Monday, October 1, 2012

UEFA CHAMPIONZ LIGI: Mabingwa Chelsea, Man United ugenini Jumanne!

Jumatatu, 01 Oktoba 2012 20:50
 
RATIBA:
Jumanne Oktoba 2
[Mechi zote Saa 3 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
Juventus v FC Shakhtar Donetsk
FC Nordsjælland v Chelsea FC
Valencia CF v LOSC Lille
FC BATE Borisov v FC Bayern München
SL Benfica v FC Barcelona
FC Spartak Moskva v Celtic FC [SAA 1 Usiku]
CFR 1907 Cluj v Manchester United FC
Galatasaray A.S. v SC Braga
TAARIFA:
MAN_UNITED-ANDO_RVP_SHINJI_EVRAJumanne Usiku ni MECHI DEI 2 ya Mashindano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na Timu za England ambazo zitakuwa dimbani, Mabingwa Chelsea na Manchester United, zote zitacheza ugenini kwa Chelsea kuwa huko Denmark kuivaa Timu mpya FC Nordsjælland inayotoka Mji wa Farum wenye Wakazi 18,000 tu na Manchester United kucheza huko Bucharest, Romania na Timu yenye uzoefu CFR 1907 Cluj.
Wakati Manchester United walianza MECHI DEI 1 kwa ushindi katika Mechi yao ya Kundi H kwa kuitungua Galatasaray ya Uturuki kwa Bao 1-0, Mabingwa Chelsea wakiwa nyumbani Stamford Bridge waliutupa uongozi wa bao 2-0 na kwenda sare na Mabingwa wa Italy kwa bao 2-2.
Man United
Manchester United imesafiri kwenda Romania bila ya Wachezaji Michael Carrick, Ryan Giggs, Paul Scholes na Antonio Valencia.
Ingawa inajulikana Valencia alikuwa na maumivu lakini kuachwa kwa Giggs, Scholes na Carrick kumekuwa hamna maelezo ingawa Wachezaji wote hao walicheza Mechi ya Jumamosi waliyofungwa 3-2 na Tottenham.
Miongoni mwa Kikosi cha Wachezaji 21 waliokuwemo kwenye msafara ni Chipukizi kina Michael Keane, Scott Wootton, Jesse Lingard, Nick Powell na Ryan Tunnicliffe ambao wanaungana na Darren Fletcher ambae ni hivi karibuni tu amerejea Uwanjani baada ya kuwa nje kwa Miezi 10.
Kikosi kamili:
Man United: De Gea, Lindegaard; Büttner, Evans, Evra, Ferdinand, M.Keane, Rafael, Wootton; Anderson, Cleverley, Fletcher, Lingard, Nani, Powell, Tunnicliffe; Hernandez, Kagawa, Rooney, van Persie, Welbeck.CHELSEA_ULAYA_2012
Chelsea huko Denmark
Hii ni Mechi ya kwanza kwa Chelsea kucheza ugenini kwenye hatua ya Makundi baada ya kucheza Mechi ya kwanza nyumbani ya Kundi E Stamford Bridge na kuutupa uongozi wa bao 2-0 na kwenda sare na Mabingwa wa Italy kwa bao 2-2.
Safari hii watakuwa Uwanja wa Parken Mjini Denmark kucheza na Timu ngeni na ndogo, FC Nordsjælland ambayo inatoka Mji mdogo wa Farum wenye Wakazi 18,000 tu.
FC Nordsjælland walifungwa Mechi yao ya kwanza bao 2-0 ugenini na Shakhtar Donetsk lakini pia Chelsea wana rekodi dhaifu kwa Mechi za ugenini kwani Msimu uliopita waliotwaa Ubingwa wa Ulaya kwenye hatua ya Makundi walitoka sare na Valencia na Genk na kufungwa na Bayer Leverkusen.
RATIBA:
Jumatano Oktoba 3
[Mechi zote Saa 3 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
FC Dynamo Kyiv v GNK Dinamo
FC Porto v Paris Saint-Germain FC
FC Schalke 04 v Montpellier Hérault SC
Arsenal FC v Olympiacos FC
RSC Anderlecht v Málaga CF
FC Zenit St. Petersburg v AC Milan [SAA 1 Usiku]
Manchester City FC v Borussia Dortmund
AFC Ajax v Real Madrid CF

No comments:

Post a Comment