TOKA TFF LEO: SIMBA vs TANZANIA PRISONS Vikosi vya leo vyatajwa!!
Jumamosi, 29 Septemba 2012 16:12
>> VIINGILIO MECHI YA YANGA, SIMBA SH. 5,000

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Septemba 29, 2012
KIINGILIO MECHI YA YANGA, SIMBA SH. 5,000
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya
Yanga na Simba itakayochezwa Jumatano (Oktoba 3 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani
ambavyo ni 19,648 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji
60,000.
Mechi hiyo namba 80 ya Ligi Kuu ya
Vodacom itachezwa kwenye uwanja huo kuanzia saa 11 kamili jioni.
Watazamaji watakaotaka kuona mechi hiyo wakiwa wameketi kwenye viti vya
rangi ya bluu ambavyo ni 17,045 watalipa sh. 7,000 kwa tiketi moja.
Viingilio vingine kwenye mechi hiyo ni
sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 wakati VIP C
inayochukua watazamaji 4,060 itakuwa sh. 15,000. Kwa upande wa VIP B
tiketi ni sh. 20,000 na VIP A yenye watazamaji 748 tu kiingilio kitakuwa
sh. 30,000.
SIMBA vs TANZANIA PRISONS LINE UPS
Timu za Simba na Tanzania Prisons
zinapambana jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11
kamili jioni. Tayari makocha wa timu zote mbili Jumanne Charles
(Tanzania Prisons) na Circo Milovan (Simba) wameshataja vikosi vyao.
Simba: Tanzania Prisons:
01.Juma Kaseja (c) 18.David Abdallah
02.Nassoro Masoud 03.Aziz Sibo
17.Amir Maftah 05.Laurian Mpalile
15.Shomari Kapombe 16.Lugano Mwangama (c)
24.Juma Nyoso 15.David Mwantika
14.Mwinyi Kazimoto 13.Khalid Fupi
28.Amri Kiemba 07.Misango Magai
08.Ramadhan Chombo 12.Fred Chudu
19.Edward Christopher 14.Elias Maguri
10.Felix Sunzu 17.Peter Michael
16.Mrisho Ngasa 19.John Matei
Wachezaji wa akiba;
22.Wilbert Mweta 01.Daudi Mwasongwe
23.Paul Ngalema 04.Jumanne Elfadhili
20.Jonas Mkude 09.Sino Augustino
12.Salim Kinje 22.Julius Kwaga
04.Komanbil Keita 08.Henry Mwalugala
13.Daniel Akuffor 11.Hamisi Ally
05.Pascal Ochieng 23.Jeremiah Juma
Refa: Paul Soleji (Mwanza)
Mwamuzi Msaidizi 1: Jesse Erasmo (Morogoro)
Mwamuzi Msaidizi 2: Mwarabu Mumba (Morogoro)
Mwamuzi wa Akiba: Israel Nkongo (Dar es Salaam
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)na tano juma
No comments:
Post a Comment