiwa kufanyika Desemba 19 mwaka huu, kwenye hoteli ya Midland mjini Morogoro huku mikoa sita ikiwa kwenye hati hati ya kutoshiriki.

Kwa mujibu wa taarifa ya TWFA, mikoa hiyo ambayo ni wanachama wa Chama cha Soka ya Wanawake Tanzania (TWFA) hawatashiriki kwa vile hadi sasa haijapokea taarifa za uchaguzi kwenye vyama hivyo.

Vyama hivyo ni vya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Rukwa, Shinyanga na Tabora.

Wagombea wanaotarajiwa kupigiwa kura nafasi ya mwenyekiti kwenye uchaguzi huo ni Isabela Kapera, Joan Minja na Lina Kessy na makamu mwenyekiti ni Rose Kissiwa.

Amina Karuma na Cecilia Mkafum nafasi ya Katibu Mkuu, Zena Chande nafasi ya Mjumbe Mkutano Mkuu wa TFF na Sophia Charles na Triphonia Temba wanaowania ujumbe wa Kamati ya Utendaji

No comments:

Post a Comment