Wednesday, October 3, 2012

Zambia, Cameroon zaomba kucheza CHALENJI CUP

Mabingwa wa Afrika, Zambia, wameomba kushiriki Mashindano ya Mwaka huu ya CHALENJI CUP, Tusker CECAFA Cup, ambayo ndio hutoa Nchi Bingwa wa Afrika Mashariki na Kati ambayo yatafanyika huko Kampala, Uganda kati ya Novemba 27 na Desemba 12.


Nchi nyingine 4 ambazo pia zimeomba kushiriki ni Cameroon, Malawi, Zimbabwe na Cote D'Ivoire.
Habari za maombi ya Nchi hizo zimethibitishwa na Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicolas Musonye, ambae amesema ushiriki wa Nchi hizo utategemea uamuzi wa CECAFA ambao utatolewa baada ya Mkutano wao.


Mkutano huo wa CECAFA unategemewa kufanyika Wikiendi ijayo baada ya Mechi za Raundi ya Mwisho ya Mtoano ya AFCON 2013.


Mwaka jana, Malawi na Zimbabwe, zilishiriki kama Wageni waalikwa.
Hata hivyo, Musonye pia amesema ushiriki wa Nchi hizo ambao si Wanachama wa CECAFA utategemea pia ikiwa kama kutakuwa na Nchi Mwanachama ambayo itajitoa ingawa hadi sasa Nchi zote 12 Wanachama wa CECAFA zimethibitisha ushiriki wao.


Droo ya kupanga Ratiba ya Michuano hiyo itafanyika huko Kampala hapo November 8.
Bingwa Mtetezi wa CHALENJI CUP ni Uganda ambao pia ndio Nchi iliyotwaa Ubingwa huo mara 12 ambazo ni nyingi kupita Nchi nyingine.
 

LISTI ya FIFA UBORA DUNIANI: Spain palepale Nambari Wani, Bongo palepale 132!


@@@@KUMI BORA, Colombia yatinga, yapanda Nafasi 13!!
@@@@BRAZIL Washuka 2, Wapo wa 14!!
FIFA_LOGO_BESTSpain, ambao ndio Mabingwa wa Ulaya na Dunia, wameendelea kushika Nambari Wani kwenye Listi ya FIFA/Coca Cola ya Ubora Duniani iliyotolewa leo huku Tanzania ikibakia Nambari 132 na kwenye Kumi Bora Portugal imepanda na kushika Namba 3, England imeporomoka na sasa ipo nafasi ya 5 kutoka Namba 3.


Barani Afrika Ivory Coast ndio wapo juu na wapo nafasi ya 16 ambayo ni ile ile kama ilivyokuwa Mwezi uliopita.


Colombia wameingia Kumi Bora baada ya kupanda nafasi 13 huku Denmark na Croatia zikiporomoka kutoka Kumi Bora.


Brazil, Mabingwa wa Dunia mara 5, wameporomoka nafasi mbili na sasa wapo nafasi ya 14.
Listi nyingine mpya itatolewa Novemba 7.


KUMI BORA:
1 Spain
2 Germany
3 Portugal
4 Argentina
5 England
6 Netherlands
7 Uruguay
8 Italy
9 Colombia
10 Greece
 

BATE Borisov yaifumua Bayern, yatikisa Ulaya!!!


@@@@REKODI: Juve sare ya 8 mfululizo!!
@@@@REKODI: Celtic wavunja rekodi ya kutoshinda Mechi 20 ugenini!


MATOKEO:
Jumanne Oktoba 2
Juventus 1 Shakhtar Donetsk 1
FC Nordsjælland 0 Chelsea 4
Valencia 2 LOSC Lille 0
FC BATE Borisov 3 FC Bayern München 1
SL Benfica 0 FC Barcelona 2
FC Spartak Moskva 2 Celtic 3
CFR 1907 Cluj 1 Manchester United 2
Galatasaray 0 Braga 2
 ++++++++++++++++++++++++++++++
RVP_ROONEY_CLEVERLYKlabu ya Belarus, BATE Borisov, jana ilileta mtikiso mkubwa huko Ulaya kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa kuwatandika Bayern Munich, ambao Msimu uliopita walitinga Fainali ya michuano hii na kubwagwa kwa Penati na Chelsea, kwa kuwatandika bao 3-1 katika Mechi ya Kundi F.


Huku Bayern Munich wakitolewa nishai, Vigogo wengine wote wa Ulaya, Mabingwa Chelsea, Barcelona na Manchester United walishinda lakini Juventus walitoka sare 1-1 na Shakhtar Donetsk.


Chelsea, wakicheza ugenini huko Denmark, waliichapa Timu mpya FC Nordsjaelland 4-0, Barcelona, pia wakiwa ugenini, waliifunga Benfica 2-0 lakini walipata mkosi pale Nahodha wao Carles Puyol alipokimbizwa Hospitali baada ya kuteguka kiwiko cha mkono na Sergio Busquets kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.


Nao Manchester United, wakicheza huko Romania, walitoka nyuma kwa bao moja na kuifunga CFR Cluj kwa bao zote mbili kufungwa na Robin van Persie ambae alipiga bao hizo kwa ushirikiano mkubwa na Wayne Rooney ambae jana ilikuwa ndiyo Mechi yao ya kwanza kuanza Mechi pamoja.


Huko Turin, Italy, Wakongwe wa Ulaya Juventus jana waliweka rekodi mpya Ulaya ya kutoka sare 8 mfululizo kwenye Mashindano ya Klabu Ulaya walipotoka 1-1 na Shakhtar Donetsk.


Valencia waliifunga Lille bao 2-0 na kuifanya Klabu hiyo ya Ufaransa ifungwe mara mbili mfululizo kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu huu.


Jana Celtic walivunja ile rekodi yao ya kutoshinda ugenini katika Mechi 20 za UEFA CHAMPIONZ LIGI baada ya kuifunga Spartak Moscow 3-2 huku bao la ushindi likifungwa Dakika za mwisho na Georgios Samaras.


Braga walendeleza wimbi lao la kutofungwa ugenini kwa kuichapa Galatasaray bao 2-0 na hiyo ni Mechi yao ya 7 kutofungwa ugenini.


Huko Copenhagen, Chelsea, wakiongoza kwa bao 1-0, walimshukuru Kipa wao Petr Cech kwa kuokoa bao la wazi katika Dakika ya 73 na Dakika chache baadae Luiz akawafungia bao la pili kwa frikiki na kuwafanya Chelsea wapige bao 3 ndani ya Dakika 11 za mwisho na kushinda 4-0 kwa bao za Juan Mata, bao 2, David Luiz na Ramires.

++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumatano Oktoba 3
[Mechi zote Saa 3 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
FC Dynamo Kyiv v GNK Dinamo
FC Porto v Paris Saint-Germain FC
FC Schalke 04 v Montpellier Hérault SC
Arsenal FC v Olympiacos FC
RSC Anderlecht v Málaga CF
FC Zenit St. Petersburg v AC Milan [SAA 1 Usiku]
Manchester City FC v Borussia Dortmund
AFC Ajax v Real Madrid CF
++++++++++++++++++++++++++++++


MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 2]
KUNDI E
Chelsea Pointi 4
Shakhtar Donetsk 4
Juventus 2
Nordsjaelland 0


KUNDI F
BATE Bprisov Pointi 6
Valencia 3
Bayern Munich 3
Lille 0


KUNDI G
Barcelona Pointi 6
Celtic 4
Benfica 1
Spartak Moscow 0


KUNDI H
Manchester United Pointi 6
CFR Cluj 3
Braga 3
Galatasaray 0

No comments:

Post a Comment