Monday, October 8, 2012

SIMBA NA OLJORO MILIONI 50 HAZIFIKI

Emmanuel Okwi wa Simba akipiga mzito katika mechi ya jana na Olljoro


MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Simba na Oljoro JKT ya Arusha lililochezwa jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 4-1, imeingiza Sh. 46,680,000.
 
 
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo amesema  leo kwamba, watazamaji 8,081 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 8,172,396.61 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 7,120,677.97.
 
 
Amesema mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 120,000, kamishna wa mechi sh. 193,000, waamuzi sh. 210,000, mwamuzi wa akiba (reserve referee) sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
 
 
Amesema umeme sh. 300,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 3,500,000 wakati tiketi ni sh. 3,175,000. Gharama za mchezo sh. 2,724,132.20, uwanja sh. 2,724,132.20, Kamati ya Ligi sh. 2,724,132.20, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,634,479.32 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,089,652.88.
 
 
Wakati huo huo: TFF imetoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama Soka Arusha (KRFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika jana (Oktoba 7 mwaka huu).
Wambura amesema ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ARFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Kigoma.
 
 
Amesema TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya ARFA chini ya uenyekiti wa Khalifa Mgonja ambaye amechaguliwa tena kuongoza chama hicho.
“Uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu mkoani Arusha kwa kuzingatia katiba ya ARFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake. 
 
 Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya ARFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF,”alisema Wambura.
 
 
Aliwataja viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni Khalifa Mgonja (Mwenyekiti), Seif Banka (Makamu Mwenyekiti), Adam Brown (Katibu), Peter Temu (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Omari Walii (Mwakilishi wa Klabu TFF) na Mwalizo Nassoro (Mhazini), wakati Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa katika uchaguzi huo uliofanyika Leganga, Usa River ni Hamisi Issa, Athuman Mhando na Eliwanga Mjema.
 

Alisema bafasi ya Katibu Msaidizi iko wazi na itajazwa katika uchaguzi mdogo utakayofanyika baadaye.

No comments:

Post a Comment