AVB hahofii Spurs kutua Old Trafford kuivaa Man Utd!
Jumamosi, 29 Septemba 2012 15:25
>>SPURS haijashinda OT tangu 1989, akumbushwa kichapo hapo akiwa na Chelsea!!

Akihojiwa kuhusu tuhuma za hivi karibuni
toka kwa Meneja wa Manchester City Roberto Mancini ambae alikwaruzana
na Meneja wa Aston Villa Paul Lambert na kudai Mameneja wengine huogopa
kusema kitu wakiwa Old Trafford, Villas-Boas, mwenye Miaka 34, alisema:
“Sina tatizo kuongea chochote nikiwa Old Trafford!”

Alipobanwa aeleza ikiwa Man United
wanapendelewa wakicheza Uwanja wao Old Trafford, Villas-Boas alisema:
“Ni swali zuri lakini ni swali ambalo Nchi hii huwezi kulijibu. Mwaka
jana nilipigwa Faini kubwa kwa kusema kitu kama hiki!”
Leo Andre Villas-Boas anaiongoza
Tottenham kucheza Old Trafford ambayo haijashinda Uwanja huo tangu Mwaka
1989 na yeye mwenyewe, akiiongoza Chelsea Msimu uliopita, alijikuta
akipigwa 3-1 na Man United.
Lakini mwenyewe amesema: “Tutakwenda
huko kucheza Soka la wazi. Hivi ndivyo ninavyopenda na kutaka Timu yangu
icheze. Ni ngumu kucheza Old Trafford lakini tunataka kufanya kitu
kitakachopa tupa fahari na kufuta hizi takwimu mbaya!”
Akielezea muda wake mfupi wa Miezi 9
alipokuwa na Chelsea na kufukuzwa Mwezi Machi Mwaka huu, Villas-Boas
amekiri zama za sasa haiwezekani Meneja akawa na himaya ndefu kama vile
Sir Alex Ferguson na Manchester United na Arsene Wenger na Arsenal.
Villas-Boas amesema: “Kwa sasa hilo
haliwezekani! Nilitegemea Rafa Benitez atapata himaya ndefu Liverpool
lakini haikutokea [Alifukuzwa baada ya Miaka 6]”
Alimalizia: “Ni ngumu Nchi hii! David Moyes wa Everton anakaribia historia hiyo lakini huwezi kupata mifano mingi kama hiyo.” na tano juma
No comments:
Post a Comment