Kibadeni wa tatu kutoka kushoto enzi zake akiwa na simba mwaka 1970 akiwa na simba
Nami nakuletea historia fupi ya kuelekea mpambano wa watani wa jadi simba na yanga kama darby kwa tanzania tujikumbushe kidogo kwa ufupi historia ya timu hizi na baadhi ya wachezaji enzi za miaka 1991.Said Sued 'Scud', alifunga bao pekee la ushindi kwenye mechi
ya watani wa jadi, akiwa anaichezea Yanga alitikisa nyavu za Simba dakika ya
saba katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara enzi zile na , sasa Ligi Kuu mwezi Mei
18, mwaka 1991.
Huo ukiwa msimu wake wa kwanza kwenye klabu hiyo, hakika
ilikuwa furaha kubwa kwake, kwani tangu hapo aliaminika na kuwa mchezaji wa
kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga.
Chipukizi huyo wa wakati huo, alipata ngekewa ya kuifunga
tena Simba katika mchezo uliofuata wa marudiano wa ligi baina ya watani wa
jadi, likiwa pia bao pekee la ushindi Agosti 31, mwaka huo huo 1991, jambo
ambalo lilimfanya awe maarufu zaidi.
Lakini katika mastaajabu ya wengi, Scud hakurejea kwenye
kikosi cha Yanga cha mwaka 2002 na huo ukawa mwisho wa umaarufu wake kwenye
soka ya Tanzania.
Kama wapo wanaodhani Scud alifanya kubwa sana katika historia
ya watani wa jadi, watakuwa wapo mbali kabisa na ukweli, kwani Kibadeni,
maarufu kama Chifu Mputa ama King, au Ndululu kama walivyokuwa wakimuita
Wakenya, anaweza kusimama na kusema ana kubwa la kujivunia katika historia ya
mechi baina ya Simba na Yanga ambalo hadi kitabu hiki kinaingia sokoni lilikuwa
halijavunjwa.
Abdallah Kibadeni ndiye mchezaji pekee hadi sasa aliyeweza
kufunga mabao
matatu peke yake katika mchezo mmoja kwenye mechi za watani wa
jadi katika Ligi.
Hiyo ilikuwa ni Julai 19, mwaka 1977 katika Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam, sasa Uwanja wa Uhuru, wakati Yanga ilipotandikwa 6-0 na Simba.
Siku hiyo, Kibadeni alitikisa nyavu za Yanga katika dakika za
10, 42 na 89, wakati mabao mengine ya Wekundu wa Msimbazi, yalitiwa kimiani na
Jumanne Hassan 'Masimenti' dakika ya 60 na 73 na jingine Selemani Sanga wa
Yanga alijifunga mwenyewe dakika ya 20 katika harakati za kuokoa krosi ya
Ezekiel Greyson 'Jujuman'.
Hivyo siku hiyo mbali na Simba kushangilia kulipa kisasi cha
kulala 5-0 kwa Yanga, Juni Mosi mwaka 1968, Kibadeni alikuwa ana sherehe
binafsi za kutumbukiza tatu peke yake kwenye mechi baina ya watani hao, jambo
ambalo liliwashinda wengi kabla yake kati ya waliowahi kuvaa jezi za Simba au
Yanga.
Hakuna cha Sunday Manara 'Computer' wala Maulid Dilunga
'Mexico' aliyewahi kufanya hivyo zaidi ya King Kibadeni pekee. Sasa baada ya
miaka 35 tangu Kibadeni awaokoteshe Yanga mipira nyavuni mara tatu, miamba hiyo
inakutana tena Jumatano ya wiki ijayo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, je
rekodi hiyo itavunjwa? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.kwani ikumbukwe kuwa yanga alishawahi kutandikwa bao 5-0 katika mechi ya mwisho ya ligi kuu vodacom tanzania bara mwaka jana na simba kutwaa ubingwa huo kwa kufikisha pointi 62 na kufuatiwa na azam ambao walijikusanyia pointi 59 na yanga kuwa wa tatu kwa pointi 49..kikosi cha simba mwisho kuifunga yanga mwaka jana 2011 kilikuwa juma kaseja,said nasor cholo,amir maftah,juma nyoso,kelvin yondan,patrick mafisango,salum machaku,mwinyi kazimotto,felix sunzu,haroun moshi boban,na emmanuel okwi,,,,tujiulize kuelekea katika mpambano huo tutarajie mambo gani kwa watani wa jadi hawa?na mwandishi wetu tano juma |
No comments:
Post a Comment