Thursday, October 11, 2012

KOMBE LA DUNIA=ULAYA: Ijumaa Mechi KIBAO!!!


>>MVUTO: Russia v Portugal, Mabingwa Spain ugenini Belarus!!!
>>USHINDANI wa JADI: Wales v Scotland!!
>>SAFI: Serbia v Belgium, Republic of Ireland v Germany!!
>>MTEREMKO: England v San Marino!!
ENGLAND_IN_WEMBLEYIjumaa Ulaya itarindima kwa Mechi za Mchujo za Makundi kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil na zipo Mechi kadhaa zenye ladha tofauti.
Ipo ya Mabingwa watetezi wa Dunia, Spain, kuwa ugenini kucheza na Belarus, ipo ile ya ushindani wa jadi kati ya Wales na Scotland huku ‘Wapwa’ zao England, wakiwa Wembley wakiongozwa na ‘Nahodha mpya’ Wayne Rooney kuwakaribisha ‘vibonde’ San Marino lakini ile inayotegemea kuwa vuta nikuvute ni Russia v Portugal na, pengine, Serbia v Belgium.
Nyingine ambayo huenda ikawa safi ni ile itakayochezwa huko Dublin kati ya Republic of Ireland v Germany na pia ile ya Bulgaria v Denmark na Switzerland v Norway.
Baada ya Raundi hii ya Ijumaa, Mechi nyingine zitachezwa Jumanne Oktoba 16.



RATIBA MECHI ZOTE:
ULAYA-Mechi za Makundi Kombe la Dunia 2014
[Saa za Bongo]
Ijumaa Oktoba 12
1800 Russia v Portugal
1830 Finland v Georgia
1900 Armenia v Italy
1900 Faroe Islands v Sweden
1900 Kazakhstan v Austria
2000 Albania v Iceland
2000 Czech Republic v Malta
2030 Liechtenstein v Lithuania
2030 Turkey v Romania
2100 Belarus v Spain
2100 Bulgaria v Denmark
2100 Moldova v Ukraine
2115 Slovakia v Latvia
2130 Estonia v Hungary
2130 Netherlands v Andorra
2130 Serbia v Belgium
2145 Greece v Bosnia-Hercegovina
2145 Rep of Ireland v Germany
2145 Wales v Scotland
2200 England v San Marino
2200 Luxembourg v Israel
2230 Macedonia v Croatia
2230 Switzerland v Norway
2245 Slovenia v Cyprus



Jumanne Oktoba 16
Albania v Slovenia
Andorra v Estonia
Belarus v Georgia
Belgium v Scotland
Bosnia-Hercegovina v Lithuania
Czech Republic v Bulgaria
Hungary v Turkey
Iceland v Switzerland
Israel v Luxembourg
Latvia v Liechtenstein
Macedonia v Serbia
Portugal v Northern Ireland
Romania v Netherlands
Russia v Azerbaijan
San Marino v Moldova
Slovakia v Greece
Spain v France
Ukraine v Montenegro
2000 Cyprus v Norway
2100 Faroe Islands v Rep of Ireland
2130 Austria v Kazakhstan
2130 Croatia v Wales
2145 Germany v Sweden
2145 Italy v Denmark
2200 Poland v England


FAHAMU:
-ULAYA yapo Makundi 9
-Washindi 9 wa kila Kundi wataingia Fainali moja kwa moja na Washindi wa Pili 8 bora wenye rekodi nzuri dhidi ya Timu zilizomaliza nafasi za Kwanza, Tatu, Nne na Tano kwenye Kundi lao watapelekwa kwenye Droo kupanga Mechi 4 za Mchujo, zitakazochezwa nyumbani na ugenini, ili kupata Timu nne zitakazoingia Fainali.
++++++++++++++++++++++++++++++


MSIMAMO:
KUNDI A
1 Serbia Mechi 2 Pointi 4
2 Belgium 4
3 Croatia 4
4 Scotland
5 FYROM 1
6 Wales 0
+++++++++++++++++++++++



KUNDI B
1 Italy Mechi 2 Pointi 4
2 Bulgaria 4
3 Armenia 3
4 Czech Mechi 1 Pointi 1
5 Denmark 1
6 Malta Mechi 2 Pointi 0
+++++++++++++++++++++++


KUNDI C
1 Germany Mechi 2 Pointi 6
2 Sweden Mechi 1 Pointi 3
3 Rep of Ireland 3
4 Austria 0
5 Kazakhstan Mechi 2 Pointi 0
6 Faroe Island Mechi 1 Pointi 0
+++++++++++++++++++++++


KUNDI D
1 Romania Mechi 2 Pointi 6
2 Netherlands 6
3 Hungary 3
4 Turkey 3
5 Estonia 0
6 Andorra 0
+++++++++++++++++++++++


KUNDI E
1 Switzerland Mechi 2 Pointi 6
2 Iceland 3
3 Albania 3
4 Cyprus 3
5 Norway 3
6 Slovenia 0
+++++++++++++++++++++++


KUNDI F
1 Russia Mechi 2 Pointi 6
2 Portugal 6
3 Luxembourg 1
4 Northern Ireland 1
5 Azerbaijan 1
6 Israel 1
+++++++++++++++++++++++


KUNDI G
1 Bosnia & Herzagovina Mechi 2 Pointi 6
2 Greece 6
3 Slovakia 4
4 Lithuania 1
5 Latvia 0
6 Liechtenstein 0
+++++++++++++++++++++++


KUNDI H
1 Montenegro Mechi 2 Pointi 4
2 England 4
3 Poland  4
4 Ukraine Mechi 1 Pointi 1
5 San Marino 0
6 Moldova Mechi 2 Pointi 0
+++++++++++++++++++++++


KUNDI I
1 France Mechi 2 Pointi 6
2 Spain Mechi 1 Pointi 3
3 Georgia Mechi 2 Pointi 3
4 Finland Mechi 1 Pointi 0
Belarus Mechi 2 Pointi 0

KOMBE la DUNIA: Rooney Kepteni Engand v San Marino!


ENGLAND_IN_WEMBLEY>>UWANJA: Wembley, London SIKU: Ijumaa Oktoba 12 SAA: 4 Usiku [Bongo]
Wayne Rooney ndie atakuwa Nahodha wa England kwenye Mechi ya Kundi H Kanda ya Ulaya la kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia la 2014 huko Brazil dhidi ya San Marino itakayochezwa Uwanja wa Wembley mbele ya Mashabiki 90,000.
Rooney amepewa wadhifa huo kufuatia kutokuwepo kwa Nahodha Steven Gerrard na Msaidizi wake Frank Lampard kwa vile wote ni majeruhi.
+++++++++++++++++
REKODI ya SAN MARINO:
MECHI:
-Wamecheza: 114
-Ushindi: 1
-Sare: 5
-KUFUNGWA: 108
MAGOLI:
-Kufunga: 19
-Kufungwa: 473
+++++++++++++++++
Rooney, ambae ameichezea England mara 76, amesema : “Hiki ni kitu ambacho nina fahari nacho kubwa. Ni changamoto kubwa kwangu na nimefurahi. Tunategemea kumaliza Siku kwa ushindi.”
Ingawa England wanacheza na San Marino, Nchi ndogo Barani Ulaya iliyozungukwa na Italy na ambayo kwenye Listi ya FIFA ya Ubora Duniani wapo nafasi ya 207, ambayo ni ya mwisho, Rooney amesema Wachezaji hawatabweteka.
Amesema: “Wachezaji hawataki kuwaangusha Mashabiki. Tangu nianze kuichezea England, Mashabiki wamekuwa wazuri sana. Wanatufuata Dunia nzima. Tunatazamia Mechi nzuri na hatutawaangusha Mashabiki!”
+++++++++++++++++++++++

MSIMAMO:
KUNDI H
1 Montenegro Mechi 2 Pointi 4
2 England Mechi 2 Pointi 4
3 Poland Mechi 2 Pointi 4
4 Ukraine Mechi 1 Pointi 1
5 San Marino Mechi 1 Pointi 0
6 Moldova Mechi 2 Pointi 0
+++++++++++++++++++++++
Huko nyuma, Novemba 2009, Rooney aliwahi kuwa Nahodha wa England ilipofungwa na Brazil bao 1-0 katika Mechi iliyochezwa Doha, Qatar.
 

AFCON 2013: Liberia waahidiwa Dola Laki 3 wakiibwaga Nigeria Jumamosi!


>>ETO’O apigiwa goti kuiokoa Cameroun ifute kipigo 2-0 toka ‘Taifa Dogo’ Cape Verde!!
AFCON_2013-NORMALNchini Liberia imepita Harambee kubwa kuhakikisha Nchi hiyo inaitoa Nigeria kwenye Mechi ya marudiano kuwania kutinga Fainali za Kombe la Mataifa Januari 2013 huko Afrika Kusini, AFCON 2013, baada ya Wachezaji kuahidiwa kitita kinono cha Dola 300,000 lakini Mechi hiyo ya marudiano itachezwa huko Calabar, Nigeria huku matokeo ya Mechi ya kwanza yakiwa ni 2-2.
Pamoja na Mechi hiyo ya Nigeria na Liberia zipo Mechi nyingine 14 za marudiano ili kupata Timu 15 zitakazoungana na Wenyeji Afrika Kusini kucheza AFCON 2013 Mwezi Januari 2013.
Mbali ya Mechi hii, Mechi nyingine tamu ni ile itakayochezwa huko Yaounde, Cameroun ambako Kisiwa kidogo cha Cape Verde tayari washaicharaza Cameroun bao 2-0 na Taifa hilo kubwa limebidi limpigie magoti Supastaa Samuel Eto’o aje awaokoe baada ya yeye kufungiwa na kususa kuichezea Nchi yake alipofunguliwa.
Nyingine tamu ni marudiano ya Mabingwa wa Afrika, Zambia, na Uganda huko Kampala huku Zambia wakiwa mbele kwa bao 1-0.
++++++++++++++++++++++++++++++

AFCON 2013=Kombe la Mataifa ya Afrika
[Fainali Afrika Kusini-Januari 2013]
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi za kwanza]
Jumamosi Oktoba 13

Malawi v Ghana [0-2]
Botswana v Mali [0-3]
Nigeria v Liberia [2-2]
Uganda v Zambia [0-1]
E.Guinea v Congo DR [0-4]
Senegal v Cote d'Ivoire [2-4]
Tunisia v Sierra Leone [2-2]
Morocco v Mozambique [0-2]


Jumapili Oktoba 14
Algeria v Libya [1-0]
Cameroon v Cape Verde [0-2]
Togo v Gabon [1-1]
Angola v Zimbabwe [1-3]
Niger v Guinea [0-1]
Ethiopia v Sudan [3-5]
Burkina Faso v Central African Republic [0-1]
FAHAMU: Washindi 15 wa Mechi hizi watajumuika na Wenyeji Afrika Kusini kwenye Fainali zitakazochezwa Afrika Kusini Januari 2013.
++++++++++++++++++++++++++++++
 

Ferguson aokota ‘Almasi’, Fellaini NJE, Sagna NDANI!


Habari toka huko Old Trafford zinasema Sir Alex Ferguson anaamini uamuzi wake wa kutumia Mfumo wa umbo la Almasi kwenye Kiungo cha Timu yake utaleta mafanikio Msimu huu wakati huko Liverpool, Klabuni Everton, kuna majonzi baada ya kupokea taarifa kuwa Kiungo wao na Mpiganaji mahiri, Marouane Fellaini, ameumia goti lakini toka Emirates kuna habari njema kuwa Fulbeki wao mzoefu, Bacary Sagna, yuko kwenye mazoezi makali akijifua ili arudi dimbani haraka.
Man United na Almasi
MAN_UNITED_ALMASISir Alex Ferguson ameubadilisha Mfumo wa uchezaji wa Timu yake na sasa, badala ya kutumia Mawinga wawili kama ilivyozoeleka, hutumia mtindo wa kuwa na umbo la Almasi kwenye Kiungo ambao husimama Mtu 4 wakiwa mbele ya Mabeki wanne na nyuma ya Mastraika wawili.
Mfumo huo ambao walianza kuutumia kwenye Mechi ya CAPITAL ONE CUP walipoifunga Newcastle, ukarudiwa ugenini kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI walipoifunga CFR Cluj bao 2-1 na majuzi ukaendelea tena huko St James Park walipoitwanga Newcastle bao 3-0 huku hiyo ‘Almasi’ ikiwa na Michael Carrick anaesimama mbele ya Mabeki wanne, Shinji Kagawa na Tom Cleverly wakicheza mbele ya Carrick na kubadilishana nafasi kulian na kushoto huku mbele yao akisimama Wayne Rooney ambae huwa nyuma tu ya Mastraika wawili Robin van Persie na Danny Welbeck.
Ferguson amesema kwenye Mechi na Newcastle Cleverley, Kagawa, Rooney na Carrick walimudu vyema kwenye Kiungo na ulikwa uamuzi wa busara kuutumia Mfumo huo mpya.
Fellaini aumia!
Kiungo wa Everton, Marouane Fellaini, amejitoa kwenye Kikosi cha Belgium ambacho kinajitayarisha kwa Mechi za Ijumaa na Jummane ijayo za Kombe la Dunia dhidi ya Serbia na Scotland baada ya kuumia goti.
Fellaini alipata maumivu hayo Jumamosi iliyopita Everton ilipocheza na Wigan kwenye Mechi ya Ligi Kuu England na Everton imesema haijulikani atakuwa nje kwa muda gani.
Hata hivyo Kambi ya Belgium imesema Mchezaji huyo atakuwa nje kwa Wiki 3 na hivyo kuzikosa Mechi za Everton dhidi ya QPR hapo Oktoba 21 na ile Dabi ya Liverpool dhidi ya Mahasimu wao Liverpool hapo Oktoba 28.
Kumkosa Fellaini ni pigo kubwa kwa Everton ambao wameanza vyema Msimu huu na wapo nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu baada ya kushinda Mechi 4, sare 2 na kufungwa moja tu.
Bacary Sagna
Bacary Sagna, ambae amepona baada ya kuvunjika mguu Mwezi Mei katika Mechi na Norwich, hataharakishwa kurudi Uwanjani bali ataimarishwa pole pole ili arudi na nguvu zaidi.
Sagna, ambae ameumia vibaya mara mbili ndani ya Mwaka mmoja, amesema yuko tayari kucheza ila bado anajiimarisha zaidi.
Wakati alipokosekana Sagna nafasi yake ilichukuliwa na Chipukizi Carl Jenkinson ambae amecheza vyema mno na Sagna amekiri hilo kwa kusema: “Amecheza vizuri sana na amejifunza mengi. Ametulia na ni Beki mzuri.”

No comments:

Post a Comment