Saturday, January 19, 2013

BPL: LIVERPOOL YANYUKA 5-0, MAN CITY YAIKARIBIA UNITED 4 NYUMA!!

BPL_LOGO
BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Januari 19
Liverpool 5 Norwich 0
Man City 2 Fulham 0
Newcastle 1 Reading 2
Swansea 3 Stoke 1
West Ham 1 QPR 1
Wigan 2 Sunderland 3
[SAA 2 na Nusu Usiku]
West Brom v Aston Villa

LIVERPOOL 5 NORWICH 0
Wakianza pamoja katika Mechi yao ya kwanza, Mastraika wa Liverpool Luis Suarez na Daniel Sturridge, kila mmoja alifunga Bao moja Liverpool walipoibamiza Norwich Bao 5-0 Uwanjani Anfield.

MAGOLI:
Liverpool 5
-Henderson Dakika ya 26
-Suarez 36
-Sturridge 59
-Gerrard 66
-R Bennett 74 (Kajifunga mwenyewe)

Kipigo cha Liverpool kwa Norwich kilianza kwa Bao lililotokana na Shuti kali la Jordan Henderson.
VIKOSI:
Liverpool: Jones, Wisdom, Carragher, Agger, Johnson, Gerrard, Lucas, Henderson, Suarez, Sturridge, Downing
Akiba: Gulacsi, Allen, Borini, Sterling, Shelvey, Skrtel, Robinson.
Norwich: Bunn, Martin, Ryan Bennett, Turner, Garrido, Elliott Bennett, Johnson, Howson, Snodgrass, Tettey, Holt
Akiba: Rudd, Jackson, Pilkington, Hoolahan, Barnett, Tierney, Kane.
Refa: Michael Oliver
WEST HAM 1 QPR 1
Bao la Dakika ya 14 la Mchezaji mpya Loic Remy liliwapa matumaini Timu ya mkiani Queens Park Rangers lakini Joe Cole aliwakatili katika Dakika ya 68 aliposawazisha kwa West Ham na Mechi kwisha 1-1.
VIKOSI:
West Ham: Jaaskelainen, Demel, Tomkins, Reid, O'Brien, Noble, Diame, Joe Cole, Nolan, Jarvis, Chamakh
Akiba: Spiegel, Carlton Cole, Collison, Vaz Te, Taylor, Diarra, Potts.
QPR: Julio Cesar, Onuoha, Nelsen, Hill, Da Silva, Derry, Mbia, Mackie, Taarabt, Wright-Phillips, Remy
Akiba: Green, Traore, Ferdinand, Park, Hoilett, Faurlin, Bothroyd.
Refa: Howard Webb
SWANSEA 3 STOKE 1
Bao mbili za Jonathan de Guzman na moja la Ben Davies limewapa Swansea City ushindi wa 3-1 walipocheza na Stoke City.
Bao zote zilifungwa Kipindi cha Pili.

Swansea 3
-Davies Dakika ya 49
-De Guzman 57 & 80
Stoke 1
-Owen Dakika ya 90

Michael Owen, alieingizwa kutoka Benchi, ndie alifunga Bao pekee kwa Stoka hilo likiwa Bao lake la kwanza kwa Stoke na la 150 katika Ligi Kuu England.
VIKOSI:
Swansea: Vorm, Rangel, Monk, Williams, Davies, Hernandez, de Guzman, Ki, Michu, Routledge, Shechter
Akiba: Tremmel, Bartley, Britton, Graham, Dyer, Lamah, Tiendalli.
Stoke: Begovic, Whitehead, Huth, Shawcross, Cameron, Etherington, Whelan, Nzonzi, Adam, Walters, Crouch
Akiba: Sorensen, Palacios, Jones, Owen, Upson, Kightly, Jerome.
Refa: Mike Dean
MAN CITY 2 FULHAM 0
Bao mbili za David Silva, moja baada ya Sekunde 95 na jingnine katika Dakika ya 69, zimewapa Manchester City ushindi wa Bao 2 dhidi ya Fulham na kuwafikisha Pointi 4 nyuma ya Vinara Manchester United ambao Jumapili wako ugenini White Hart Lane kucheza na Tottenham.
VIKOSI:
Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Clichy, Barry, Javi Garcia, Milner, Tevez, Silva, Dzeko
Akiba: Pantilimon, Lescott, Nasri, Kolarov, Aguero, Rodwell, Balotelli.
Fulham: Schwarzer, Riether, Hughes, Hangeland, Richardson, Duff, Karagounis, Sidwell, Dejagah, Ruiz, Berbatov
Akiba: Etheridge, Senderos, Baird, Petric, Briggs, Rodallega, Kacaniklic.
Refa: Jon Moss
NEWCASTLE 1 READING 2
Adam Le Fondre alitoka Benchi na kupachika Bao mbili ndani ya Dakika 6 na kuupindua uondozi wa Bao 1-0 wa Necastle na kuipa Reading ushindi wa 2-1 uliowang’oa toka Timu 3 za mkiani.

MAGOLI:
Newcastle 1
-Cabaye Dakika ya 35
Reading 2
-Le Fondre Dakika ya 71 & 77

Newcastle ndio waliotangulia kufunga kwa frikiki safi ya Yohan Cabaye.
VIKOSI:
Newcastle: Krul, Coloccini, Santon, Debuchy, Williamson, Cabaye, Anita, Cisse, Marveaux, Gutierrez, Shola Ameobi
Akiba: Elliot, Perch, Steven Taylor, Bigirimana, Obertan, Sammy Ameobi, Ranger.
Reading: Federici, Pearce, Mariappa, Harte, Kelly, Leigertwood, McCleary, Kebe, McAnuff, Guthrie, Pogrebnyak
Akiba: Taylor, Gunter, Morrison, Akpan, Karacan, Le Fondre, Hunt.
Refa: Andre Marriner
WIGAN 2 SUNDERLAND 3
Steven Fletcher ameweka historia ya kuifunga Wigan Bao 6 katika Mechi 7 za Ligi Kuu England dhidi yao leo alipofunga Bao mbili zilizowasaidia Sunderland kutoka nyuma kwa Bao moja na kushinda 3-2.

MAGOLI:
Wigan 2
-Vaughan Dakika ya 4 (Kajifunga mwenyewe)
-Henriquez 79
Sunderland 3
-Gardner 17 (Penati)
-Fletcher 20 & 42
+++++++++++++++++++++++
Sunderland walijikuta wako nyuma katika Dakika ya 4 baada ya Shuti la Ronnie Stam kutumbukizwa wavuni na David Vaughan lakini Craig Gardner akasawazisha kwa Penati baada ya James McCarthy kuunawa mpira na Steven Fletcher kupiga Bao mbili zilizowafanya Sunderland wawe 3-1 mbele.
Straika Chipukizi wa Man United, Angelo Henriquez, ambae yuko Wigan kwa Mkopo aliwafungia Bao la Pili.
VIKOSI:
Wigan: Al Habsi, Boyce, Caldwell, Figueroa, Stam, McCarthy, McArthur, Beausejour, Gomez, Di Santo, Maloney
Akiba: Robles, Jones, Henriquez, McManaman, Espinoza, Boselli, Golobart.
Sunderland: Mignolet, Gardner, O'Shea, Bramble, Colback, Larsson, N'Diaye, Vaughan, Johnson, Fletcher, Sessegnon
Akiba: Westwood, Bardsley, Wickham, McFadden, Kilgallon, McClean, Elmohamady.
Refa: Anthony Taylor

BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA:
Jumapili Januari 20
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Chelsea v Arsenal
[SAA 1 Usiku]
Tottenham v Man United
Jumatatu Januari 21
[SAA 5 Usiku]
Southampton v Everton

No comments:

Post a Comment